Watu
wengi wanaofanya biashara za huduma, hasa za ushauri au mafunzo, huwa
wanaanza kutoa huduma hizo bure ili watu wawajue. Ni vigumu sana kuanza
kwa kuwachaji watu fedha ndiyo uwashauri au kuwafundisha mambo
mbalimbali.
Hivyo
mtu anapoanza kutoa huduma zake bure, watu wengi wanamfuatilia na
kujifunza au kunufaika na huduma hizo kama ni za ushauri au nyinginezo.
Sasa
mtu anaweka juhudi kubwa kutengeneza wafuasi wengi, akiwa na lengo
kwamba watu wanaomfuatilia wanapokuwa wengi na wengi zaidi kuhitaji
huduma zake, basi anaweza kuwatoza ada na kutengeneza kipato.
Lakini
unapofika wakati wa kuwaambia watu wakulipe ili kuendelea kupata huduma
ambazo umekuwa unawapa bure, wengi huwa wanaogopa. Wengi wanajenga hofu
hii pale wanapoanza kuwaambia watu kuhusu malipo na watu hao
wakawaambia hawakutegemea kulipia ushauri au mafunzo yanayotolewa.
Watu
wengi ambao wamekuwa wananufaika na mafunzo hayo ya bure watapinga sana
pale mtu aliyekua anatoa mafunzo hayo bure anapoanza kutoza ada. Na
hili limekuwa linawafanya wengi kushindwa kuendelea na huduma zao na
hivyo huduma hizo zinakufa.
Nikuambie
leo rafiki yangu, kama unaendesha huduma yoyote ile, iwe ni ushauri,
uandishi, ukocha, au huduma ya kiimani, lazima ujue kwamba ili huduma
hiyo iendelee unahitaji njia ya kukuingizia kipato. Hivyo basi usiogope
kuwatoza watu fedha pale wanapohitaji huduma zaidi kutoka kwako.
No comments:
Post a Comment