Showing posts with label MAKALA MBALIMBALI ZA MAISHA NA MAFANIKIO---TANZANIA-----NA MWL. JAPHET MASATU. Show all posts
Showing posts with label MAKALA MBALIMBALI ZA MAISHA NA MAFANIKIO---TANZANIA-----NA MWL. JAPHET MASATU. Show all posts

Saturday, May 31, 2025

MAKALA : JE, WAJUA KUSUDI LAKO KUWAKO HAPA DUNIANI ?? NDANI YAKO KUNA MOTO WA NDOTO ZAKO UMEFICHWA------NA MWL JAPHET MASATU ------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Rafiki Yangu Mpendwa,

‎Watu wengi wanamka kila siku…

‎Wanaoga, wanavaa, wanatoka.

‎Lakini hawajui kwa nini wanaishi.

‎Wanapambana… lakini hawajui wanapambana kwa lipi.

‎Wanaume wanahangaika na mihangaiko,

‎Wanawake wanahangaika na wanaume.

‎Kila mtu anakimbia, lakini hakuna anayeuliza:

‎"Tunakoenda ni wapi?"

‎Ishu Hii Ndio Inasababisha Maisha Ya Watu Yatupwe Kama Karatasi Iliyotumika.

‎Unajikuta una miaka 30... lakini unahisi hujaanza kuishi.

‎Unajiona hufai.

‎Unachoka bila kazi.

‎Una usingizi wa saa 10 lakini bado umechoka.

‎Unapoteza nguvu kwenye mambo yasiyojenga.

‎Unapata hela unazimaliza bila hata kumbukumbu.

‎Unapenda unakataliwa.

‎Unajifunza lakini bado maisha yako yapo vile vile.

‎Unapambana, lakini unapambana gizani.

‎Umefungwa kwa minyororo usiyoiona…

‎Na minyororo hiyo inaitwa: "Kutokujua KUSUDI la maisha yako."

‎Kujua Kisudi Ni Siri Ya Waliotoka Chini Wakafika Juu.

‎Wewe si maskini umepoteza mwelekeo tu.

‎Wewe si mvivu hujagundua unachopaswa kufanya.

‎Wewe si mshindwa hujajua sababu ya wewe kuwa hai.

‎Watu wakishajua walichozaliwa kufanya,

‎wanabadilika kama mwewe aliyefunguliwa.

‎Wanapaa.

‎Wanang’ara.

‎Wanatesa!

‎Ukweli Ni Huu: Maisha Hayaanzi Kwa Kupata Pesa Yanaanza Kwa Kujielewa.

‎Na huwezi kujielewa bila MWONGOZO.

‎Huwezi kufika bila RAMANI.

‎Huwezi kushinda bila KUJUA UNAPIGANIA NINI.

‎Ukweli mwingine ni huu:

‎Watu wengi wameishia kuishi maisha ya kuigiza.

‎Maisha ya watu wengine.

‎Wanavaa kama wengine.

‎Wanakimbia mafanikio ya wengine.

‎Wanajilinganisha.

‎Wanashindana.

‎Lakini ndani yao kuna MOTO UMEFICHWA.

‎Moto wa ndoto zao.

‎Moto wa kusudi lao.

‎Moto wa ukubwa wao halisi.

‎SULUHISHO?

‎Chukua MWONGOZO huu: “MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.”

‎KWA   KUEDELEA    KUSOMA    VITABU  Ndani yake utajifunza:

✅ Jinsi ya kugundua kusudi lako.

‎Sheria 100 za maisha ya mafanikio.

✅ Jinsi ya kuamka kila asubuhi ukiwa na maana

✅ Jinsi ya kuishi maisha ya tofauti

✅ Jinsi ya kuacha kuigiza na kuanza kuishi maisha yako halisi

‎Bado namkumbuka Huyu Kijana.

‎Kuna kijana mmoja alinitafuta.

‎Alichoka kuishi maisha ya ‘kawaida.’

‎Alikuwa na degree.

‎Alikuwa na kazi.

‎Lakini kila kitu kilionekana kimekosa ladha.

‎Akaanza kunywa.

‎Akaanza kuchelewa kazini.

‎Akaanza kujichukia.

‎Siku moja akaniambia:

‎“Bro, naishi kama si mimi.”

‎Nikampa mwongozo huu.

‎Akarudi baada ya wiki tatu na macho yenye mwanga.

‎Sasa ameanzisha kitu chake.

‎Anaamka kabla ya saa kumi.

‎Anapata pesa.

‎Anapendwa.

‎Anajipenda.

‎Maana sasa anajua KUSUDI lake.

‎Uko Tayari Kuamka?

‎Ama utaendelea kuishi kama ndoto ya mtu mwingine?

👉 Usiishi kama kivuli jifunze kuangaza.

ENDELEA   KUSOMA   VITABU    KILA  SIKU  ILI  UENDELEE  KUANGAZA  NA    KUISHI  KUSUDI  LAKO

Friday, May 30, 2025

MAKALA : MJASIRIAMARI MJANJA ANA TABIA GANI ???

 Kakaa/Dadaa Yangu,

‎ Unajua shida ya wengi?

‎Wengi wanaanza biashara kwa kishindo...

‎Lakini baada ya miezi mitatu,

‎BAM! Kimya kama kaburi la usiku.

‎Wanaanza kuuza nguo,

‎Wanaingiza mzigo wa milioni mbili,

‎Lakini hakuna anayenunua.

‎Wanashindwa kuelewa nini kinakwenda kombo.

‎Wanakata tamaa fasta.

‎Wanarejea kutegemea mshahara.

‎Wengine wanakata tamaa kabisa—wanakufa na ndoto zao.

💔 Na hapa ndipo kuna maumivu makali.

‎Biashara si kupost tu bidhaa kwenye status.

‎Si kutegemea rafiki zako watanunua.

‎Wala si kushusha bei kila siku eti "promo."

‎Ukiwa huna akili ya mjasiriamali mjanja

‎utachezewa kama karata mitaani.

🎯 Ngoja nikufunze kitu.

‎Mjasiriamali mjanja ana akili ya pesa.

‎Anajua kutafuta wateja wake popote.

‎Anajua jinsi ya kuwashawishi bila kusumbua.

‎Anajua kutoa ofa ambayo haiwezi kukataliwa.

‎Anaelewa psychology ya mteja.

‎Na zaidi ya yote, anajua kuji-brand.

‎Na kama hujui hayo yote,

‎Usijidanganye eti “ni mapenzi ya Mungu.”

‎Ni mapenzi ya kukosa maarifa.

⚙️ Sasa suluhisho liko hivi:

‎Ukiamua kuwa mjanja kwenye biashara

‎Lazima ujue kuuza hadithi.

‎Ndiyo, HADITHI!

‎Watu wananunua stori kabla ya bidhaa.

‎Wakiigusa hadithi yako,

‎Wanafika mwisho wa status tayari wamejishawishi.

‎Ukiuza sabuni,

‎Usiuze sabuni uza usafi wa mtoto wako.

‎Ukiuza viatu,

‎Usiuze kiatu uza heshima ya mguu wake kazini.

‎Mjasiriamali mjanja anauza HISIA si bidhaa tu.

🧠 Nikupe hadithi moja ya kweli.

‎Mrembo mmoja anaitwa Amina.

‎Alikuwa anauza mikoba Kariakoo.

‎Alihangaika sana, kila siku status 50, likes 2, wateja 0.

‎Alipojifunza kuuza kwa stori, mambo yalianza kubadilika.

‎Siku moja aliandika:

‎“Mwanamke mmoja alikuja dukani kwangu, akiwa amechoka, alinyamaza muda mrefu...

‎Aliponunua hii handbag,

‎Alisema, ‘Kwa mara ya kwanza najihisi mwanamke kamili.’

‎Niliogopa kusema chochote,

‎Ila moyo wangu ulichanua.

‎Na hapo ndipo nilijua,

‎Siuzi mikoba, nauza imani kwa mwanamke.”

‎Dakika 20 baadaye mikoba 7 iliuzwa.

Thursday, May 22, 2025

MAKALA : MAISHA SI BAHATI NASIBU AU KUBET . NI RAMANNI YA MABADILIKO NA DIRA . NI MAAMUZI NA MAANDALIZI------NA MWL. JAPHET MASATU------TANZANIA -------FRIKA YA MASHARIKI--------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Kakaa/Dadaa....

‎Unajua shida kubwa inayowakumba wengi?

Wanaamka kila siku…

‎Wanakimbizana kama mchwa waliomwagiwa maji…

‎Lakini hawajui wanakimbilia wapi.

‎Kila siku ni kujituma…

‎Lakini mwisho wa mwezi, mfuko ni kama shimo la panya.

‎Kila mwaka unakatika…

‎Lakini hakuna mabadiliko ya maana.

‎Wengi wako kwenye 'autopilot' ya maisha.

‎Wanajisukuma tu.

‎Wakiamini ipo siku mambo yatajileta.

‎Mambo hayajileti. Wewe ndo lazima uyasogeze.

‎Hii Inatisha Kidogo…

‎Unaamka ukiwa na nguvu.

‎Unaota mafanikio.

‎Lakini kila jioni, unarudi na uchovu tu.

‎No progress.

‎No peace of mind.

‎Unasema utabadilika kesho.

‎Kesho ikifika, unafanya yaleyale.

‎Ni kama umefungwa pingu zisizoonekana.

‎Hii ni hatari sana.

‎Inaua ndoto zako taratibu bila kelele.

‎Alafu unakuja kushangaa:

‎“Mbona maisha yananizunguka?”

‎Ni kwa sababu hakuna mwongozo.

‎Kuna Uongo Mmoja Mkubwa…

‎Eti “kuwa na bidii, utafanikiwa.”

‎Wongo huo.

‎Watu wengi wana bidii kuliko hata gari la kubeba mawe.

‎Lakini wako pale pale.

‎Tatizo si bidii.

‎Tatizo ni kutokuwa na DIRA.

‎Hakuna ramani.

‎Hakuna mwongozo.

‎Na kama hujui unakokwenda…

‎Hutajua hata ukifika.

Sasa Sikiliza Vizuri…

‎Maisha yako yanahitaji mfumo.

‎Mfumo wa kuweka malengo.

‎Kujijua wewe ni nani.

‎Unataka nini.

‎Na kwa nini unakitaka.

‎Halafu?

‎Anza kupanga hatua ndogo ndogo.

‎Kila siku.

‎Kidogo kidogo hadi kikamilike.

‎Na muhimu zaidi, tafuta maarifa ya kweli.

‎Si porojo.

‎Maarifa ya watu waliopitia moto.

‎Walioungua.

‎Wakaamka.

‎Wakasimama tena.

‎Ngoja Nikupe Kisa Cha Huyu Bwana Mdogo Hapa…

‎Kuna Bwana Mdogo mmoja mtaani kwetu Anaitwa Baba T.

‎‎Miaka mitano iliyopita alikuwa anauza vocha na peremende stendi.

‎Maskini alikua anavaa viatu vilivyochanika…

‎Watu walimcheka.

‎Lakini kuna siku moja aliniambia:

‎“Bro, nimeshaamua. Sitaki kufa maskini. Nataka mafanikio ya ukweli.”

‎Akanunua daftari.

‎Akaandika malengo yake.

‎Akasoma vitabu.

‎Akatafuta mentor.

‎Akaanza kuandika kila kitu anachotumia.

‎Leo hii?

‎Ana duka lake la simu.

‎Anauza online.

‎Anatoa ushauri kwa vijana wengine.

‎Na bado ni yule yule – Baba T ila mwenye mwongozo mpya wa maisha.

‎Na Wewe Unaweza Kubadilika Leo…

‎Ukiamua, unaweza.

‎Ukiwa na mwongozo sahihi, maisha yanabadilika.

‎Unapunguza makosa.

‎Unafupisha safari ya mateso.

‎Unapanda ngazi haraka.

‎Chukua hatua.

‎Andika malengo yako.

‎Soma kila siku.

‎Tafuta watu wanaojua kuliko wewe.

‎Achana na kelele za mtaani.

‎Focus.

‎Maisha ni yako.

‎Na hakuna atakayeyaishi kwa niaba yako.

‎Unataka mafanikio ya kweli?

‎Tafuta mwongozo.

‎Fuata mfumo.

‎Jitahidi bila kusahau mwelekeo.

‎Maisha si bahati.

‎Ni maamuzi na maandalizi.

ENDELEA   KUSOMA  HAPA   UTAPATA    RAMANI  YA  MABADILIKO   NA  DIRA    YA  MAISHA  YAKO. 

Sunday, May 18, 2025

MAKALA : NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA NDOTO ZAKO UMEIBEBA WEWE MWENYEWE NA SI MTU MWINGINE--------NA MWL. JAPHET MASATU -------CALL / SMS / WHATSAPP + 266 716 924 136

 Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Umesahau wewe ni nani.

‎Umesahau kuwa ndani yako kuna nguvu ya kutikisa dunia.

‎Umejikatia tamaa kimya kimya.

‎Kila siku unasema *labda mimi sina bahati.*

‎Umeanza kuamini maisha ni magumu na huwezi kubadilisha chochote.

‎Lakini ukweli ni huu: UNA NGUVU YA MIUJIZA NDANI YAKO  ,  

‎Unaitumia vibaya.

‎Au hujui hata ipo.

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyeanzisha biashara kwa buku 5 akafika juu?

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyefeli shule lakini leo anaajiri waliopata division one?

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyetelekezwa, akasota, lakini leo anajenga nyumba yake?

‎Wote hawa hawakuwa na miujiza ya mbinguni.

‎Walitumia nguvu ya ndani waliyoamka nayo kila siku.

‎Na hiyo nguvu wewe pia unayo.

‎Lakini... unaitumia kuskroll TikTok.

‎Unaitumia kulalamika.

‎Unaitumia kutafuta huruma badala ya suluhisho.

‎Una nguvu lakini hauna mwelekeo.

‎Miujiza sio kupasuliwa mbingu.

‎Sio malaika kushuka.

‎Miujiza ni pale mtu wa kawaida anapoamua kuamka na kuchukua hatua isiyo ya kawaida.

‎Ni pale mtu anapoamua kuamka kabla ya wengine.

‎Kuanza kuandika ndoto zake.

‎Kuanza kusoma vitabu badala ya magazeti ya udaku.

‎Kuanza kuomba kazi kwa bidii badala ya kuomba msaada.

‎Miujiza ni matokeo ya msimamo.

‎Suluhisho Lipo. Na Lipo Ndani Yako.

‎Badilisha namna unavyofikiri.

‎Acha kusema “sina mtaji” sema “naanza na hiki kidogo.”

‎Acha kusema “nimechelewa”  sema “leo ndiyo siku yangu ya kwanza.”

‎Acha kujificha nyuma ya visingizio.

‎Toka uvunguni.

‎Toka kwenye comfort zone ya umaskini wa mawazo.

‎Chukua hatua.

‎Anza leo.

‎Fanya kitu.

‎Kwa sababu NGUVU YA MIUJIZA UMEIBEBEA WEWE MWENYEWE.

‎Bado namkumbuka....

‎Kuna bro mmoja alichoka na maisha.

‎Alikuwa hana kazi. Hana mtaji. Hana cheti.

‎Alikaa chini akaandika: “Mwaka huu lazima niwe mtu mwingine.”

‎Akaanza kuuza karanga mtaani.

‎Akaweka akiba ya mia mia.

‎Alikuwa anasoma vitabu alivyokopeshwa.

‎Alifungua YouTube kujifunza marketing.

‎Miaka mitatu baadaye...

‎Ana biashara ya kuuza nafaka.

‎Ana familia.

‎Ana ndoto mpya kila mwaka.

‎Aliniambia hivi:

‎“Miujiza haikunitokea, niliitengeneza mwenyewe.”

‎Sasa Wewe Una Sababu Gani Ya Kukata Tamaa?

‎Huna sababu.

‎Una kila sababu ya kusimama.

‎Chukua kalamu na kuandika ndoto zako.

‎Zima data saa tatu usiku na kupanga kesho yako.

‎Na anza kutenda miujiza ya kweli kupitia nguvu yako ya ndani.

‎Kumbuka: Miujiza Haiporomoki.

‎Miujiza hutengenezwa.

‎Na hutengenezwa na watu kama wewe.

‎Watu wa kawaida lakini walioamua kuishi maisha ya ajabu.

 

ENDELEA   KUTEMBELEA    BLOG  HII     UTAJIFUNZA  MENGI   "  MAISHA    NA  MAFANIKIO ( LIFE  &   YOU  )  BLOG  "  PENDA    KUNUNUA    VITABU  NA    KUVISOMA   UTAGUNDUA  SIRI  NYINGI   ZA  DUNIA  HII.

Wednesday, April 30, 2025

MAKALA : UNASEMA HUNA MUDA ?? JE , RATIBA YAKO YA KILA SIKU INASOMAJE ?? KULALA , KULA , KUONGEA UMBEA , KULALAMIKA ?? KUCHATI MITANDAONI ? TUMIA MUDA VIZURI KUINGIZA KIPATO -----NA MWL. JAPHET MASATU-------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Rafiki, kila siku unasema, *sina muda* , kumbe ni wewe tu hujui namna ya kuutumia.

Haupo peke yako.

Kila siku unajiambia “sina muda”,

...lakini unatumia masaa mengi (masaa manne kwa siku) kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp, Facebook, Instagram, TikTok).

Unasema unataka kufanikiwa, lakini ratiba yako inasoma: kulala, kula, kuskrolu kwenye mitandao, kulalamika.

Unajua ni nini kinauma zaidi?

Ni kuona mtu ambaye alikuwa hana chochote, alikuwa anakunywa chai kavu na maandazi ya mia tano, leo hii anaingiza laki kwa siku,

... na bado wewe uko pale pale.

Tofauti si akili, si bahati, ni jinsi mtu alivyoamua kutumia muda wake.

Wengi wameaminishwa kuwa mafanikio ni kwa watu waliobahatika, au waliotoka familia nzuri.

Lakini ukweli ni huu: kila mtu ana masaa 24.

Elon Musk ana masaa 24.

Wewe pia una masaa 24.

Ukitumia saa 1 kwa siku kuboresha maisha yako, hayo ni masaa 365 kwa mwaka.

Nani anakuzuia?

Zifuatazo Ni Mbinu 3 Za Kuchukua Hatua Leo:

1. Saa Moja Tu Kila Siku:

Jifunze kitu kimoja kinachoweza kukuingizia kipato (kama Copywriting, content creation).

Simu yako iwe zana, sio toy.

2. Panga Muda Kama Mzigo Wa Gari:

Jua dakika zako zinaenda wapi.

Tengeneza ‘to-do list’ ya kweli, sio ndoto.

Fanya vitu 3 vya maana kila siku kabla ya saa tano asubuhi.

3. Tafuta Mtandao Wa Watu Wenye Malengo:

Unakuwa kama watu 5 unaotumia nao muda mwingi.

Kama wote ni wasumbufu, utakua msumbufu pia.

Hii hapa ndiyo ile hadithi ya kweli ya Kelvin wa Tandika:

Jamaa alikuwa mtaani, hana kazi rasmi.

Aliamua kujifunza jinsi ya kuuza bidhaa za watu wengine kupitia WhatsApp na Instagram.

Kila siku aliweka saa moja kujifunza na kupost.

Mwaka mmoja baadaye, ana duka la perfume na ameshaandika eBook inayoingiza hela kila mwezi.

Alianza na muda, si mtaji.

Usilale na “kesho nitaanza.”

Anza leo.

Kumbuka; Muda haukupi second chance, ila wewe unaweza kuamua kuanza upya leo.



MAKALA : KUWA NA NIDHAMU NA PESA ZAKO !! ANZA KUWEKEZA BUKU ( SH 1000 ) KILA SIKU UJENGE UTAJIRI WAKO WA KESHO ----NA MWL. JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

Mpendwa Rafiki,

‎Watu wengi wanaamini kuwa ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na hela nyingi ,milioni tano, kumi, au hata zaidi.

‎Wengine wanasema, *Mimi ni wa mshahara wa chini, siwezi kufika mbali.*

‎Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawajui kitu kimoja muhimu: nguvu ya *buku* moja tu.

‎Buku ambayo unaitumia bila mpango kila siku, inaweza kuwa tiketi yako ya kutoka kwenye umaskini hadi kwenye uhuru wa kifedha.

‎Ni mara ngapi umetumia buku kununua soda, chipsi, vocha, au kitu usichohitaji halafu ukaishia kusema, *Ah ni buku tu*?

‎Halafu mwisho wa mwezi unakuta umekopa, umeshindwa kuwekeza, hata akiba huna.

‎‎Inasikitisha, siyo? Sasa fikiria, kama kila siku unapoteza buku moja tu, ndani ya mwezi umepoteza buku 30.

‎Mwaka mzima? Hiyo ni buku  360,000!

‎Na kama ungezitumia kuanzisha biashara ndogo au kuwekeza, ungekuwa mbali.

‎Hiyo ndiyo nguvu tuliyo nayo lakini hatuitumii.

‎Wengi tulifundishwa kwamba hela nyingi ndiyo hujenga utajiri.

‎Tukaanza kusubiri *mshahara mkubwa,* *tenda kubwa za kibiashara," au *mjomba wa Dubai.*

‎Lakini hizo ni hadithi.

‎‎Angalia Uhalisia : Hela hujengeka kwa nidhamu na mpango, siyo kiasi.

‎Watu matajiri hawakuanza na mamilioni.

‎Walitumia kile kidogo walichokuwa nacho kwa akili.

‎Walitunza, wakawekeza, wakaendeleza.

‎Kwa hiyo, tukiachana na dhana ya *nitakapoanza kupata hela kubwa,* tunaweza kuanza safari ya utajiri hata leo,

‎Kwa ile buku tuliyonayo mfukoni.

‎Sasa hebu tuweke wazi, unataka kujenga utajiri kwa kutumia buku?

‎Hizi hapa ni hatua 3 rahisi lakini zenye nguvu:

‎a. Weka akiba ya buku 1 kila siku:

‎Tafuta kopo, lipachike mahali salama. Kila siku, kabla ya kutumia hela yoyote, tengeneza tabia ya kuweka buku moja pembeni.

‎b. Anza kuwekeza kidogo:

‎Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na zaidi ya buku 30.

‎Tafuta biashara ndogo, lipia kozi fupi, au nunua bidhaa za kuuza mitandaoni.

c. Wekeza kwenye maarifa:

‎Buku moja inaweza kununua data. Tumia hiyo kusoma makala, kuangalia video za elimu ya fedha, au kusikiliza podcast. Maarifa ni mtaji.

‎Kuna jamaa yangu mmoja anaitwa Mussa,

‎Alikuwa na mshahara wa laki na 20 kwa mwezi.

‎Alikuwa na majukumu mengi lakini alianza kuweka buku moja kila siku.

‎Miezi sita baadaye, alikuwa na buku 180.

‎Akanunua kahawa na kuanza kuuza kikombe ofisini kwao, faida yake ilikuwa buku 2 kwa kila kikombe.

‎Siku moja akaniambia,

‎‎*Bro, ile tabia ya kuweka buku moja kwa siku ilinibadilishia maisha.

‎Sasa hivi nina biashara mbili na bado naendelea kuweka akiba!*

‎Ukweli ni huu:

‎Buku moja inaweza kuwa mtaji wa maisha yako mapya.

‎Usidharau kile kidogo, ndani yake kuna nguvu kubwa sana ya kifedha.

‎Anza leo, anza sasa.

‎Usisubiri mshahara mkubwa, anza na buku!


‎Kumbuka; Buku yako ya leo, ndiyo utajiri wako wa kesho.

MAKALA : MSHAHARA HAUJAWI KUMTOSHA MTU YEYOTE DUNIANI ??? HUJUI PESA YAKO INAPOTELEWA WAPI ?? MATUMIZI NI MAKUBWA KULIKO KIPATO UNACHOPATA ???!!!---- -----NA MWL . JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Basi Sikiliza Hii Siri Ya Wale Wanaofanikiwa Na Kipato Kidogo!…

Mpendwa Rafiki,

Wengi wetu tunasoma, tunahangaika, tunachapa kazi usiku na mchana,

...lakini hela inavyopatikana si sawa na inavyopotea.

Kule shule waliwahi kukufundisha (compound interest), lakini hawakuwahi kukufundisha kutokutumia hela hovyo wiki ya mshahara.

Ujuzi wa fedha ni uwezo wa....

Kujua hela yako inaingia wapi na inatoka vipi,

Kujua muda gani ni wa matumizi na muda gani ni wa kuweka akiba,

Kuweza kupangilia matumizi kabla mshahara haujalala kwenye simu.

Na ukweli mchungu ni huu:

Si kiasi cha hela unachopata kinachokufanya uwe vizuri, ni vile unavyotumia hiyo hela.

Ebu Niambie, Wewe Uko Wapi?

Hebu kuwa mkweli...

Umewahi kupata mshahara, halafu wiki ya pili unakopa kwa mpesa?

Umewahi kuwa na hela nzuri mkononi, ukajisikia *bosi* – halafu baada ya wiki mbili ukawa broke kama mwanafunzi wa form one?

Umewahi kujiambia, *Mwezi huu nitapanga matumizi vizuri,* lakini siku ya tarehe 5 mshahara ushakwisha?

Kama jibu lako ni *ndiyo* hata mara moja,

... basi wewe si mgeni kwenye kasheshe hili la kukosa ujuzi wa fedha.

Waliokudanganya Kwamba…

Hela inaisha tu bro, hakuna jinsi ya kuizuia.

Maisha ni magumu kwa kila mtu, hakuna anayefanikiwa bila kuibia watu.

Weka hela benki? Hela ya matumizi si ya kuwekwa tu!

Hizi ni kauli tunazojidanganya nazo kila siku.

Lakini ukweli ni huu....

Hela yako haitoshi si kwa sababu hujui kupata, ni kwa sababu hujui kuitunza.

Na hakuna mtu atakayekuja kukuokoa hadi uanze kujifunza wewe mwenyewe.

Na Hii Ndio Njia....

Ujuzi wa fedha sio somo gumu kama hesabu za algebra.

Ni mambo madogo sana ambayo ukiyajua, unabadilika kama saa.

Zifuatazo Ni Njia Tatu (3) Rahisi Unazoweza Kuanza Kuzitumia.

1. Tenga asilimia 10 ya kipato chako mara tu inapopatikana.

Hata kama ni buku tano, anzia hapo.

2. Andika matumizi yako ya kila siku.

Ukishangaa unavyonunua vinywaji vya 3,000 kila jioni, utajua hela zako zinapotelea wapi.

3. Jifunze njia za kuongeza kipato bila kuongeza kazi.

Huu ndio wakati wa kujua kutumia maarifa yako, sio nguvu zako tu.

Chukua Hatua....

Bro, Dada, ukikaa unasema ‘nitabadilika tu muda ukifika’, muda wenyewe haufiki.

Muda upo, ila wewe ndo hujaamka.

Kumbuka;
Maisha yako ya kesho yanatengenezwa na maamuzi yako ya leo, si mshahara wako wa mwezi ujao.