Biashara
zinazofanikiwa huwa zina upekee ambao haupo kwenye biashara nyingine
yoyote ile. Hata kama kwa nje biashara hiyo inaonekana kufanana na
nyingine, lakini kwa ndani ipo tofauti kabisa. Na utofauti huo wa ndani
ndiyo unaoifanya biashara ifanikiwe sana.
Kuna
vitu viwili ambavyo vinatofautisha biashara yoyote ile, vitu hivyo ni
misingi au maadili ya biashara na kusudi la biashara. Misingi ni kile
ambacho biashara inasimamia, ile miiko ambayo biashara inasimamia katika
uendeshaji wake. Na kusudi la biashara ni ile sababu ya biashara
kuwepo, kile kitu cha tofauti ambacho biashara hiyo inafanya kwa wateja
wake.
Vitu
hivi viwili, miiko na kusudi ndiyo DNA ya biashara yoyote ile. Hivi
ndiyo vinaifanya biashara iweze kusimama licha ya kuwepo kwa changamoto
mbalimbali. Kama ambavyo mtu akikatwa mkono hazai mtoto aliyekatika
mkono, ndivyo hivyo pia biashara inaweza kuendelea vizuri licha ya
changamoto za nje, kwa sababu msingi wa ndani ni imara.
Kwa
biashara unayofanya au kutegemea kufanya, anza kujiwekea msingi au
miiko ambayo utaisimamia kwenye biashara hiyo. Kisha jua kusudi la
biashara hiyo kuwepo, inatatua tatizo au kutimiza mahitaji gani ambayo
watu wanayo. Ukiwa na vitu hivi viwili, utakuwa na biashara yenye
mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment