Mpendwa rafiki yangu, Mdau wangu
Unapokuwa kiongozi unakuwa na mamlaka makubwa juu yaw engine, una
uwezo wa kuamuru chochote na kikafanyika. Hivyo basi, kama ukisema
utumie mamlaka hayo vibaya lazima utaharibu watu. Utatumia vile
unavyotaka na matokeo yake cheo kinakupa kiburi utajiona wewe ndiyo wewe
hakuna mwingine.
Tukianzia hata uongozi ndani ya familia zetu, kama baba akiwa ni mtu
wa kutumia madaraka yake vibaya lazima ataharibu familia yake. Kama
umepewa madaraka basi yatumie vizuri hayo madaraka kuleta matokeo
mazuri. Watu wakufurahie uwepo wako kwa kufanya makubwa ambayo yanakuwa
ni msaada kwa wote.
Mfano baba anaweza kuwa ni kiongozi wa familia lakini huwa anatoa
adhabu kwa watoto kupita kiasi au kwa upendeleo sasa hii inaleta mpasuko
kwa watoto, inaleta vinyongo na kuwagawa watoto katika familia.
Kama kiongozi unatakiwa kuwa na nguzo muhimu katika uongozi wako
ambayo nguzo yenyewe ni msamaha. Msamaha ni nguzo muhimu sana kwa
kiongozi yoyote yule. Siyo kila kosa linahitaji adhabu, kama kiongozi
unatakiwa uwe na msamaha katika uongozi wako.
Ukiwa ni mtu wa kufuata sheria katika uongozi wako, yaani kila kosa
wewe ni adhabu tu basi utawapoteza watu wengi. Kwa sababu watu wengi
wana udhaibu wa kibinadamu na huwezi ukakosa kosa kwa mtu kama ni mtu
unayesimamia sheria.
Hapa ndiyo inakuja nguzo muhimu sana ya uongozi ambayo ni msamaha.
Msamaha unaleta amani kwenye eneo lolote la uongozi. Msamaha unaleta
utulivu,kama kuna mahali watu walikuwa hawana utulivu basi baada ya
kiongozi wa sehemu husika wanafurahia msamaha huo na kuwaletea utulivu
wa wa akili.
Msamaha unafanya eneo kuwa tulivu,mtaa, nchi, mkoa, kijiji, familia
na hata dunia kiujumla. Kwa kupitia msamaha unawaleta watu na kusahau
hata tofauti walizonazo.
Kama kiongozi unatakiwa uwe unavaa sifa ya uungu ndani yako, kama
ingekuwa Mungu anatoa adhabu kama binadamu basi leo hii hakuna ambaye
angeweza kusimama lakini kwa kuwa kuna msamaha, tunaweza kujirudi na
kuwa watu wapya tena.
Hatua ya kuchukua leo; kama wewe ni kiongozi siyo kila kosa unapaswa
kutoa adhabu muda mwingine unasamehe. Na kumbuka kuwa siyo kila kosa ni
la kusamehewa ukiwa unatoa msamaha kwenye kila kosa watu wataacha
kufuata tena sheria.
Kwahiyo, kumbuka kuwa kila nafasi ya uongozi uliyonayo ni kama vile
unamsaidia Mungu, hivyo angalia sifa za Mungu je unavyoongoza watu wako
una nguzo za huruma, msamaha na siyo mwepesi wa hasira? Kuwa mtu wa
msamaha na usiwe mwepesi wa hasira maana utawapoteza wengi kama siyo
kuwamaliza.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Showing posts with label VIONGOZI NA SEMINA ELEKEZI. Show all posts
Showing posts with label VIONGOZI NA SEMINA ELEKEZI. Show all posts
Friday, August 9, 2019
JINSI YA KUWA KIONGOZI BORA
Mpendwa rafiki yangu, Mdau wangu Jamii yoyote ile iliyostarabika lazima iwe na kiongozi anayewaongoza. Uongozi ni kitu muhimu sana, kuanzia katika familia zetu mpaka ngazi ya taifa. Eneo ambalo hakuna kiongozi huwa linajulikana kwa sababu wanakuwa hawana mwelekeo.
Ni muhimu sana kila mmoja wetu kujifunza mambo ya uongozi, hata kama huna unaowaongoza basi unajiongoza mwenyewe. Jichukulie wewe ni kiongozi mkubwa na anza kufanya mambo ambayo viongozi wakubwa wanafanya.
JE , NI NAMNA GANI UNAWEZA KUWA KIONGOZI BORA ?
(1). Onesha mfano; kiongozi bora ni yule ambaye anakuwa anaongoza kwa mfano. Kama wewe ni kiongozi eneo lako la kazi unatakiwa kuwa mfano. Kama unasisitiza kuwahi, basi mtu wa kwanza kuwahi atakuwa uwe wewe. Na ukifanya hivyo utashangaa wote wanakuwa wanawahi kazini. Hata siku moja usitegemee kupata kile ambacho hukitoi kwa wengine.
Unapohamasisha juu ya jambo fulani basi hakikisha uwe kinara wa kuwa kwanza katika utekelezaji wa jambo hilo. Usiwe tu mtu wa kuongea bali kuwa mtu wa kuonesha njia, ili na watu wengine wapiti. Utakapoweza kuonesha njia hata wengine nao watakuwa rahisi kupita. Kama kiongozi ukiwa mwoga usitegemee unaowaongoza watakuwa tofauti na wewe.
( 2 ). Uwe mtu makini. Kadiri unavyoonesha umakini katika mambo yako ndivyo watu nao wanakuwa kama wewe. Binadamu wanatabia ya kumsoma mtu ni mtu wa namna gani, wakishajua wewe ni mtu wa namna gani, wala hawawezi kujisumbua tofauti na wewe unavyotaka. Kiongozi unatakiwa kuonesha umakini juu ya yale unayosema.
Kama wewe hujali yale yale unayosema unafikiri naye atajali? Anza kujali kwanza wewe kuonesha kuwa jambo hilo ni muhimu na akiona kiongozi wake yuko makini anajali lazima na yeye atajali. Akili ya binadamu inasetiwa ukishawaseti watu utawaongoza vile unavyotaka wewe na siyo vile wanavyotaka wao.
( 3 ). Uwe mfuatiliaji kweli; kuna viongozi wengine huwa wanaishia kusema tu. Ni bora usiseme kuliko unasema halafu unashindwa kuchukua hatua. Kusema halafu hapana utekelezaji ni sawa na kujidharau. Unamaliza nguvu zako bure tu.
Uwe unafuatilia mambo yako yote jua kile kinachoingia na kinachotoka. Jua kila kitu kuhusu kazi au biashara yako na wale ambao wako chini yako hakikisha wanafuata mwongozo wa kazi. Usitegemee kupata watu makini kama wewe siyo mtu makini. Watu wanakuwa makini kama wewe ukiwa makini.
Hakuna mtu ambaye atakuchezea kama wewe hutaki kuchezewa. Jinsi utakavyojichukulia ndivyo na watu watakavyokuchukulia.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa kiongozi wa mfano, kuwa makini, kuwa mfuatiliaji na jali yale unayosema. Ukiishia kusema na watu unaowaongoza wataishia kusikia na kutokufanya.
Hivyo basi, kama unataka mambo yako yaende kama unavyotaka wewe, anza kuwa mtekelezaji wa kwanza wa jinsi vile unavyotaka mambo yako yaende. Utakuwa kiongozi bora kama utakuwa mwaminifu, mwadilifu, mwajibikaji kwenye yale unayosema.
Subscribe to:
Posts (Atom)