Tuesday, August 25, 2015

MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI



  
Kila    mzazi  angependelea  mwanae  afanikiwe   katika  masomo  na   kufaulu  mitihani  yake.  Pia  kila   mwanafunzi   anahitaji    KUFAULU   katika  mitihani    yake . Walimu  nao  hujisikia  vizuri  wakati   wanafunzi  wao   wanapofanya   vizuri   katika   mitihani  yao.
      KUFAULU   mtihani   ni  muhimu  kwa  malengo   ya   mwanafunzi , kwani    anaposhinda  mitihani   humwezesha   kuwa  na  mtazamo   wa  juu  kielimu ,  kwa  mfano   KUPATA  CHETI ,  DIPLOMA  AU  DIGRII, kitu  ambacho   humfanya  afae  kwenye   KAZI. Wakati   mwingine   inakuwa   ni  vigumu  kwa  baadhi  ya  WANAFUNZI  kumudu  MASOMO  na  mitihani  yao. WAKATI  HUO  HUO  wapo   baadhi  yao   ambao  wao   KUFAULU   MITIHANI  si   tatizo.
     Sasa   mtu  anaweza   kujiuliza ,  kwa  nini  WANAFUNZI   wengine   WASHINDWE   na   wengine  WAFAULU  vizuri  katika  Masomo  NA  MITIHANI  yao ?  MAFANIKIO  katika   MASOMO  na  KUFAULU  MITIHANI    kunahitaji  UWEZO  WA  ASILI , KUFANYA   KAZI  KWA  BIDII   na  KUFUATA   KANUNI   NA  MBINU  ZA   KUSOMA.
   Wanafunzi  wengine  huona   ugumu  katika  MASOMO  na  KUFAULU  MITIHANI ,  si  kwa  sababu  hawana  akili ,  bali  hawafuati   MBINU  na  KANUNI  fulani   za  KUSOMA  na  KUFAULU   MITIHANI.  WANAFUNZI   wengi   wana  uwezo   mzuri , kama   watajifunza   mbinu  hizi.
     Mbinu    na   kanuni   hizi  zinazweza   kutumiwa   na  wanafunzi  wa  SHULE  ZA   MSINGI ,  SEKONDARI ,  VYUO   na    hata   VYUO   VIKUU.

 KANUNI  ZA   KUSOMA
{1}. Weka  LENGO   maalumu  la KUSOMA   kila  siku  na   litimize.
{2}. Jiandae  kwa  mtihani  kila  wakati , usingoje  mwalimu    atangaze  kuwa  ataleta  mtihani  ndipo  usome. SOMA   KILA   SIKU.
{3}.Weka  RATIBA  ya  kila   somo   na  ifuate.
{4}.Tenga  muda  wa  kutosha   kwa  kila  somo.
{5}.Uwe  na  mahali  maalumu  pa  kusomea.
{6}.Epuka  kitu  chochote  kinachoweza  kukufanya  usisome   vizuri.
{7}.Tafuta  mahali  pasipo  na  kelele  za  aina   yoyote.
{8}.Usifanye  mambo   mengi   kwa   wakati   mmoja.Kwa  mfano ,  MAPENZI  au  ANASA   ZA   KIMWILI  wakati  ungali  mwanafunzi.Hivyo   ni  vikwazo  masomoni.
{9}.Jijengee  tabia   njema  ya  kujizuia  katika  tama  za  mwili.
{10}. Fanya   MAZOEZI  ya mwili  mara   kwa  mara.
{11}.Jiwekee   MUDA   wa  kutosha  kila  siku  kwa  ajili   ya   kazi   za   utoaji  taarifa  za   MASOMO   na  PROJEKTI.
{12}.Ni   jambo   la  busara  kuwa  na usiku  mmoja  wa  kumpumzika  katika   juma  ambayo  si   Jumapili  au   Jumamosi.
{13}.Ni  muhimu   kujihusisha  na  watu  wengine ,  jambo  hili   litakufariji  kimawazo.

WAKATI   WA  KUJISOMEA
{14}. Kabla  hujaanza  kujisomea ,  hakikisha  kuwa   zana  zote   muhimu  kwa  kusomea  zipo.
{15}.Epuka  vishawishi  vinavyoewza  kukufanya  uairishe  KUJISOMEA.
{16}.Tafuta  mahali  pasipo  na  kelele  za  aina   yoyote.
{17}.Hakikisha   kuwa    mahali    pa  kusomea   pana   mwanga  wa  kutosha.
{18}.Usisome   mambo  mengi   kwa   wakati   mmoja.
{19}.Epuka   kusoma   hadi  usiku   sana; utaharibu   afya   yako.
{20}.Jisomee  katika   MUDA   unodhani  unafaa  zaidi.
{21}.Epuka   KUSOMA    ukiwa  umejilaza  kitandani.
{22}.Uwe  na  MUDA  wa   KUPUMZIKA  kila   unapochoka   KUSOMA.
{23}.Uwe   na   muda  mwingi   wa  KUJISOMEA  kila   siku ,  usipoteze  MUDA  kwa  mambo  yasiyo  ya  lazima  kama  vile   MAONGEZI.

UNAPOKUWA   SHULENI /  CHUONI /  DARASANI  FANYA  YAFUATAYO
{24}. Fika   darasani  kwa  wakati  unaotakiwa  ili  usikose MAAGIZO.
{25}. Usikose  kipindi  bila  sababu   maalumu.
{26}.Wakati  mwalimu   hajafika  darasani ,  pitia  yale  uliyojifunza  kipindi   kilichopita.Soma  kazi   zako  zote  za  darasani  kabla  ya  kuanza   darasa.
{27}.Wakati  Mwalimu anafundisha   darasani    SIKILIZA  KWA  MAKINI  kile   anachofundisha  na  mwangalie   machoni  mwalimu  usiangalie pembeni .
{28}.Baada  ya  kipindi , pitia  yale  uliyojifunza.
{29}.Chunguza  masomo   yako  ili ujue  udhaifu  wako   uko  wapi.
{30}.Jenga  tabia    ya  UVUMILIVU  na  kamwe  usikate  tama  wakati  ugumu   unapoibuka   masomoni.
{31}.Jenga  tabia  ya   kupania  KUFAULU  katika  MASOMO  yako. AMINI  KUWA  UTAFAULU.
{32}.Usiwe  MWANAFUNZI  wa  kukaa   tu darasani,  ULIZA  na  JIBU  MASWALI  yanapoulizwa.
{33}.Epuka  kukaa   kimya  na  nyuma  ya  darasa ,  bali   shiriki  katika   mazungumzo   ya  darasani  na  wenzako.
{34}.Ni  vizuri  pia   kuwa   na   MWENZAKO  wa   kujadili  naye.
{35}.Uwe   MWANAFUNZI  mdadisi  wa   mambo  kwa  walimu  na hata  kwa  wanafunzi  wenzako   pia.

{36}. Wasilisha  kazi   za  darasani   kwa  wakati   wake.
{37}.Unapokuwa  na  matatizo   kimasomo, mwone   mwalimu   , anayehusika.
{38}.Hudhuria  shughuli  zote  za  shule  nje  ya  darasani.
{39}. Jenga  uhusiano  mzuri  kwa  walimu  wako  na  kwa  wanafunzi   wenzako.Ukiwa  na  AMANI   moyoni , utasoma  na  kuelewa.  JISTAHI   na  KUWAPENDA  walimu  wako. Ukimpenda  mwalimu  utalielewa   vzuri   somo  lake.
{40}.Epuka  marafiki  wabaya  wenye  nia  ya  kukupotosha.
{41}. Epuka  POMBE , UVUTAJI  WA  SIGARA , BANGI  na   MADAWA   YA KULEVYA.Huharibu  ubongo  na  kudhoofisha  afya.

KABLA    YA  MITIHANI     FANYA  HAYA
{42}.Kabla  ya   mtihani , SOMA   KWA  BIDII  SANA  usingoje  mtihani  umekaribia  ndipo  usome.
{43}.SOMA  kwa   mpangilio  kila  siku  ili    KUJIANDAA   kikamilifu  kwa      MTIHANI.
{44}.USIKU  unaofuatiwa   na   siku  ya    mtihani  uwe  na  MUDA  WA  KUTOSHA  WA  KULALA.
  KULALA.Usisome  hadi  usiku    wa  manane.
 SIKU   YA  MITIHANI   FANYA  HAYA
{45}.Siku  ya  mtihani , usifikirie   kushindwa   bali  uwe  na   IMANI  kuwa  utashinda.ONDOA  WASIWASI  NA  MASHAKA.
{46}.Wahi  kwenye  chumba  cha  mtihani  kwani  kuchelewa  huleta  HOFU.
{47}.Chukua  vifaa  vyote muhimu  katika  mtihani  kama  vile  kalamu, penseli  na  rula.
{48}.Soma  MAAGIZO  YA  MTIHANI  kwa   uangalifu  sana,  na  hakikisha  uko  makii  kwa  kile  unchotakiwa   kufanya   kabla  ya  kujibu  swali  lolote
{49}. Kabla  hujaanza  kujibu  maswali , angalia  maswali  ambayo  ni rahisi  kwako  kujibu.
{50}.JIBU   maswali   rahisi  kwanza  na kwa  haraka  ili  upate   MUDA  wa   kutosha  kujibu maswali  magumu.

Asante   sana   wanafunzi  wangu  wa  SHULE  ZA  MSINGI, SEKONDARI,   VYUO  na  VYUO  VIKUU  kwa   kusoma   makala  hii  nzuri sana.  Mwandishi  wa  makala  hii  ni   MWL  JAPHET   MASATU ,  anapatikana  kwa    + 255 716  924  136 ,  EMAIL,  japhetmasatu@yahoo.com ,   DAR  ES   SALAAM, TANZANIA, AFRIKA  YA MASHARIKI.
                                             
                                             MUNGU  AWABARIKI     WOTE

2 comments:

  1. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete