Showing posts with label MATUKIO YA KUTISHA. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO YA KUTISHA. Show all posts

Wednesday, September 28, 2016

MSHUKIWA WA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA AFURUSHWA MAREKANI



Mshukiwa wa mauaji ya kimbari Rwanda afurushwa Marekani
  • 27 september  2016

Marekani imemrudisha nyumbani msomi mmoja wa Rwanda anayetuhumiwa kuwa mtu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994.
Kufurushwa kwa Leopold Munyakazi kunajiri baada ya kupoteza kesi ya kupata uhifadhi nchini Marekani.

Anatuhumiwa kwa kuvaa majani ya mgomba wakati wa mauaji hayo ya kimbari ili kujitambulisha kuwa raia wa kabila la Hutu,mbali na kupanga mashambulio ya usiku katika nyumba za familia za watu wa kabila la Tutsi .
Bwana Munyakazi ,aliyewahi kuhudumu kama profesa wa chuo kikuu amekana madai hayo.

Takriban Watutsi 800,000 na watu wa kablila la Hutu wenye ustani waliuawa na wapiganaji wa Kihutu katika kipindi cha siku 100 pekee mwaka 1994.


 


Mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda 

BBC   SWAHILI