Monday, June 15, 2015

SIRI YA UTAJIRI ----NJIA ZA KUPATA PESA NA UTAJIRI


 
Watu   wengi  hujiuliza ,  SIRI   YA  UTAJIRI  NI   NINI ? “  Je  ni  mbinu  gani  zinaweza   kumsaidia  mtu   kupata  UTAJIRI ?  Siri  kubwa  ya  UTAJIRI  ni   kuwa   MBUNIFU, unabuni  njia  mbalimbali  za  kuingiza  kipato   yaani  unatega  MITEGO / MIRADI. Kadiri   unavyotega   mitego  ndivyo  unavyo  nasa   FEDHA  zaidi .
Lazima  ubuni  kitu   chochote  kinachoweza    kutoka  kama  BIDHAA   au  HUDUMA.Unapotoa  bidhaa  unapata  FEDHA  kwa   kadiri  ya   bidhaa  uliyotoa.Na  unapotoa   huduma   utalipwa  na  inawezekana  ukalipwa  kwa  masaa, siku , wiki  na  hata  kwa  mwezi.
TAMBUA  HILI :  Fedha  haina  mwenyewe , wala  upendeleo, si  za  watu   wa  kabila  au   taifa  fulani , tabia  mojawapo  ya  fedha  ni  kwamba   hufuata   MTEGONI  AU   MRADI uliobuni.  Hivyo  jifunze   kutega   mitego  mbalimbali  ambayo  mwisho  wa  siku , mwezi  au  mwaka  utasema  umepata  fedha. Fedha   zipo  kila  mahali   yaani  mijini   na   mashambani. Hutembea  huku  na  kule zikifuta   mahali   imewekewa  MTEGO.
Fedha  hufuata   mbunifu !  hutoroka  mvivu ! hutembea  huku na  kule ,hupenda   mwerlevu , n.k.  hufuata  na  kuingia  kwa  Yule  anaye  zitengenezea njia  na  mahali  pa  kuingia.
HAKUNA  MUUJIZA  WA  KUAPATA  FEDHA  !! Usidanganyike  kwamba  utapata  muujiza wa  fedha   ukuangukie  kama  palachichi , pesa  zinatafutwa   zinategewa  mitego , zinaweza  kutoka  kwa  mteja, ndugu ,  rafiki , au  Mungu  akatumia  mtu  yeyote  kukupa  fedha, kitendo  ambacho  tunakiita   muujiza , na  wala  sio  mtu  anakaa  hafanyi   chochote, ati  anangojea   muujiza  wa  fedha, ndio  maana  wengi  hawana  kitu.

ACHA   UVIVU : Usiwe  mtu  wa  kukaa  bila  kufanya   kitu,  hata  kama    huna    kazi   tafuta  kazi  ambayo   itakupatia   kipato  bila  kusahau  KUWEKA  AKIBA ,asilimia   20   ya   kipato  chako   usitumie  yote  hata  kama  mshahara  ni   mdogo  kiasi  gani. Usijali  muda,usiwe   na  haraka . Baada  ya  miaka  kadhaa,unaweza  kuwa   na  MTAJI  mkubwa  wa   kuanzisha  shughuli  yako  yoyote , iwe  ni  biashara au   vinginevyo . Tumia  hicho  kipato    kuanzisha   kitu  chako. Wewe   acha  sababu  zisizo  za   msingi  ambazo  wengi   hujifariji  nazo  na  kumbe  ni  WAOGA  na  wasiotaka  KUTHUBUTU  kufanya  jambo,
Mtu  mvivu  husema , simba  yuko  nje, nitauawa  katika  njia  kuu.  {  MITHALI  22:13

 Wengi  wana  sababu  nyingi  hasa  vijana   wanasingizia  serikali  haitaki  kuwapa  AJIRA !!!  Vijana   dunia  ya  sasa  ni  UJASIRIAMALI  SIYO  AJIRA  YA  SERIKALI. Walioko  katika  AJIRA  YA  SERIKALI  wanapata   shida  sana   kwa  kutegemea  mshahara !!  Hautoshi !!! CHUKUA  KARATASI   NA  KALAMU TUFANYE   MAZOEZI  MAWILI   TOFAUTI   TUUONE  UKWELI   WA  MAMBO !!
     Hebu  chukua  karatasi  na  uandike  orodha ya  mahitaji  yako mfano kutoa  michango  ya  arusi ,msiba n.k. kulipia  umeme ,kugharamia  chakula  kila  siku ,kumlipa  mshahara  mfanyakazi  wako  wa  ndani , kununua  vocha   za  simu , kununua  nguo/mavazi , kulipia  nauli/ usafiri ,  kulipia / kununua  maji  , kutengeneza nywele  saluni, kugharamia  huduma   za  internet , kutoa  sadaka, zaka  na  changizo  mbalimbali  kwenye  dini  zetu ,  kuhonga—unacheka   hiyo  ipo , kulipia  matibabu,  n.k.
Orodha  ni  ndefu   sana  ya   mahitaji   yetu   ndugu  zangu  watanzania. Fanya  zoezi  la   pili   chukua karatasi   na   andika   Orodha  ya  vyanzo  vya  mapato  YAKO  yaani  MIRADI / MITEDO  YA  FEDHA !!   Vipi  mbona   washangaa ANDIKA  !!!!  HAKUNA !!  BASI  SAHAU   SUALA  LA  KUWA  TAJIRI  KAMA  HAUTACHUKU A  HATUA !!! 
Unaona   sasa  Mishahara  haiwezi   kutosheleza  mahitaji  yet  hata  kidogo !!


USHAURI  WANGU : Wewe  uliye  na  kazi  zako  au  za  watu   yaani  waajiriwa   , jitahidi  sana   uwe  na  shughuli  zako  ambazo  zitakuingizia  kipato  cha  zaidi. Jitahidi  hata  kama  una  shughuli  zako  kama ilikuwa  moja, ziwe  mbili, tatu  au  zaidi. Tumia  kipato  cha  mshahara  wako   KUWEKEZA.

JE, WAJUA ?  Kila  shughuli  au  kazi  yoyote   utakayoibuni  ujue  mna  faida , hivyo  huna  budi  kuifanya  kwa  moyo  mmoja  ukijiua  kupitia   hiyo  shughuli   au  kazi   ndiyo  itakayo  kuletea   Mafanikio  ya     kifedha.
Katika  kila  kazi  mna  faida , bali  maneno  ya   midomo  huleta  hasara  tu.  {  MITHALI   14:23 }.

WENGI   WANASEMA  HAWANA   MTAJI  WA   BISHARA .  NDIYO  SABABU  YA  KUTOFANIKIWA  KIMAISHA.  JE, NI  KWELI  ?  Cha  msingi  ni  kuwa  na  nia   ya  kufanya  kitu, . MTAJI  sio  tatizo , tatizo  ni  kutokuwa  tayari  na  kukosa   ubunifu  wa  kufanya  kitu. Unapokuwa  na   nia  mtaji   utapatikana    maana  PENYE   NIA   PANA  NJIA. MTAJI  unaweza  kupatikana   toka  kwa  wale  walio karibu   nawe, ndugu, marafiki  au  taasisi   za  kifedha.  Uoga  wa kuthubutu , Kutojitambua ,  uvivu  , kukosa   maarifa , ujuzi, elimu  sahihi  ya  biashara  na  mbinu  za  kutafuta  fedha  ni   miongoni  mwa  mambo  yanayotufanya   na   kutukwamisha  tusifanikiwe.  Nitaeleza  kwa  kirefu  njia  mbalimbali  za  kupata   MTAJI    katika  makala  yangu yenye  kichwa  NI  VIPI  UPATE   MTAJI ? ndani  ya  blogu  hii . MAISHA   NA   MAFANIKI  BLOG

 

 
NINI  TOFAUTI    YA    MASKINI  NA  TAJIRI  ?
    Tofauti  kati  ya  MASKINI  na  TAJIRI  iko  katika  kuchukua   hatua. Tajiri  hujifunza  mambo  ya  kumwendeleza   na  KUCHUKUA  HATUA  AU   KUTHUBUTU  kwa   kutekeleza  kwa  vitendo  yale  anayojifunza  na anayoyaona   yanaweza   kumuinua  kiuchumi.MASKINI  huwa  anajifunza  mambo  na  kuyaacha  kichwani  bila  kuchukua  hatua  au  kuyafanyia  kazi   aliyojifunza  na  hivyo   FURSA  ya  KUPATA UTAJIRI  inampita  hivi  hivi.
Siri   kubwa  ya  UTAJIRI  ni   kujifunza  elimu   ya  kutafuta  mtaji , kuwekeza  kwa  busara   kwa  namna  ambayo  daima  panakuwa na  ziada   na  faida.  Kwa  bahati   mbaya  sana, elimu  hii  haifundishwi   darasani  ila  wanayo   wafanyabiashara  wachache  na  kila  anayefanikiwa  kuifunza  siri  hii  huwa  TAJIRI  na  huendelea  kuificha.


    NJIA     ZA  KUKUWEZESHA  KUWA  TAJIRI
{1}.Wataalamu   na  Watafiti  wa  masuala  ya   fedha  wamegundua  njia rahisi ya  kupata UTAJIRI ambayo   haihitaji   uwe  na  kipato  kikubwa,  kama  unafanya  kazi   na    Kipato   chako ni  kidogo  anza  LEO kujenga tabia  ya kuweka AKIBA  ya  T.shs  1,000 kila  siku  sawasawa  na  TShs  30,000  kwa  mwezi , matokeo  yake  ni  kwamba   kama  utaweka  AKIBA  yako  kwa  kipindi  cha  miaka  65  ila  riba  yoyote  utakuwa  na  AKIBA  ya  Tshs  23,725,000 { Milioni  Ishirini  na  Tatu  Mia  Saba Ishirini  na  Tano  Elfu }. Kama  utawekeza  fedha  hiyo  na  kuapata   riba  ya  asilimia  10%  kwa  kila  mwaka  itazaa  na  kukuletea  Tshs  2,750,000,000 { Bilioni  Mbili  na  Milioni  Mia  Saba  Hamsini }.


{2}. Unaweza  kurithi  mali  na  fedha  kutoka   kwa  wazazi   wako. Hii  ni  njia   ya   kubahatisha   kwani  watu    matajiri  siyo  wengi   na  hivyo   watoto  wenye  bahati  kama  hii  ni  wachache pia. Nikiwa  kama  mwalimu   na  mwelimishaji huwa  nawaambia  wanafunzi  wangu wasome   kwa  bidii  sana   wafaulu  mitihani  yao  na  kuendelea  mbele kielimu ,  wasitegemee  sana  mali   na  fedha   za  wazazi  wao . Katika  familia  zetu  hizi  za  kitanzania suala  hili  haliko  sawa  huleta   migogoro  sana  kuhusiana  na  mali  na  fedha  za  wazazi . Watoto  hugombana  sana  mpaka  kupelekana  mahakamani . Katika  familia  zetu  hizi  watoto  ni   wengi , mali  ni  chache . Katika   familia  zenye  ndoa  za  mitara,   tatizo  hili  kubwa  sana . Haliwezekani   kabisa. Zipo  familia  chache  sana   waliofanikiwa  kuwarithisha  watoto  wao  fedha  na  mali  bila  migogoro  miongoni mwa  watoto.
  Kwa  wenzetu   nchi  zilizoendelea   inawezekana  kumrithisha  mtoto  fedha  na  mali   kutoka  na  mifumo  yao  maisha  ipo  vizuri.  Familia  zao  zinajali  sana  kuhusiana  na  idadi  ya  watoto  wanaozaliwa  huku  kwetu  Afrika hatujali  sana  kuhusiana  na   uzazi   wa   watoto  na  matunzo  yao . Huku  kwetu  urithi  wa  mtoto no  elimu  tu.


{3}.Unaweza  kusomea   ujuzi  au  utaalamu  katika  fani  yenye  malipo   mazuri  na   KUJIAJIRI  mwenyewe. Kwa  mfano , unaweza  kusomea  fani   kama  UANASHERIA , UHASIBU, UDAKTARI,UFAMASIA ,  UFUNDI , UALIMU, SANAA, UFUNDI  WA VIFAA  VYA  ELEKTRONIKI, n.k.  Unaweza  kuanza  kwa  kuajiriwa  kwenye  ofisi  inayotoa  huduma  ya  fani  yako  ili  upate  uzoefu  na  siri  ya  biashara  au  kazi  hiyo.  Kisha  tafuta  kuanza   taratibu  kufanya  kazi  zako  binafsi. Ukiona  biashara  yako  inaenda  vizuri  acha  kazi   na  uende  kufanya  biashara  yako   kwa   juhudi  na  maarifa  yako  yote  na  UTAFANIKIWA.
 Tafadhali  sana  msomaji  wangu   kama  ni  wewe  au   ndugu  yako  au  rafiki  yako   usimshauri   kuacha   kazi  ya  kuajiriwa  haraka  !!! Wanafunzi  ambao  wapo   vyuoni ,  mashuleni    huwa  nawaambia  ukweli   njia  ya  uhakika   na  nzuri   ni  kusomea   ujuzi  au  utaalaamu   na  kuwashauri   KUFANYA  JUHUDI  KATIKA  MASOMO  YAO  ILI  WAFAULU  VIZURI !!


 
 


{4}.Kuwa  na  BIASHARA    yako  na   kuiendesha  ili kupata  ziada  na   faida kubwa. Anza  kufanya  UTAFITI  kuona  utafanya  biashara  gani.

{5}. Unaweza  kutunga   VITABU    juu  ya  suala   lolote  unalolijua.Kwa  mfano  Unaweza  kutunga  kitabu  kuhusu  suala  lolote  ambalo  linaweza  kuelimisha  jamii  au  kuburudisha  jamii. Kwa  mfano  unaweza   kutunga   kitabu   cha  hadithi  na  unaweza  kueleza   jambo  lolote  linalogusa  jamii. Au  Kama  wewe  ni  mtu   uliyebobea  katika  masuala  ya  muziki   unaweza    kutunga  kitabu  kinachofundisha   namna   ya  kuwa  mwanamuziki. Watunzi  wengi  wa  vitabu  ni  Matajiri  wakubwa. Hii  Ni  kazi    unayoweza  kuifanya  kwa  shida  mwanzoni  na  mara moja   lakini   ukavuna  matunda   yake    kwa  muda  mrefu.


{6}.Unaweza   kuwa   MBUNIFU  na  kuanza  kuuza   mawazo  yako  au  kutumia  chombo  ulichokibuni  kukuingizia  fedha.


{7}. Unaweza  kuendeleza  VIPAJI  vyako  na  kuwa  mwanamichezo  au   msanii  wa  kulipwa. Usidharau   kipaji  chako   chaweza  kukutajirsha   sana . Kwa  mfano  kipaji  cha  ualimu , uimbaji , ususi , uchoraji , uimbaji, kupiga  vyombo  vya   muziki , kucheza   mpira  wa  miguu ,  n.k. Kila   mtu –kila   mtu  hata  wewe  msomaji  wangu, umepewa  kipaji  na  mungu .Hakuna  mtu  asiye  na  kipaji. Wengi  wetu  tuna  tuna  vipai  zaidi  ya  kimoja{ multigifted}.Nitaeleza  kwa   vizuri   na  kirefu  kodogo    katika   makala  yenye  kichwa  KITUMIE  KIPAJI  CHAKO  KIKUTAJIRISHE
{8}. Unaweza  kucheza  bahati    nasibu   na  kushinda.Watu   wengi  wanapenda  kucheza  michezo  ya   kubahatisha . Hiki  ni  kitu  cha   kubahatisha  uwezekano wa  kutajirika  kwa  njia  hii  ni  mdogo  sana.Hivyo  nawashauri  wasomaji  wangu  kuachana  kabisa   na  njia   hii  ya   kutafuta  UTAJIRI.

{9}. Kama  wewe  ni  Mwajiriwa , kipimo  chako  cha  Mafanikio  kiwe   ni  kujiuliza  swali, kama  utaacha  kazi  yako  ya  Mshahara  utaweza  kuishi  kwa  kutumia  kipato  chako  cha  pembeni  kwenye  biashara  yako  kwa  muda  gani ? Mafanikio  yako  yatakuja  pale  utakapoweza  kutumia   kiapto  chako  cha  ziada  bila  kutegemea  mshahara ,  na  hapo  ndipo  unaweza  kuacha  kazi  na  kwenda   Kuimarisha  biashara  zako  au  kuendelea  na  kazi  huku  pia  ukijiaamarisha  kibaiashara.
{10}.Panga  malengo  ya  muda  wa  mwaka  mmoja , miaka  mitano  na  miaka  ishirini  ili  kuhakikisha  kwamba  unajikomboa  kiuchumi. Malengo  yako  makuu  yawe  n :--  Kuwa  na  AKIBA  ya  fedha   za   kutosha  katika  akaunti  yako , kuwa  na  biashara  yako , na  VITEGA  UCHUMI  VYA  AINA  TOFAUTI  ambavyo  unaweza  kuvisimamia  vizuri.
{11}. Jifunze  mbinu  za   kutafuta   fedha. Njia  rahisi  na  ya  uhakika  ya kukuwezesha  kufanikiwa  kiuchumi  katika  maisha  ni  kutafuta  MSHAURI  AU  MTAALAMU  anayejua  mbinu  za  uongozi  wa  biashara  ili  akushauri  vizuri  juu  ya  yale  unyonuia   kutekeleza. Pia  SOMA  VITABU   VYA  BIASHARA  ili  uweze  kupata  maarifa  mapya !! Ndugu  Msomaji  wangu  MAARIFA   NI  NGUVU.

Kwa  kuhitimisha  nasema  fedha  ni  chombo  cha  muhimu  sana  kwa  kila  mtu  anayeishi  chini  ya  jua  au  dunia  hii  kwa  kukidhi  mahitaji  muhimu  ya  kibinadamu. Ni  chombo   kinachotumika  kuhalalisha  mambo  baina  ya  pande  mbili  yaani  kwa  MTOAJI  na  MPOKEAJI  katika  kulinganisha  mapatano  yaliyofikiwa  katika  hali  ya  kununua  au  kuuza.Ni  chombo  ambacho  kila  mtu  anahitaji  kuwa  nacho.
Neno  la  mungu  linasema  fedha  na  dhahabu  ni  mali   ya  MUNGU  na  wala  sio   ya  shetani. Kama  fedha  ni  mali  ya  mungu  na  sisi  tu  watu  wake  basi  tunayo  haki ya  kumiliki  na  kuwa  nayo  katika  hali  ya  utele.

 

 

Fedha  na  mali  yangu  na  dhahabu  ni  mali  yangu, asema   BWANA  wa  MAJESHI {  HAGAI  2:8 }

Makala  hii  imeandikwa  na  MWL   JAPHET  MASATU ,  anapatikana  kwa namba  + 255 716  924 136 /  +  255  755  400  128 /  +  255 785  957   077.  Kama  una  lolote  unataka  kuchangia   mawazo , ushauri   kuhusiana  na   mada  yetu  hii  SIRI  YA  UTAJIRI .  Karibu  sana.
Kama   unataka  kuniuliza   swali   kuhusu  mada  yetu    hii  uliza   !!!

 ASANTE  MSOMAJI  WANGU  KWA  KUSOMA , MUNGU AKUBARIKI

7 comments:

  1. Ni Somo zuri sana thnks mwl .japhet

    ReplyDelete
  2. Natakuwa tajiri Mimi... No somo hili limenipa hamasa kubwa

    ReplyDelete
  3. Natakuwa tajiri Mimi... No somo hili limenipa hamasa kubwa

    ReplyDelete
  4. Uzidii kuelimisha wanajamii
    Ubarkiwe mno.

    ReplyDelete
  5. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)


    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU

    ReplyDelete
  6. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)


    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete
  7. UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    (Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)

    MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    Everyone

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete