Showing posts with label BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Show all posts
Showing posts with label BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Show all posts

Wednesday, July 21, 2021

BIASHARA YA GENGE : JINSI YA KUIENDESAHA NA KUFANIKIWA.

Rafiki yangu mpendwa,
Nimekuwa naamini na kusema hili mara kwa mara na nilirudie tena hapa, kukosa mtaji siyo sababu ya kushindwa kuingia kwenye biashara. Ni kisingizio tu.

Sasa visingizio vyote huwa ni vya uongo, kwa sababu vinaficha kile ambacho mtu hataki kukikabili.

Wengi wanaotumia kisingizio cha mtaji, hawapo tayari kuukabili ukweli kwamba ni wavivu, wazembe, wasio tayari kujitoa na wanaopenda mazoea. Ni vigumu sana mtu kukiri una tabia hizo, hivyo kisingizio cha mtaji au muda kinakuwa rahisi.

Kwa zama tunazoishi sasa, hakuna kinachoweza kumzuia mtu aliyejitoa kweli kuingia kwenye biashara. Siyo wazo, siyo mtaji na wala siyo muda.
Kinachomzuia mtu hakitoki nje, bali kipo ndani yake.
Na yule ambaye hana kizuizi cha ndani, anaweza kuyafanya makubwa mno.




Chukua mfano wa biashara ya genge la mahitaji muhimu ya kila siku kwenye familia.
Ni biashara yenye uhitaji, kwa sababu watu kila siku wanakula.
Ni biashara unayoweza kuanza kwa mtaji kidogo.
Ni biashara ambayo huhitaji kuwa na eneo la gharama kubwa kuifanyia.
Na ni biashara ambayo haina vitu vingi, hivyo unaweza kuisimamia vizuri.

Hii ni biashara ambayo mtu ambaye hana shughuli nyingine ya kufanya anaweza kuianzisha, akaiendesha vizuri na ikawa sehemu ya yeye kupiga hatua na kuelekea kwenye biashara kubwa zaidi.

Unapochagua kufanya biashara kama hii, unapaswa kuifanya kwa tofauti, ili ikue na kuweza kuzalisha biashara nyingine kubwa zaidi.

Huenda unawajua wauza genge ambao miaka yote unawaona wakiwa pale pale. Siyo kwamba biashara hailipi, ila wanaifanya kwa viwango vya chini.

Kwenye makala hii unakwenda kujifunza jinsi ya kuifanya biashara ya genge kwa viwango vya juu sana na ikawa na manufaa makubwa kwako.

Kabla hatujaingia kwenye ushauri, tusome aliyotuandikia msomaji mwenzetu aliyeomba ushauri kwenye hili.

“Nahitaji kufungua genge la matunda na mboga mboga napenda kuelimishwa namna ya kuboresha iliniweze kukuza biashara yangu na wateja wavutiwe na huduma yangu.” – Hussein B. M.

I. MAONO MAKUBWA.
Anza kidogo lakini fikiri kwa ukubwa. Japo unafanya biashara ya genge, kwenye fikra zako usione genge, bali ona biashara kubwa kabisa.
Ona ukiwa na maduka mengi ya kuuza mahitaji hayo ya msingi na ona ukifanya kwa kiwango kikubwa zaidi.
Ni maono makubwa unayokuwa nayo ndiyo yanakusukuma kupiga hatua kubwa pia.
Tunapata kile tunachoona, hivyo kuwa na maono makubwa na jisukume kuyafikia.

II. BIDHAA BORA.
Kwenye biashara ya genge wateja wanaangalia vitu vikuu viwili, bidhaa bora na kwa bei nafuu. Pambana kuwapatia wateja vitu hivyo viwili na watakuwa wako kwa muda mrefu.
Chagua bidhaa zilizo bora kabisa ndiyo uweke kwenye biashara yako.
Jua maeneo unayoweza kupata bidhaa hiyo bora kwa bei nafuu ili pia uweze kuwauzia wateja wako kwa bei nzuri.
Jiwekee viwango vya ubora wa bidhaa utakazouza ili wateja waweze kujenga imani kwako na kwa biashara yako.

III. ENEO ZURI.
Biashara yako inapaswa kuwa eneo ambalo ni rahisi kuwafikia wateja wako na hata wateja kuifikia pia.
Kwa kuwa unachouza ni mahitaji muhimu ya maisha ya kila siku, biashara itafanya vizuri pale inapokuwa eneo lenye watu wengi.
Lakini pia mazingira ya eneo lako la biashara yanapaswa kuwa safi na mazuri, yamfanye mteja aiamini na kuithamini biashara yako.
Wengi wanaofanya biashara ya genge hawaweki maeneo yao ya biashara kwenye mwonekano mzuri, ukifanyia kazi hilo unajitofautisha kabisa na wengine.

IV. HUDUMA BORA KWA WATEJA.
Wahudumie vizuri saba wateja wako ili waweze kurudi tena na tena. Wasikilize kwa umakini na wajali pia. Jua mahitaji yao na uwatimizie.
Usiuze tu na kuishia hapo, jenga mahusiano mazuri na wateja wako na hayo yataiwezesha biashara kukua zaidi.
Pale wateja wanapopata huduma nzuri, wanaendelea kuja na wanawaleta wengine pia.

V. KUWEKA MAFUNGU.
Unayajua mahitaji ya wateja wako, unaweza kutengeneza mafungu ya vitu vinavyonunuliwa kwa pamoja na kisha kumshawishi mteja anunue kama fungu badala ya kununua kimoja kimoja.
Kumsukuma kuchukua hatua, hakikisha bei ya fungu inakuwa na unafuu kuliko mteja akinunua kimoja kimoja.
Njia hii itakuwezesha kuuza zaidi kwa wateja ambao tayari unao, ambao ni wateja wazuri tayari.

VI. KUWAFIKIA WATEJA.
Usisubiri tu wateja waje, badala yake watuate kule walipo. Watu sasa wametingwa na mambo mengi wanaweza kusahau kabisa hata uwepo wako.
Hivyo watembelee wateja wako maeneo walipo na kuwashawishi kuja kununua.
Hapa pia unaweza kutoa huduma ya mteja kuagiza na kupelekewa bidhaa zake.
Na kama umeziweka bidhaa kwa mafungu na bidhaa zako ni bora, mteja anaagiza na kupelekewa, akijua anapata anachotaka na ambacho ni bora pia.

VII. KUWASILIANA NA WATEJA.
Omba mawasiliano ya wateja wako na wasiliana nao mara kwa mara.
Unajua wateja wa genge wanapanga mahitaji yao ya siku asubuhi. Unaweza kuwatumia ujumbe asubuhi kuwasalimia na kuwaomba oda pia. Mteja anapopata ujumbe wako, anakufikiria kwa muda mrefu na hilo linamshawishi kuja kununua kwako.
Tumia kila sababu na ushawishi kupata mawasiliano ya wateja wako na wasiliana nao kwa njia ambayo siyo ya usumbufu kwako.

VIII. KUWEKA AKIBA.
Kwa lengo lako la kufika kwenye mafanikio makubwa kibiashara, unapaswa kuweka akiba kwenye kila faida unayoingiza kwenye biashara yako.
Wakati biashara inafanya vizuri, usibweteke na kuona mambo yataenda hivyo wakati wote.
Weka akiba ambayo itakusaidia wakati biashara haiendi vizuri.
Akiba hiyo ndiyo itakusaidia kwenye ukuaji wa biashara yako.

IX. KUKUZA BIASHARA.
Kwa kuwa una maono makubwa ya biashara yako, kila wakati angalia fursa za ukuaji zaidi.
Kila wakati piga hatua kuikuza biashara yako zaidi.

X. KUJIFUNZA KILA SIKU.
Kujifunza kila siku ni hitaji muhimu la ukuaji wa biashara yako.
Kila siku hakikisha unajifunza kitu kwenye kuikuza biashara yako.
Biashara inahitaji ubobezi maeneo mbalimbali kama masoko, mauzo, fedha, ushawishi na uongozi.
Soma vitabu mbalimbali vya biashara yako na  unayojifunza yafanyie kazi.

Tuesday, June 15, 2021

JINSI YA KUPATA NA KUTUNZA WATEJA KWENYE BIASHARA YAKO.

Rafiki yangu mpendwa,
Kila ninapopata nafasi ya kushauri au kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, huwa nawauliza kama wanajua dhumuni na malengo ya biashara zao.

Majibu ambayo huwa napata yanaonesha wazi kwamba wengi hawajui tofauti ya dhumuni na lengo la biashara zao.
Wengi hujiona wapo kwenye biashara ili wapate faida.

Ni fikra na mtazamo huo ndiyo vimekuwa kikwazo kwa ukuaji wa biashara zao. Kama biashara inachoangalia ni kuingiza faida pekee, lazima itapoteza wateja kwa kiasi kikubwa sana.



Dhumuni la biashara linapaswa kuwa ni kutengeneza na kutunza wateja. Lakini lengo kubwa la biashara linapaswa kuwa kutengeneza faida. Ni kupitia wateja ndiyo biashara inaweza kuingiza faida.
Hivyo kwa kuanza na wateja, biashara itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutengeneza faida nzuri.

Biashara nyingi huwa zinashindwa kwa sababu hazina wateja wa kutosha kuziwezesha kujiendesha kwa faida. Kwenye makala ya leo ya ushauri wa changamoto tunakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza na kutunza wateja kwenye biashara na iweze kufanikiwa.

Wasomaji wenzetu waliotuandikia kuomba ushauri kwenye hili walikuwa na haya ya kusema;

“Biashara yangu inapoteza wateja kila siku haikui zaidi ya kumaliza pesa zangu za kubrandy nimefungua Min Juice bar huduma na bidhaa tunazozalisha ni nzuri na bora sana lakini tatizo ni nini?” – Victor V. G.

“Sehemu nilipo weka biashara sio chumba cha njee ni ngum kufikiwa na wateja nifanye nini ili niweze kufikiwa na wateja na kujulikana pande zote” – Laban H.

Changamoto hizo mbili linamlenga mteja, moja kupata mteja na ya pili kumtunza asipotee. Tutayajadili haya mawili kwa kina.

Kupata wateja wa biashara.

Ili kupata wateja kwenye biashara yako, lazima kwanza uchague ni wateja wa aina gani unaowalenga, lazima ujue sifa zao kabisa.
Kwa bidhaa au huduma unayouza, jua ni watu gani unaowalenga na jua sifa zao muhimu.
Jua matatizo au mahitaji waliyonayo ambayo biashara yako inatatua.
Jua uwezo wao wa kuweza kumudu gharama ya unachouza.
Jua wanakopatikana na njia gani ya kuweza kuwafikia.

Ukishazijua sifa za wateja wa biashara yako, usiwasubiri waje kwenye biashara, bali wafuate kule walipo.
Uzuri wa zama hizi siyo lazima biashara yako iwe eneo linaloonekana ndiyo ipate wateja.
Kwa kuwa na mkakati mzuri wa masoko unaweza kuwafikia wateja kule waliko, iwe ni ana kwa ana au kwa mawasiliano.
Usifanye biashara kizamani kusubiri waje, bali toka na watafute wateja.
Tayari umeshajua matatizo au mahitaji yao na tayari una suluhisho linalowafaa, ni wewe kuwafikia na kuhakikisha wanajua uwepo wa biashara yako na kushawishika kuja kwenye biashara yako.

Baada ya kuwashawishi wateja na wakaja kwenye biashara yako, unapaswa kuwashawishi wanunue.
Usiwakubalie kirahisi pale wateja wanapokuambua wameshaona na watakuja siku nyingine kununua, hapo wanakukimbia kirahisi.
Washawishi wanunue kwa kuwahakikishia kwamba hawatapoteza fedha zao wanapofanya maamuzi ya kununua.
Kumbuka wateja wako wametafuta fedha zao kwa maumivu na hawapo tayari kutengana nazo kirahisi. Lazima uwape uhakika kwamba wakitumia fedha zao kwenye biashara yako yatakuwa ni matumizi bora kuliko mengine wanayoweza kufanya kwa fedha hizo.

Mjue mteja, mfikie mteja na kumshawishi kuja kwenye biashara na anapofika mshawishi anunue, hizo ni hatua tatu kubwa za kupata wateja kwenye biashara yako.

Kutunza wateja wa biashara wasipotee.

Kama mteja hajanunua kwenye biashara yako, huyo siyo mteja wako. Hata kama amekuahudi atanunua, kama bado hajanunua, usimhesabie ni mteja.
Mteja akishanunua kwako mara moja, ni rahisi kununua tena kwa mara nyingibe kulimo kwa mteja ambaye hajanunua kabisa.
Mteja ambaye ameshanunua, kuna imani ambayo tayari ameshaijenga kwenye biashara.

Wanapokosea wafanyabiashara wengi ni kuhangaika kukimbizana na wateja wapya huku wakiwasahau kabisa wateja ambao tayari walishanunua.
Hii ni sawa na kuacha dhahabu ya uhakika uliyonayo ndani na kwenda kuhangaika kutafuta dhahabu sehemu ambayo huna uhakika nayo.

Sisemi uache kutafuta wateja wapya, ila ninachosema ni juhudi unazoweka kutafuta wateja wapya, weka juhudi za kiwango hicho hicho kuwatunza wateja ambao tayari wameshanunua.
Kuwatunza wateja ambao wameshanunua kwako, zingatia haya muhimu.

Moja ni kuwapatia huduma bora kabisa kwenye biashara yako. Wape wateja wako huduma bora ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote. Hilo litawasukuma kurudi tena kwako kwa sababu wanajua watapata ambacho hawawezi kupata pengine.
Kama hakuna tofauti ya wanachopata kwako na wanachopata kwa wengine, hawatajisumbua kurudi tena kwako.

Mbili ni kuendelea kuwasiliana nao mara kwa mara. Kila mteja ambaye ameshanunua kwako, hakikisha unakuwa na mawasiliano yake. Uzuri kila mtu ana njia mbalimbali za mawasiliano, kuanzia namba za simu, barua pepe na mitandao ya kijamii.
Mteja akishanunua kwako hawezi kuwa mgumu kutoa mawasiliano yake, hivyo muombe akupe mawasiliano hayo na yatumie kuwasiliana naye.
Siyo tu unatumia kumtangazia biashara yako, bali kumjulia hali, kumtumia salamu mbalimbali kulingana na sikukuu au matukio mbalimbali.
Kadiri unavyowasiliana na wateja wako, ndivyo wanavyokufikiria wewe na biashara yako na kuja kwako pale wanapokuwa na uhitaji.

Tatu ni waombe wakuletee wateja zaidi. Kama mteja ameridhika na huduma unazompa, na hilo utalijua kwa shuhuda atakazokupa yeye mwenyewe, muombe awaalike watu wake wa karibu nao waje kupata huduma hizo.
Mteja anapochukua hatua ya kuwaalika wengine, yeye mwenyewe ataendelea kuja maana hawezi kuwaleta watu halafu yeye asije.
Kwa kumshawishi na akakubali kuleta wateja zaidi, anakuwa amechagua kuendelea kuwa mteja wako kwa muda mrefu zaidi.
Na mteja anapokuletea wateja zaidi, hakikisha unawapa huduma bora kabisa ili asipoteze imani yake kwa wale aliowashawishi kuja kwenye biashara yako.

Utoaji wa huduma bora na za kipekee, mawasiliano ya mara kwa mara na wateja kukuletea wateja zaidi ni njia bora za kuwafanya wateja kuendelea kuwa kwenye biashara yako.

Kama mfanyabiashara jua dhumuni na lengo la biashara na weka juhudi kubwa kwenye kutafuta wateja wapya wa biashara yako, na juhudi za aina hiyo pia kwenye kuwatunza wateja ambao tayari wameshanunua.
Kwa namna hiyo biashara itakuwa na wateja wengi na kuweza kuingiza faida nzuri.

 

Saturday, May 8, 2021

KWA NINI WENZAKO WANAFANIKIWA NA WEWE UNABAKI ULIPO ??

Rafiki yangu mpendwa,

Huenda hili ni swali umekuwa unajiuliza kwa muda mrefu.

Unapoona wenzako ambao mmeanza kazi pamoja, kazi ambayo ni sawa na malipo yanalingana, ila wao wanapiga hatua huku wewe unabaki nyuma.

Au ni kwenye biashara ambapo unaona wengine wanaofanya biashara ya aina hiyo na mlioanzia kwa kiwango sawa wanapiga hatua wewe unabaki ulipo.

Watu wa kawaida, ambao hawawezi kufanikiwa huwa wanatafuta sababu za kuhalalisha hali zao.

Wanajiambia wale waliopiga hatua wamependelewa au wamepata bahati au kuna njia zisizo sahihi wanazotumia.

Ni kweli hivyo vinaweza kuchangia kwa namna fulani, lakini siyo sababu hasa.

Wale waliopiga hatua kuliko wewe kuna mambo mawili yanayowatofautisha na wewe ambayo kama hutayajua na kuyafanyia kazi, utaendelea kubaki hapo ulipo.

Jambo la kwanza ni namna wanavyofikiri.

Kuna watu wanapewa urithi na wanaweza kuuendeleza na kufanikiwa. Wakati kuna wengine wanapewa urithi na kuupoteza wote.




Kinachowatofautisha watu hau siyo wanachopewa, bali namna wanavyokichukulia.

Namna mtu anavyofikiri inaathiri sana yale anayofanya kwenye maisha yake. Wanaopiga hatua wanafikiri kwa uchanya, uwezekano na ukuaji.

Kwenye fikra zao wanaona picha kubwa ambayo wanapambana kuifikia. Wanaamini bila ya shaka yoyote kwamba watafikia picha hiyo.

Na pale wanapokutana na vikwazo mbalimbali, wanajua siyo mwishi wa safari, bali wanaimarishwa ili waweze kupokea makubwa.

Wasiofajikiwa wao hufikiri kwa udogo, uhasi na kutokuwezekana. Hawana picha kubwa, wanaona mengi ni mabaya na wanapokutana na changamoto wanaona ni mwisho.

Kama hutabadili namna unavyofikiri hutaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Jambo la pili ni namna watu wanavyofanya.

Kama watu wawili wanafanya kazi au biashara ya aina moja na mmoja akapiga hatua kuliko mwingine, ukimuangalia utaona wazi kuna vitu anafanya tofauti.




Wanaofanikiwa na kupiga hatua wanafanya mambo yao kwa namba ya tofauti kabisa.

Wana viwango walivyojiwekea katika kufanya, viwango ambavyo ni vya tofauti kabisa na wengine.

Wanakwenda hatua ya ziada na kutoa thamani kubwa tofauti na wanavyotegemewa kufanya.

Wanajua mafanikio ni mbio za muda mrefu na hivyo hujipanga vizuri kwenye ufanyaji wao.

Kamwe hawaahirishi yale waliyopanga kufanya, wana nidhamu kubwa ya kutekeleza kama walivyopanga.

Wale wasiofanikiwa huwa wanafanya mambo yao kwa mazoea, hawawezi kujituma wenyewe mpaka wasukumwe na ni wazuri sana kwenye kuahirisha yale waliyopanga kufanya.

Kama hutajifunza namna waliofanikiwa wanavyofanya na wewe kufanya kwa namna hiyo, utaendelea kubaki pale ulipo.

Habari njema kwako rafiki yangu ni una nafasi nzuri ya kujifunza kwa kina namna ya kufikiri na kutenda ili uweze kufanikiwa sana.

JIUNGE   NA  DARASA  ONLINE  --UJIFUNZE    KWA   KINA    NA  VITENDO

JIFUNZE  ,ELIMIKA   NA   CHUKUA  HATUA.

TUWASILIANE  SASA    KWA  MAELEKEZO  ZAIDI

NA  KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

WhatsApp  + 255 716  924 136  /   +  255  755 400 128  /  + 255 688 361  539

EMAIL : japhetmasatuy@gmail.com




JIFUNZE HAPA : JINSI YA KUZIVUTA FURSA NA KUZITUMIA NDANI YA MUDA MFUPI.

Unakwama Wapi Mpaka Sasa Hujui Jinsi Ya Kuzivuta Fursa?

Huzioni fursa lakini wenzako wanaziona na kuzitumia je, unajua tatizo ni nini?

Ulichofichwa kwa muda mrefu leo unakwenda kukifahamu na kukitumia ipasavyo.

Angalia huu mfano hapa chini;

MARAFIKI  WAWILI  WAKIVUA.

Kulikuwa kuna wavuvi wawili ambao ni marafiki wa karibu.

Walitumia wikiendi kuvua samaki pamoja.

Pale wanapokuwa wametingwa na shughuli zao na familia zao ilikuwa ngumu kuonana.

Ilikuwa ni siku ya juma mosi waliamua kuongozana  pamoja karibu na ziwa kufurahia shughuli za uvuvi kwenye siku yao.

Wote walibeba nyenzo muhimu za uvuvi pamoja na vikorombezo vingine kwa ajili ya kupikia samaki.

Walifika kwenye bwawa.

Walikaa kwa mbali na kuanza kuwinda samaki.

Mvuvi wa kwanza alipata samaki mkubwa na mzuri ndani ya dakika chache.

Alifurahi akamuweka samaki ndani ya jokofu la plastiki lenye mabonge ya barafu na kumuhifadhi.

Alitumia muda kidogo kuwanasa samaki wengine wachache.

Aliamua kuwapika wachache,

Pia aligandisha samaki wachache na wengine aliwaacha kwa ajili ya kuwapeleka nyumbani.

Ilichukua zaidi ya li saa wakiwa wanavua.

Mvuvi wa kwanza  akamfuata mvuvi wa pili na kumuuliza kama anahitaji msaada.

Mvuvi wa pili akamjibu hapana.

Dakika chache , mvuvi wa pili anakamata samaki mkubwa.

Ata hivyo, alimrudisha tena ndani ya ziwa.

Mvuvi wa kwanza alishangazwa na iko kitendo.  

Mvuvi wa pili akawa ana kamata samaki wakubwa , lakini anawarudisha wote ndani ya maji.

Mvuvi wa kwanza anachukizwa sana na iko kitendo cha mwenzake, anamuuliza kwa hasira “ Una wazimu?

Kwanini unawarudisha samaki wote ndani ya maji?

Walikuwa wazuri na wakubwa.

Mvuvi wa pili anajibu, “ Najua walikuwa wakubwa, bali sina kikaango kikubwa cha kupikia hao samaki wakubwa.

Kwa hiyo natafuta samaki wadogo ambao wataenea kwenye kikaango changu kidogo.

Akasema mungu ananisumbua sana leo.

Baada ya kusikia hilo, mvuvi wa kwanza anashangazwa na hilo jibu.

Anamshauri mvuvi wa pili kumkata samaki mkubwa vipande vipande ili aweze kuenea kwenye kikaango na wapike bila shida.

Somo;

Watu wengi wapo kama mvuvi wa pili.

Wanazungukwa na fursa nyingi lakini wanashindwa kuzitumia , na hii ni kwa sababu hawazioni  na hawajui jinsi ya kuzivuta.

Wanachokiona ni vikwazo, uchache, matatizo na hatari ya kupoteza.

Ata wewe mwenyewe unajishangaa unazungukwa na fursa nyingi lakini unashindwa kuziona na kuzitumia, lakini wenzako wanaziona na kuzitumia.

Na hiki ndicho kinachowatofautisha matajiri na maskini.

Matajiri wanajua jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ipasavyo lakini masikini wanafanya kinyume chake.

Ata wewe leo hii unaweza kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.

Kwa kusoma na  kujifunza , unakwenda kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.

Unakwenda kufahamu vizuizi vinavyokuzuia usizione  fursa.

Karibu sana UJIUNGE  NA    " DARASA  ONLINE "--ujifunze  TABIA ZA KITAJIRI na FURSA  MBALIMBALI   ZINAZOKUZUNGUKA  na Mengine  mengi  YANAYOHUSU FALSAFA , SAIKOLOJIA, MAHUSIANO ,

Ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako,

 Kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

 

Kwa  Maelekezo  Tuwasiliane 

NA  KOCHA   MWL.  JAPHET  MASATU

WhatsApp + 255 716 924 136 ,  + 255 755 400 128 

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com

 

JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA ILI LIWEZE KUKULETEA MAFANIKIO MAKUBWA SANA---NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU---( PDF )

JINSI YA KUPATA MTAJI WA BIASHARA NA VYANZO VYAKE---NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU-----( PDF )

Saturday, September 5, 2020

JINSI YA KUKUZA BIASHARA KUTOKA WATU 10 MPAKA WATU 10,000 KATIKA KAMPUNI.

Jukumu La Mtendaji Mkuu (CEO)

Kwenye vitabu vingi vya biashara, majukumu ya CEO yamekuwa yanaainishwa kuwa;

1. Kuweka mwelekeo na mkakati wa kampuni na kuuwasilisha kwa wafanyakazi, wateja na wawekezaji.

2. Kuajiri, kufundisha na kutengeneza utamaduni sahihi kwenye kampuni.

3. Kukusanya mtaji na kuugawa kwa usahihi kwenye shughuli za kampuni.

4. Kuwa mwanasaikolojia mkuu wa kampuni, kwa kuwapa wengine moyo pale mambo yanapokuwa magumu.

Kutafuta, Kuajiri Na Kusimamia Vipaji.

Ukuaji na mafanikio ya kampuni unategemea sana watu unaowaajiri kwenye kampuni yako. Ni muhimu uajiri watu sahihi, wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao na hamasa ya kufanya hivyo.

Kujenga Timu Ya Watendaji.

Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya biashara yako ndiyo watendaji kwenye kampuni. Hawa wanahusika kusimamia vitengo vyao ili viweze kuisaidia kampuni kufikia maono yake. Kama mkurugenzi mkuu, utaweza kukuza kampuni yako unapokuwa na timu nzuri ya watendaji.

Kujenga timu bora ya watendaji ni zoezi gumu kwa waanzilishi wachanga, kwa sababu mwanzoni walikuwa wanafanya kila kitu peke yao. Lakini sasa kampuni inakua kwa kasi, hawawezi tena kufanya hivyo. Na hapo bado wengi wanakuwa hawajawa tayari kugatua majukumu yao.

Lakini inafika hatua ambapo kama mwanzilishi huwezi tena kusimamia kila kitu peke yako, kwa sababu majukumu yanayotaka muda wako ni mengi kuliko muda ulionao. Hivyo unakuwa huna budi kujenga timu ya watendaji.

Changamoto kubwa kwenye kuajiri watendaji ni kwamba unapaswa kutafuta watu wenye uzoefu zaidi yako, kitu ambacho siyo rahisi. Lakini unapofanikiwa kuajiri mtendaji wa kwanza vizuri, wanaofuata haitakuwa changamoto kwenye kuwaajiri.

Unapokuwa na watendaji wazuri, mambo mengi kwenye kampuni yanaenda bila ya wewe mwenyewe kuhusika moja kwa moja. Unaona kama ni miujiza maana mambo yaliyokuwa yanakusumbua awali hayakusumbui tena kwa sababu wapo wanaoyafanyia kazi.

Lakini pia kuna wakati makosa yanafanyika kwenye uajiri na mtendaji anayeajiriwa anakuwa siyo sahihi. Hapo msongo unakuwa mara mbili, kwa majukumu yanayokutegemea na mtendaji asiyefaa. Mtendaji wa aina hiyo huwa chanzo cha wafanyakazi wazuri kuikimbia kampuni yako.

Muundo Wa Kampuni Na Ukuaji Wa Kasi.

Muundo wa kampuni kwenye kipindi cha ukuaji wa kasi ni jambo lenye changamoto kwa waanzilishi wasio na uzoefu. Hii ni kwa sababu inakuwa vigumu kuwa na muundo mmoja, kadiri kampuni inavyokua, ndiyo mabadiliko yanayohitajika kwenye muundo.

Masoko Na Mahusiano Ya Umma.

Masoko na mahusiano ya umma (marketing and PR) ni eneo muhimu kwenye ukuaji wa kampuni yoyote ile. Ila kwa kampuni zilizo kwenye hatua ya ukuaji wa kasi, eneo hilo ni muhimu na linapaswa kufanya kwa usahihi.

Mchango wa masoko na mahusiano ya umma ni kujenga jina la kampuni (brand), kutengeneza taswira nzuri kwa umma, kupata kutunza wateja wa kampuni.

Kwenye uchambuzi kamili utajifunza njia bora za kufanya masoko na mahusiano kwa umma ili kampuni iweze kunufaika.

Usimamizi Wa Bidhaa.

Usimamizi wa bidhaa ni eneo muhimu wakati wa ukuaji wa kasi wa kampuni. Hii ni kwa sababu uhitaji unakuwa mkubwa na hivyo kusipokuwa na usimamizi mzuri, bidhaa inaweza isiwe bora au mahitaji ya wateja yasifikiwe.

Usimamizi mzuri wa bidhaa unaiwezesha kampuni kuweka maono makubwa ya bidhaa, mipango ya kufikia maono hayo, mikakati ya kufanyia kazi na hatua za kuchukua.

Usimamizi mbaya wa bidhaa unakuwa fujo kwa kampuni nzima kwani hakuna maono, na mambo hayafanyiki kwa wakati.

Ili kuwa na usimamizi mzuri wa bidhaa, unapaswa kuwa na kitengo mahususi kwa ajili ya bidhaa, kinachosimamiwa na meneja wa bidhaa ambaye anakuwa na ujuzi wa juu kwenye bidhaa husika. Pia unapaswa kutengeneza mchakato sahihi unaofuatwa kwenye kuandaa bidhaa husika.

Fedha Na Uthaminishaji.

Fedha na uthaminishaji ni eneo muhimu kwenye ukuaji wa kasi wa kampuni. Katika kipindi cha ukuaji wa kasi, japo kampuni inaweza kuwa na wateja wengi, lakini inaweza isiwe inazalisha faida. Hivyo kama CEO utahitaji kupata fedha za kuendelea kuendesha kampuni. Huu ndiyo wakati utakaohitajika kuithaminisha kampuni na kisha kukaribisha wawekezaji kuwekeza mitaji yao. Pia unaweza kuiuza kampuni au kuipeleka kwa umma.

Kuungana Na Kununua.

Njia nyingine ya kukuza zaidi kampuni yako ni kuungana na kampuni nyingine ambayo ni kubwa zaidi au kununua kampuni ambayo ni ndogo.

Kuungana na kununua (Mergers & acquisitions) kunaiwezesha kampuni kupata bidhaa, teknolojia, timu na hata kuondoa ushindani kwenye soko.

 

Wednesday, August 19, 2020

WATEJA WA ZAMANI NI LULU ?? WEKA KUMBUKUMBU ZAO . !!!

 Nguzo muhimu katika biashara yoyote duniani ni wateja. Ninaweza kusema kwamba biashara inafanikishwa na watu wawili; yaani mfanyabiashara ambaye ndiye anauza bidhaa au huduma na wa pili ni mteja ambaye ananunua bidhaa. Kama unafanya biashara ambayo wateja wapo, tunasema biashara hiyo inalipa lakini kama wateja hawapo tunasema biashara yako hailipi. Kwahiyo, kuendelea kwa biashara yako ni
wateja. Kwenye biashara kuna aina mbili za wateja, ambao ni wateja wa zamani na wateja wapya. 

Kwa jinsi hali ilivyo huku mitaani kwetu, ni kwamba wafanyabiashara wengi wanajali zaidi wateja mpya. 

Mteja mpya anaonyeshwa kila aina ya upendo kiasi cha kumkatishatamaa mteja wa zamani endapo ikitokea wote wawili wakawepo pamoja eneo la biashara. 

Hali hii ya kutengwa kama mteja wa zamani imenitokea mara nyingi na kunifanya niamini kwamba kadiri unavyozidi kununua bidhaa mara nyingi kutoka kwa mfanyabiashara fulani ndivyo anavyoacha kukujali. 

Kiashiria mojawapo ni wakati mwingine mteja wa zamani anapouziwa vitu kwa bei tofauti na Yule mteja mpya. Yaani ni ajabu wateja wapya wanapunguziwa wakati wale wa zamani wanaonunua vitu mara kwa mara wanapandishiwa bei. 

Wakati mwingine baadhi ya wafanyabiashara wanakupunja wewe mteja wao wa zamani kupitia vipimo hasa kwa bidhaa kama sukari, nyama, mchele n.k. 

Ukweli ni kwamba, mteja wa zamani ni LULU. Unapashwa kumtengenezea mazingira rafiki kwa kuhakikisha unampatia unafuu kadiri mtakavyozidi kukaa pamoja kibiashara. Ikiwa utazidi kumjali na yeye atazidi kuwa na sababu ya kuendelea kuwa mteja wako daima. 

Kwanini mteja wa zamani? 

Ukizidi kuwajali wateja wa zamani inakusaidia wewe kupata wateja wapya kwa gharama kidogo sana; kuliko ambavyo ungewatafuta wewe mwenyewe moja kwa moja. 

Mteja wa zamani ni mtaji mkubwa” endapo utakaanaye vizuri, na hii nikutokana na ukweli kwamba, anaouwezo wa kukuletea wateja wapya kila mara. 

Mteja wa zamani ni rahisi kumtunza kuliko kupata mteja mpya. 

Sisi wataalamu wa masuala ya masoko tunasema kuwa gharama za kumpata mteja mpya ni mara saba zaidi ya gharama za kukaa na mteja wako wa zamani. 

Mteja wa zamani tayari anakufahamu kwahiyo, akiambiwa juu ya mali mpya hana mud sana wa kuhoji kwasababu tayari anakuamini na hivyo ataweza kuitikia haraka. 

Uzoefu wangu unaonyesha kuwa inachukua muda na nguvu nyingi kumshawishi mteja mpya kukubali bidhaa yako kuliko wa mteja zamani. 

Tayari wewe unafahamu vizuri tabia na mahitaji ya wateja wako wa zamani, kwahiyo inakuwa rahisi kujua namna nzuri ya kutengeneza mkakati wa kuongeza mauzo yako bila kusahau kuwapa kilicho bora. 

Nifanye nini kukuza uhusiano na wateja wangu wa zamani? 
Unachotakiwa kufanya ni kujifunza jinsi ya kujenga na kuimalisha mahusiano na watu hasa wale wanaokuja kununua bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwako. 

Ni muhimu sana kujenga mahusiano ya karibu na kila mteja mpya wakiwemo wale walioletwa na mteja wako wa zamani, lakini jenga uhusiano na kila mmoja peke yake siyo kama kikundi. 

Katika mchakato wa kujenga uhusiano na wateja fanya yafuatayo; 

Badili tabia yako juu ya mahusiano: Tabia yako ya mahusiano na watu wengine ni muhimu sana. Usidhani suala zima la kujali watu litatokea tu siku moja, lazima uzame ndani kwenye tabia yako kwanza. 

Andaa orodha ya majina na namba za simu: Jiwekee utaratibu wa kuwa na orodha ya majina pamoja na namba zao za simu. Ukiwa na orodha ya majina ni rahisi kuwa na kumbukumbu ya nani kanunua nini na kiasi gani mwaka mwezi au mwaka huu. 

Inapofika sikukuu maalum kama Krismas hawa ndio wa kuwapa kipaumbele unapotuma salam za pongezi. Sijui wewe kama uliwahi kumtumia mtu heri ya krismas kwasababu tu ni mteja wako mzuri..kama hujafanya hivyo basi jitafakari na uchukue hatua. 

Toa elimu juu ya bidhaa/huduma: Hakikisha wateja wako wanapata elimu bora juu ya matumizi sahihi ya bidhaa zako, ili waweze siyo tu kununua bali kueneza habari njema kwa wateja wengine. Kadiri utakavyozidi kuwaelimisha ndivyo utakavyozidi kuzalisha wateja wengi ambao ni waaminifu. 

Shirikiana nao shughuli za kijamii: Jaribu kuwa nao karibu kwenye shughuli za kijamii; kama ni kuchangia harusi fanya hivyo, hawa ndio unatakiwa kuwachangia, kama ni misiba hawa unalazimika kuwatembelea na kuwafariji. 

Kwahiyo, kupitia mahusiano yako na wateja, unajikuta umejenga kundi kubwa la marafiki na ndugu mlioshibana. 

Bahati mbaya sana wengi tunashiriki zaidi shughuli za kijamii kwa watu ambao hawana uhusiano wowote na biashara zetu. 

Unahitaji kuwaongeza kwenye orodha wateja wako, ili linapofika suala zima la kushirikiana katika shughuli za kijamii, nao wawe ni sehemu ya watu unaowakumbuka. 

Toa tuzo kwa wateja: Kama unachukua kumbukumbu za wateja vizuri ni rahisi kwako kuona nani amechukua pesa zake kwa wingi kwa katika kipindi cha mwezi, robo, nusu mwaka au mwaka mzima. 

Hapa utakuwa na nafasi ya kujua ni nani umpe tuzo. Tuzo hiyo siyo lazima uwambie, unaweza ukatafuta utaratibu wa kumpongeza au kumpa tuzo. 

Mafano; kutoa mwaliko wa chakula cha jioni au kinywaji nyumbani au hoterini; unaweza kutuma salam za pongezi mfano kupata mtoto, kumaliza shule kwa watoto n.k. 

Wewe uliye na biashara yoyote tambua kuwa unahitaji kuendelea kujifunza mpaka ufike sehemu uone kwamba wateja ndio ndugu namba moja. 
 
KWA   KUJIFUNZA   KWA  MAPANA  NA   MAREFU    JIUNGE  NA   "  DARASA   ONLINE "   KWA  KUWA  MWANACHAMA.
Tuwasiliane  kwa  WhatsApp  + 255 716924136  /   + 255 755  400128  + 255  688  361  539

Ndimi  RAFIKI   NA   KOCHA   MWL.  JAPHET  MASATU , 
DAR  ES  SALAAM , TANZANIA.

 

Monday, August 17, 2020

NI WAKATI GANI WA KUCHUKUA MKOPO WA BIASHARA ILI UWE NA MANAUFAA ?


WAKATI    SAHIHI  WA  KUCHUKUA   MKOPO    KWA  AJILI  YA    BIASHARA .



Kwenye makala hii nitakwenda kushauri mambo matatu ambayo kila mfanyabiashara anapaswa kuyafanyia kazi ili biashara yake iweze kukua.

JAMBO LA KWANZA; WAKATI SAHIHI WA KUCHUKUA MKOPO.

Usichukue mkopo kwenye biashara kwa sababu umeambiwa unakopesheka,

Usichukue mkopo kwa sababu wewe ni mfanyakazi hivyo unaweza kukopa kwa kutumia mshahara wako.

Na usichukue mkopo kwenye biashara kwa sababu umesikia watu wanasema biashara haiwezi kufanikiwa bila mkopo.

Zote hizo ni sababu mbovu za kuchukua mkopo kwenye biashara, ambazo zimewapoteza wengi.

Kabla hujachukua mkopo kwenye biashara, hakikisha imetimiza vigezo hivi vikubwa vitatu;

Kigezo cha kwanza ni biashara inajiendesha kwa faida, yaani tayari biashara inaingiza faida, hivyo unapochukua mkopo unakwenda kukuza faida hiyo zaidi.

Kigezo cha pili ni biashara ina mfumo mzuri wa uendeshaji ambapo kuna vitengo mbalimbali na kila kitengo kina majukumu yake ya kutekeleza. Hata kama uko mwenyewe kwenye biashara, unapaswa kuwa na vitengo hivyo.

Kigezo cha tatu ni matumizi ya fedha za biashara na matumizi yako binafsi hayaingiliani. Yaani fedha ya biashara inakaa kwenye biashara na huitumii kwa namna yoyote ile, una akaunti ya biashara benki ambapo fedha zinaenda huko. Hata kama huna pesa ya kula, hutoi tu kwenye biashara kiholela.

Kama biashara yako haijafikisha vigezo hivyo vitatu, ukichukua mkopo unaiwahisha kufa.

JAMBO LA PILI; MAMBO YA KUZINGATIA PALE UNAPOCHUKUA MKOPO.

Baada ya kuhakikisha kwamba biashara yako imefikia vigezo vya kuchukua mkopo, kwa maana kwamba inajiendesha kwa faida, ina mfumo mzuri na fedha za biashara haziingiliani na matumizi yako binafsi, basi unaweza kuchukua mkopo.

Lakini pamoja na kukidhi vigezo hivyo, mkopo unaweza kuwa hatari kwa biashara kama hutazingatia mambo muhimu katika kuuchukua na kuutumia. Yafuatayo ni mambo matano muhimu ya kuzingatia pale unapochukua mkopo wa biashara.

Moja ni kupanga matumizi ya mkopo huo kabla hujauchukua. Usichukue mkopo kisha ndiyo upangilie unautumiaje. Badala yake iangalie biashara yako kwanza, angalia ni bidhaa au huduma zipi zinazotoka haraka, zina uhitaji na faida yake ni nzuri, hivyo unapochukua mkopo unaenda kuweka kwenye bidhaa au huduma hiyo. Mfano kwenye hardware kama umegundua cement ndiyo inatoka sana na yenye faida na kwa mtaji wako huwezi kununua kwa wingi, unapochukua mkopo basi unawekeza kwenye eneo hilo.

Mbili ni kutokutumia mkopo wote uliouchukua, tumia robo tatu na robo iache kama akiba. Mipango yako ya mwanzo inaweza kuwa siyo sahihi, sasa kama mkopo wote umeshautumia, utajikuta umekwama. Acha kiasi fulani cha mkopo kama fedha taslimu, ili kama ulivyopanga awali mambo hayajaenda hivyo, unakuwa na kiasi cha kukuwezesha kufanya mpango mwingine wa kuokoa hali unayokuwa umeingia.

Tatu ni usitumie mkopo kufanya mambo yasiyozalisha faida, mfano kufanya marekebisho eneo la biashara, kununua samani na mengineyo. Mkopo unarudi kwa riba, hivyo unapaswa kuzalisha faida ambayo ni kubwa kuliko riba unayolipa. Kama mkopo hauzalishi faida, maana yake riba unayoilipa inatoka kwenye mtaji wako, ndiyo maana utamaliza kulipa mkopo na biashara kufa.

Nne ni kuweka nguvu na kujisukuma zaidi, ulipokuwa huna mkopo, hukuwa na gharama kubwa za kuendesha biashara, ukishachukua mkopo, gharama zimeongezeka. Hivyo pia lazima ujisukume sana, pambana kuongeza wateja na kuwashawishi wateja wako kununua zaidi. Usiendelee kuendesha biashara yako kwa mazoea kama wakati huna mkopo.

Tano ni kufuatilia kwa karibu mwenendo wa biashara na marejesho ya mkopo. Usirejeshe tu bila kuangalia biashara inaendaje, kama unafika wakati unakuta marejesho unayofanya ni makubwa kuliko faida unayoingiza, jua mapema kabisa kwamba unamega mtaji wa biashara. Hivyo anza kuchukua hatua mapema na siyo kusubiri mpaka umemaliza kurejesha mkopo huku biashara imekufa. Ukishagundua marejesho ni makubwa kuliko faida una mengi ya kufanya, kwa upande wako ni kukazana kuongeza mauzo, kwa upande wa mkopo unaweza kwenda kuongea nao wapunguze kiwango cha marejesho unachofanya.

Ukizingatia haya matano pale unapochukua mkopo, utainufaisha biashara yako na kuiwezesha kukua zaidi.

JAMBO LA TATU; UFANYE NINI PALE UNAPOKUWA HUNA VIGEZO VYA KUCHUKUA MKOPO.

Wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati wamekaririshwa na kuamini kwamba njia pekee ya kupata mtaji wa kuanza na kukuza biashara ni kuchukua mkopo. Ndiyo maana utasikia kilio cha wengi kwamba hawakopesheki au hawana dhamana ya kupata mkopo.

Usikimbilie kuchukua mkopo kama bado hujakidhi vigezo vya kuchukua mkopo ambavyo tumejadili hapo juu.

Swali ni je ufanyeje ili kukuza biashara yako wakati huwezi kuchukua mkopo? Kuna mengi ya kufanya, hapa kuna matatu ya kuzingatia.

Moja ni kuanza biashara kwa akiba zako wewe mwenyewe. Kwenye njia nyingine ulizonazo za kuingiza kipato, basi weka akiba kwenye kila kipato na akiba hiyo iwekeze kwenye biashara, anza kidogo na endelea kukua. Kila mwezi jiwekee kiango ambacho utawekeza kwenye biashara yako kutoka kwenye njia zako nyingine za kuingiza kipato.

Mbili ni kutokuondoa fedha kwenye biashara kabisa, acha biashara ijiendeshe yenyewe kwa kutokuingilia na kutoa fedha kwa matumizi yako binafsi. Unapaswa kuwa na nidhamu kubwa sana ya kutenganisha matumizi yako binafsi ya fedha na fedha za biashara. Zione fedha za biashara kama za mtu mwingine kabisa na usiwe na mazoea ya kutumia biashara kutatua shida zako.

Tatu ni kuanza na biashara nyingine ili kutengeneza mtaji wa kwenda kuanza biashara ya ndoto yako. Kama biashara unayotaka kuanzisha inahitaji mtaji mkubwa ambao huna, anza na biashara nyingine unayoweza kuanza kwa mtaji kidogo kisha tumia biashara hiyo kutengeneza mtaji wa kuingia kwenye biashara ambayo ndiyo unataka kufanya. Hili ni jibu kwa wale watakaokuwa wamesoma namba moja hapo na kusema sina ajira nitatengenezaje mtaji au kuendesha maisha bila kutegemea biashara. Fanya chochote unachoweza kuhakikisha kwanza unaingiza kipato, omba hata kuwa wakala wa mauzo kwenye biashara za wengine ambapo watakulipa kamisheni, pambana kuuza na tengeneza mtaji wako ili baadaye uwe na biashara yako.

Kuanzisha na kukuza biashara ili ikupe mafanikio kunahitaji kazi, msimamo na uvumilivu. Hakuna njia ya mkato inayoweza kuondoa mahitaji hayo matatu. Wengi wamekuwa wanakimbilia kuchukua mkopo wakifikiri ni njia ya mkato na kinachotokea ni kuua kabisa biashara zao.

Zingatia haya uliyojifunza kwenye ushauri huu, yafanyie kazi na biashara yako itapata manufaa makubwa.

Wednesday, May 20, 2020

HAMISHA TABIA ZA AJIRA KWENDA KWENYE KUJIAJIRI UTAFANIKIWA SANA.

Tabia hizo kumi ni kama ifuatavyo;
(1).UNAENDA  KILA SIKU.

Kila siku ambayo ni ya kazi, unaenda kazini. Haijalishi kama unajisikia au hujisikii, umechoka au hujachoka, ni siku ya kazi na unaenda kazini. Na ili kuhakikisha unaenda, sehemu za kazi kuna daftari au mashine ya kuweka sahihi, ili kuthibitisha kwamba kweli umefika kazini.

Unapojiajiri, hakikisha kila siku ya kazi ambayo umejipangia kulingana na kile unachofanya basi unaenda kwenye eneo lako la kazi. Japokuwa una uhuru wa kwenda au kutokwenda, usiutumie kabisa uhuru huo, wewe nenda, iwe unajisikia au hujisikii, iwe umechoka au la. Chukulia kuna bosi anakusubiria pale, na hawezi kukuelewa kama hujaenda.
(2). CHANGAMOTO  ZA  MAISHA  HAZIINGILII  KAZI.
Usiku umegombana na mke wako au mume wako, asubuhi unaamka na kujiandaa kwenda kazini. Hukai nyumbani na kumwambia bosi leo huendi kwa sababu kuna ugomvi nyumbani. Umeamka una mafua makali unajiandaa na kwenda kazini, husemi mafua haya wacha nipone kwanza. Mwajiri wako hawezi kukuelewa.

Peleka tabia hiyo kwenye kujiajiri pia, usikubali sababu ndogo ndogo zinazoendelea kwenye maisha yako kuingilia kazi zako. Endelea na kazi kila siku, kama ambavyo ungeenda kwenye kazi ukiwa umeajiriwa. 
(3). UNAKAA  KAZINI  MUDA  WA  KAZI.
Unaenda kazini kila siku, na ukifika, unakaa mpaka muda wa kazi uishe ndiyo unaondoka. Hata kama siku hiyo huna kazi za kufanya, utakaa hapo kazini mpaka muda wa kutoka ufike. Hata kama siku hiyo hujisikii kufanya kazi, utazurura zurura hapo ofisini mpaka muda wa kutoka ufike. Hutakatisha siku yako ya kazi kwa sababu tu hujisikii, siku ya kazi inaisha muda wa kazi unapoisha.

Hamishia hili kwenye kujiajiri, kwenye muda uliopanga kufanya kazi yako, fanya kazi na usiruhusu kuingiliwa na kitu kingine. Kama umepanga utaandika kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa sita mchana, basi fanya hivyo. Usiahirishe kwa sababu siku hiyo hujisikii kuandika. Kama umepanga utafungua biashara yako saa moja asubuhi na kufunga saa moja jioni fanya hivyo, isitokee siku unafunga saa 10 kwa sababu siku hiyo umechoka zaidi. Jiulize kama ingekuwa kazi ya kuajiriwa je ungeacha, kama hapana, fanya.
( 4 ).UNAFANYA  KAZI  KWA MIAKA  MINGI.
Kazi yoyote unayoifanya, utaifanya kwa miaka mingi. Kama ni mwalimu utafundisha kwa miaka mingi, unaweza kuhama shule mbalimbali, lakini utafundisha. Kama wewe ni daktari utatibu kwa miaka mingi, unaweza kubadili vituo vya kazi, lakini utatibu. Utafanya kazi yako mpaka pale utakapostaafu au kufikia uhuru wa kifedha. Na hufikirii kuifanya kwa muda mchache na isipolipa unaacha, unaifanya kwa miaka mingi.

Peleka tabia hiyo kwenye kujiajiri pia, kile unachochagua kufanya, jiandae kukifanya kwa miaka mingi. Kama ni uandishi, jua utaandika kwa miaka mingi, kama ni biashara pia, jipe muda mrefu wa kufanya. Acha kabisa kujidanganya kwamba utafanya kwa siku chache na kama hailipi utaacha. Jiandae kufanya kwa muda mrefu.
( 5 ). UNA  MAHITAJI  MAKUBWA.
Kinachokufanya uendelee kuifanya kazi yako, hata kama ni ngumu au huipendi ni mahitaji makubwa uliyonayo. Unahitaji fedha ya kuendesha maisha yako, kula, kulala, kuvaa, kuendesha familia, kusomesha watoto na mengine. Una ndugu wanaokutegemea ambapo kazi yako ndiyo inakuwezesha kuwasaidia. Mwajiri akikuambia fanya tu kwa upendo hakuna haja ya malipo huwezi kumwelewa, una mahitaji, unataka fedha, unafanya kazi ili ulipwe.

Chochote unachofanya pale unapojiajiri, hakikisha unalipwa ili uweze kuendesha maisha yako. Na hili ni muhimu sana kwenye kazi za sanaa, ni rahisi kujiambia naandika kwa sababu napenda, siyo kwa sababu nataka kulipwa. Andika ili ulipwe, una mahitaji ya maisha yako, unafikiri utayamudu vipi kama unachofanya hakikulipi?
(6 ). UNAKUBALI MALIPO  YA  KAZI.
Unapoomba kazi, cha kwanza unachouliza ni mshahara. Unapofanya kazi hiyo kwa muda unamtaka mwajiri wako akuongeze mshahara. Unaenda kusoma au kuongeza ujuzi ili upate mshahara zaidi. Unafanya kazi muda wa ziada ili upate malipo zaidi.

Peleka tabia hii kwenye kujiajiri pia, hakikisha unapata malipo na kila wakati kazana kutoa thamani zaidi ili ulipwe zaidi. Weka juhudi kubwa ili kupata malipo makubwa. Na asikusumbue mtu kwamba unataka sana kulipwa, kama hayupo tayari kulipia achana naye. Hufanyi unachofanya kuuza sura, ndiyo kinawasaidia watu, lakini asante haitaleta chakula mezani, hakikisha unalipwa.

( 7 ). KAZI   YAKO  SIYO  WEWE.
Kama wewe ni mwalimu, unajua kabisa ualimu wako unaishia shuleni, hukutani na watoto barabarani na ukaanza kuwafundisha hapo hapo. Kama ni daktari udaktari wako unaishia hospitali, hupandi kwenye daladala na kuanza kuwatibu watu. Kwa kifupi ni kwamba unapokuwa umeajiriwa, unajua kuyatenganisha maisha yako binafsi na maisha ya kazi, huchanganyi hivyo pamoja.

Hapa ndipo wengi waliojiajiri huwa wanafeli, hawajitofautishi wao binafsi na kazi zao. Kila wakati wanachanganya kazi na maisha, na ndiyo maana hawapati muda wa kupumzika. Hivyo kwa kile ambacho umejiajiri kufanya, tenga muda wa kukifanya na tenga muda wa maisha pia. Kushindwa kufanya hivyo, utachoka haraka na kushindwa kuendelea. 
(8). UNAJUA  MBINU  ZA  KUFANYA  KAZI.
Kama wewe ni mwalimu, unajua mbinu za ualimu, njia za kufundisha watu mpaka waelewe na pia unaendelea kujifunza. Kama wewe ni daktari, unajua jinsi ya kudadisi dalili za mgonjwa, vipimo gani ufanye mpaka ujue mgonjwa anaumwa nini na kisha umpe matibabu sahihi. Huamki siku moja na kujiita daktari kisha ukaanza kutibu, unajifunza.

Peleka tabia hii kwenye kile unachojiajiri kufanya, mwanzoni jua kabisa ni muda wa kujifunza, kuzijua njia bora za kufanya kitu hicho na kila wakati kazana kujua mbinu bora zaidi. Unafanya vizuri pale unapokuwa na ujuzi wa kufanya. Hivyo jifunze ujuzi wa kile ulichojiajiri kufanya.
(9 ). UNA UCHESHI  AU  UTANI  KWENYE  KAZI.
Kwa kila kazi, kuna utani fulani upo, ambao huwa haukuumizi. Utani huo unaweza kuonekana kama ni kejeli, lakini haukusumbui. Mfano baina ya madaktari, huwa wanataniana sana, mfano daktari wa upasuaji atamuita daktari wa magonjwa ya ndani ni mtu wa kubahatisha, maana anatibu kitu ambacho hakioni. Daktari wa magonjwa ya ndani atamuita daktari wa upasuaji kama mtu wa buchani, kazi yake ni kukata vitu. Huu ni utani ambao upo na madaktari hao hawapigani kwa sababu ya utani huo.

Tuhusu utani au ucheshi kwenye kile ambacho umejiajiri kufanya. Kuna watu watachukulia hiyo kama sehemu ya kukudhihaki au kukukejeli, lakini wewe utachukulia ni kama utani tu na utaendelea kufanya. Mfano unaweza kuwa mwandishi na watu wakakuambia unachoandika ni nadharia tu, hakiwezekani kwa vitendo. Usichukulie kwa umakini sana hilo, ona kama ni utani na endelea kuandika.
(10 ). UNAPOKEA  SIFA  NA  LAWAMA  KWA  KAZI  UNAYOFANYA.
Ukiwa kwenye ajira, unaweza kufanya kazi yako vizuri na ukasifiwa sana, wakati mwingine unakosolewa na kulaumiwa kupitia kazi yako. Unajua hiyo ni sehemu ya kazi, hivyo huendi nyumbani na kukosa usingizi kwa sababu bosi wako amekuambia ripoti uliyoadika siyo sahihi. Unajua kesho utaenda kufanya marekebisho kama alivyokuambia, ni sehemu ya kazi.

Peleka tabia hii kwenye kujiajiri pia. Kwa kila unachofanya, jua kuna wakati itasifiwa na kuna wakati utapingwa, kukosolewa au kulaumiwa. Kuwa tayari kupokea hayo na kuchukua hatua sahihi. Usiache kuandika kwa sababu mtu amekuambia makala yako au kitabu chako ni cha hovyo, jua kipi hakipo sahihi na boresha zaidi kwenye uandishi ujao.

MIRADI 10 INAYOWEZA KUENDESHWA NA WANAWAKE

Mwanamke kuwa na kazi au biashara ya kufanya na ikamwingizia kipato ni kitu cha muhimu sana, maana dunia ya sasa hivi tunaishi Kwa kutegemeana. Na wanawake tuna fursa nyingi sana za kujiongeza kiuchumi kama mtu ukiwa na bidii, uvumilivu na kutogopa vikwazo.
Nitakwenda kuorodhesha biashara au miradi ambayo mwanamke unaweza kuifanya , kitu cha muhimu ni anza mradi kutokana na mtaji na ujuzi ulionao na uwe unakipenda hicho kitu kutoka moyoni;

1. Bakery: hii ni bishara ya kutengeneza na kuuza vitafunwa inapata kasi sababu watu wengi hawapendi kununua vitafunio mitaani, hata kama huna mtaji wa kufungua bakery unaweza kupika vitafunwa mbalimbali nyumbani Kwa order au ku supply kwa wenye maduka au migahawa.

2. Shule za chekechea, ni biashara nzuri Kama ukipata eneo zuri na ukatoa huduma nzuri, na walimu wakiwa wana ujuzi wa kutosha. Pia kama wewe ni mwalimu unaweza kuanzisha shule yako mwenyewe kutokana na mtaji wako.

3. Event management and catering , siku hizi sherehe ni nyingi sana na watu wawataki kuangaika na mambo ya chakula, mc, mapambo, usafiri nk, wana kodi kampuni ya watu Kwa ajili hiyo.

4.Ufundishaji wa ujuzi mbalimbali, wanawake wengi wana penda kujifunza mambo mbalimbali ili watumie huo ujuzi kwenye ujasiriamali, iwe ni kupika vyakula, utengenezaji wa sabuni, mapambo, kilimo nk. Ukiwa na ujuzi wowote utumie kufundisha wengine na ujipatie kipato.

5.Maduka ya urembo na kuuza nguo za wanawake, hii ni biashara nzuri sababu supply ni kubwa mfano Dar kariakoo kuna maduka mengi tu ya jumla unaweza kupata bidhaa, na wanaume wengi wanafanya Biashara hii Ila ikifanywa na mwanamke ni bora zaidi unajua kabisa vitu gani wanawake wanapenda.

6.Insurance, consultancy companies: Kama una elimu, uzoefu na mtaji wa kutosha unaweza kuanzisha kampuni yako ya bima au kotoa ushauri mbalimbali au watu kukupa kazi zao uwafanyie na unaweza kufungua kampuni mbalimbali.

7.Biashara ya chakula, unaweza kuanzisha hotel au kimgahawa na ukapika vyakula, muhimu uweze kuandaa chakula vizuri, na kuandaa mazingira masafi na huduma ziwe nzuri.

8.Biashara ya kuuza maua na miche, hii ni biashara unaweza kuanza bila mtaji au mtaji kidogo sana, kama una maua yakate na uoteshe mengi zaidi katika vifuko, pia miche ya miti au matunda unaweza kuetengeneza kitalu, unaweza kupata maua Kwa watu hata kununua bei sio ghali. Tafuta eneo zuri la kuuzia hata kwako muhimu ni kujitangaza.

9.Biashara ya vinywaji; soma zaidi hapa

10.Biashara ya mapambo ya nyumba

Miradi iko mengi sana na bidii yako ya kufanya utafiti na kujifunza wengine wanafanya nini. Pia kumbuka biashara yoyote mwanamke unaweza kufanya na suala la mtaji sio tatizo sana mikopo ipo mradi utafute yenye masharti nafuu.


Kwa ushauri wa  BIASHARA / UJASIRIAMALI na MAISHA  wasiliana nami WhatsApp 0716924136  /   + 255 755 400 128 /  + 255 688 361 539  /  + 255 629 748 937
KOCHA MWL JAPHET MASATU

Thursday, May 14, 2020

MTAJI NI MDOGO ? --JINSI YA KUKABILIANA NA USHINDANI WA BEI .

Zifuatazo ni hatua za kuchukua ili kukabiliana na ushindani wa bei pale unapofanya biashara kwa mtaji mdogo.
 (01 ). CHEZA  MCHEZO  WAKO  MWENYEWE.
Kama unataka kupata ushindi kwenye eneo lolote la maisha yako, basi unapaswa kucheza mchezo wako mwenyewe. Hii ina maana kwamba unapaswa kutengeneza mchezo wako, kujiwekea sheria zako mwenyewe, kisha kucheza mchezo huo. Ukiingia kucheza mchezo wa wengine, ambao wameutengeneza wao na kuweka sheria zao, huwezi kushinda, maana wao ndiyo wanaoujua mchezo huo kuliko wewe.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye biashara, haijalishi unafanya biashara gani, unapaswa kucheza mchezo wako mwenyewe. Hapa unapaswa kupanga ni aina gani ya biashara unaifanya na utaifanya kwa njia zipi. Tengeneza njia zako mwenyewe, ambazo zinatumia uwezo ulio ndani yako na aina ya wateja unaowalenga, kwa kile unachouza. Jiwekee sheria zako mwenyewe na kisha endesha biashara yako kwa sheria hizo.
Chagua kufanya biashara ya tofauti, ambapo sheria yako kuu kwenye ushindani siyo bei, bali utofauti. Usishindane kwa kupunguza bei, bali shindana kwa kutoa kitu ambacho biashara nyingine hazitoi. Kwa maneno mengine, usikazane kuwa bora zaidi ya wengine, bali kazana kuwa tofauti na wengine.
Hakikisha kuna kitu ambacho wateja wanakipata kwenye biashara yako, ambacho hawawezi kukipata kwenye biashara nyingine yoyote. Inaweza kuwa aina ya bidhaa unazouza, inaweza kuwa aina ya huduma wanayoipata. Ni lazima uwe na kitu ambacho wateja wanakipata kwako tu na hawawezi kukipata kwa wafanyabiashara wengine.
Kama kwenye biashara unayoifanya huwezi kutengeneza kitu cha aina hiyo, ushindani wa bei hauwezi kukuacha salama. Usitegemee utoe kile ambacho kinaweza kupatikana kwa wengine, halafu wateja waje kununua kwako kwa bei juu wakati wanaweza kupata kwingine kwa bei ya chini.
Kumbuka ubinafsi ni asili yetu binadamu, huwa tunaangalia maslahi yetu kwanza kabla ya kitu kingine. Hivyo hakikisha kwenye biashara yako kuna kitu unachowapa wateja wako, kinachowanufaisha na hawawezi kukipata sehemu nyingine. Kwa kuwa na kitu hicho, watakuwa tayari kuja kununua kwako kwa bei ya juu kuliko kwenda kwa wengine wanaouza kwa bei ya chini.
 ( 02 ). ANZA  NA  WATEJA  SAHIHI.
Kuna wateja ambao wanachoangalia ni bei tu, na wapo wateja ambao wanachoangalia ni thamani wanayoipata. Ni vigumu sana kumshawishi mteja anayeangalia bei rahisi kuona thamani.
Hivyo kabla hujaweka nguvu zako kwenye ushawishi au mengine yoyote, anza na wateja sahihi. Jua kwanza kinachomsukuma mteja kununua ni bei au thamani.
Kama kinachomsukuma mteja kununua ni bei peke yake, usipoteze hata muda wako, kwa sababu atakwenda kule ambapo anapata kwa bei ya chini. Lakini unapokutana na mteja ambaye anaangalia thamani anayoipata, hapo una nafasi ya kumshawishi kulipa zaidi ili apate thamani zaidi.
Wateja wa thamani siyo wengi, lakini wale wachache unaowapata watakufanya ufurahie kuifanya biashara yako, maana huwa ni waelewa na hawakusumbui sana.
Wateja wa bei rahisi huwa ni wengi, lakini pia ni wasumbufu. Unaweza kuwapunguzia bei na bado wakaona umenufaika zaidi na hivyo kutaka zaidi kutoka kwako.
Kwa biashara unayofanya, chagua aina ya wateja unaotaka kwenda nao, kisha tafuta aina hiyo ya wateja. Wanapokuja wateja wanaoangalia bei tu, waeleze thamani unayotoa na kama bado wanasisitiza kwenye bei, unaweza kuwaelekeza wapi pa kupata kwa bei wanayotaka wao, lakini pia waoneshe nini watakosa kwa kuangalia bei pekee.
 ( 03 ). KUWA  KARIBU   ZAIDI  NA  WATEJA WAKO.
Biashara ndogo huwa zinazishinda biashara kubwa kwenye eneo hili, uwezo wa kuwa karibu na wateja. Biashara kubwa zinahudumia watu wengi, hivyo huwa hazihangaiki na mteja mmoja mmoja, hivyo mteja hawezi kupata upekee kwenye biashara kubwa.
Ila kwenye biashara ndogo, kwa sababu wateja ni wachache, ni rahisi kumpa kila mteja upekee anaostahili. Ni rahisi kumjua kila mteja na matakwa yake, hivyo wajibu ni kumtimizia mteja yale anayotaka kwa namna yake mwenyewe.
Kosa kubwa ambali wafanyabiashara wengi wadogo huwa wanafanya ni kufanya biashara zao ndogo kama vile ni biashara kubwa, kitu ambacho kinawagharimu sana.
Kuwa karibu zaidi na wateja wako, wasiliana nao mara kwa mara, jua matukio mbalimbali kwenye maisha yao, mfano siku zao za kuzaliwa, watu wao wa karibu na kadhalika. Kisha watumie salamu au jumbe mbalimbali katika siku zao hizo muhimu.
Tumia kila fursa kuwapa wateja wako upekee, uwafanye wajisikie vizuri wanapokuja kwenye biashara yako ambapo wanalipa zaidi kuliko wanavyojisikia wanapokwenda kwenye biashara kubwa ambapo wanalipa kidogo.
 ( 04 ).  WAFUATE  WATEJA  KULE  WALIPO.
Njia nyingine ya kuongeza thamani kwa wateja wako ili wawe tayari kulipa zaidi kwako ni kuwafuata kule walipo. Sasa hivi watu hawana muda, hivyo wanapenda sana pale biashara inapowafuata wao kule walipo. Lakini pia uaminifu umekuwa mdogo, hivyo watu wengi huhofia kuagiza vitu ambavyo hawajaviona.
Wewe kwa kuwa na biashara ndogo, una nafasi ya kujenga uaminifu na wateja wako na kisha kuwafanya waweze kuagiza kile unachouza popote walipo na wakapelekewa. Hii inawafanya wateja wawe tayari kulipa zaidi, kwa sababu imewapunguzia usumbufu na upotevu wa muda kutoka walipo na kwenda kutafuta wanachotaka.
Biashara ndogo inaweza kuwafikia wateja kule walipo kwa ufanisi zaidi kuliko biashara kubwa, hivyo tumia vizuri nafasi hiyo.
 ( 05 ) WEKEZA  ZAIDI  KWENYE  BIASHARA  YAKO.
Unapomtaka mteja alipie zaidi kile anachonunua kwako, ambacho anaweza kukipata kwa bei ya chini sehemu nyingine, lazima utengeneze mazingira ambayo yatamfanya mteja aone anastahili kulipa zaidi. Mfano ukinunua soda ya cocacola kwenye duka la mtaani utalipa shilingi mia tano, lakini soda hiyo hiyo ukiinunua hotelini utalipa shilingi elfu mbili. Ukiwa hotelini hutalalamika kwa nini uuziwe soda ya mia tano kwa shilingi elfu mbili, kwa sababu kuna mazingira yanayokufanya uone kulipa elfu mbili ni halali. Unakuwa umekaa eneo zuri na tulivu, unahudumiwa na watu wanaokujali na kadhalika.
Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kufanya kwenye biashara yako, fanya uwekezaji unaoipa biashara yako thamani zaidi kuliko washindani wako. Kuna kitu kidogo sana unaweza kukifanya kwenye eneo lako la biashara na likawafanya watu waipe thamani kubwa. Kitu hicho ni mwonekano wa eneo la biashara, linapaswa kuwa safi na lililopangiliwa vizuri. Mtu akifika kwenye eneo hilo anaona utofauti mkubwa, na ndani yake anakuwa tayari kulipa zaidi.
Wewe mwenyewe ni shahidi, huenda umewahi kufika kwenye eneo la biashara, na kwa jinsi lilivyo na mwonekano mzuri, ukajua utatozwa gharama kubwa, lakini ulipotozwa gharama za kawaida ukashangaa. Hiyo ndiyo hali unayopaswa kuileta kwenye biashara yako pia, kufanya uwekezaji unaowaandaa wateja kuwa tayari kulipa zaidi.
Mwonekano na mpangilio wa eneo la biashara, vifaa unavyotumia na huduma unayowapa wateja wako vinapaswa kuwa vya viwango vya juu sana kiasi cha mteja kuona kama anakuibia pale unapomtajia bei. Na kumbuka hapa utakuwa unawalenga wateja sahihi na siyo wale wanaoangalia bei ya chini pekee.
Rafiki, hizo ndizo hatua tano za kuchukua ili kuweza kukabiliana na ushindani wa bei pale unapofanya biashara kwa mtaji kidogo. Kama ulivyoona, kuna mengi ya kufanya kuliko kuingia kwenye ushindani wa moja kwa moja kwenye bei, ambao utakuumiza sana.
Nimalizie kwa kukuambia hili rafiki yangu, kama upo kwenye biashara ambayo kitu pekee unachoweza kujitofautisha nacho ni kupunguza bei, basi upo kwenye biashara ambayo siyo sahihi. Kwa sababu kuna wengine wapo tayari kupunguza bei zaidi yako, na wakiwa na mtaji mkubwa kuliko wewe, watapata faida kwa kuuza kwa wengi zaidi kuliko wewe unayeuza kwa wachache.
Hivyo fanyia kazi haya matano uliyojifunza, na mengine yanayoendana na hayo, lakini siyo kupunguza bei. Na kama biashara haina namna nyingine bali bei basi achana nayo na nenda kwenye biashara sahihi, ambapo unaweza kutengeneza mchezo wako mwenyewe na kuucheza vizuri.

JIUNGE  NA  DARASA  ONLINE  KWA  KULIPIA   ADA  YA  MWEZI , MWAKA---UJIFUNZE KWA  UNDANI  NA  MAPANA--ELIMU  YA  BIASHARA &  UJASIRIAMALI--- NA  UCHUKUE  HATUA --UTAFANIKIWA

SEE  YOU  AT  THE    TOP
Ndimi  rafiki   yako KOCHA /   MWL.  JAPHET   MASATU , BLOGGER
Kwa   maelekezo   zaidi  tuwasiliane  kwa ;--
SIMU / MESEJI / ( WhatsApp  + 255 716 924136 )    /    +255 755 400128  /  + 255 688  361  539 /  + 255 629 748  937