Namna
ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional Rafiki yangu mpendwa,
salaam Miongoni mwa ujuzi muhimu sana ambao unahitaji ili kufanikisha
malengo Yako ya mwaka 2025 ni ujuzi wa kuipangilia wiki yako. Wiki ni
ndogo sana ila usipoipangilia vizuri inapotea na ukipoteza wiki nyingi
mfululizo, mwisho wa siku unakuwa umeupot
Sasa ya nini uupoteze mwaka mzima wakati Kuna uwezekano mzuri tu wa
kufanya makubwa kwa kuanza kitu kidogo kama kuipangilia wiki yako.
Anza wiki hii kuipangilia kila wiki yako.
Ni majukumu gani uliyonayo?
Ili kuipangilia wiki yako kiprofessional, anza kwa kujiuliza ni majukum gani yaliyombele yako kwa wiki inayofuata?
Kisha yapangilie kulingana na umuhimu. Majukumu ambayo ni ya muhimu zaidi yape kipaumbele kwanza.
Kwenye siku yako usipange vitu VINGI VYA kufanya.
Ukiweza kuwa na vitu vitatu tu vinatosha, vikizidi visiwe zaidi ya sita.
Hii itakusaidia kufokasi kwenye mambo machache ila utakayoyawekea NGUVU
kubwa na kuyafanikisha pia.
Unavyoianza wiki yako pia, hakikisha wiki hii unapanga muda wa kujisomea vitabu.
Inashangaza kuona kwamba watu wanapangilia mpaka muda wa kula ila
hawapangilii muda wa kujisomea. Changamoto kubwa ni kwamba, tumbo likiwa
na njaa huwa linapiga kelele. Ndiyo utasikia mtu anasema; “nina njaa“.
Ila akili yako ikiwa na njaa haisemi. Ila ilipata utapiamlo wa akili,
utazidi kuwa nyuma mara zote. Hivyo, fanya kadiri uwezavyo kuhakikisha
kwamba, kila siku unapata muda wa kujisomea.
Pata kozi yoyote fupi. Online kuna kozi nyingi fupi.
Kwenye ratiba yako weka muda wa kujifunza kozi yoyote fupi kuhusiana na
eneo ambalo ungependa kulifahamu kwa undani. Inawezekana Hilo eneo
tayari unalifahamy vizuri tu, lakini Kuna jambo moja au mawili unaweza
kujifunza kuongezea au kutanua kile ambacho tayari unajua.
Siwezi moja kwa moja kukwambia ujifunze kozi gani, ila fahamu ya kuwa
kozi za namna hii zipo nyingi. Ni juu Yako kujua wapi unahitaji
KUWEKEZA NGUVU ili uwe Bora zaidi. Maeneo ya kujifunza na kupata kozi
kama hizi pia ni mengi, mfano skillshare, Udemy, Coursera, learn digital
with Google, na nyingine nyingi kama zinavyoonekana kwenye picha hapo
chini.