USIWE BENDERA FUATA UPEPO
Kila siku asubuhi
tunapoamka tunafanya chaguzi
nyingi sana kuhusu
maisha yetu kwa
siku hiyo. Huwa tunachagua
kuoga au hapana , kupiga mswaki
au la.Huwa tunachagua
kama tunywe chai au hapana.Huwa tunachagua
tuvae nguo gani , na
kwa akina mama
tuziweke vipi nywele
zetu.Vile vile, huwa tunachagua
tupite njia gani
kuelekea kwenye shughuli
zetu.
Hebu jaribu
kujiuliza kama huwa
unachaguliwa au kuamuliwa
na mtu mwingine
yeyote katika kufanya
mambo hayo unapoamka
asubuhi nyumbani kwako.Bila
shaka , wengi wetu huwa
tunachagua wenyewe .Ndugu yangu
kila tunachofikiri ,
tunachofanya au kukisema
maishani , huwa ni uchaguzi wetu .
JE, WAJUA
HILI ? KUFANIKIWA au
KUTOFANIKIWA maishani ni suala
la uamuzi wetu
wenyewe, kama vile tunavyoamua
kuoga au kutooga
asubuhi kabla hatujatoka
nyumbani kwenda kwenye
shughuli zetu.
Sisi ndiyo tunaochagua
maisha yetu yawe
vipi. SISI NDIYO
WAAMUZI.Kwa sehemu kubwa , mambo tunayofanya
ni matokeo ya MAZOEA.Ukishajenga mazoea
fulani , huwa unafanya bila kujiuliza
na wakati mwingine
hujui kama unafanya.Hata
pale unapojua kwamba
unafanya na kujua
kwamba kufanya huko
kunakuumiza , unaweza
kushindwa kujitoa kwa
sababu moja tu----MAZOEA.
Kwa mfano, Mvuta
sigara anaweza kujua
kwamba sigara inamuumiza
kiafya , mnywaji sugu wa
pombe au mzinzi
naye ni hivyo
hivyo , lakini kujitoa inaweza
kuwa vigumu sana
kwa sababu ya
MAZOEA. Watanzania wengi huishi
kimazoea !!
Kama tunajitahidi
sana maishani bila
Mafanikio, ni lazima turudi
nyuma na kuanza
kukagua tabia zetu
ambazo zinatokana na
namna tulivyoamua kuyatazama
maisha.Kama tunachotaka maishani { mafanikio } hakipatikani ,
inawezekan ni kwa
sababu tumechagua aina
ya maisha ambayo
haiwezi kutupa mafanikio , hivyo inabidi
tukubali KUBADILIKA na KUINGIA
kwenye KUCHAGUA aina
ya maisha itakayotunufaisha.
JIFUNZE
SIRI HII : Naomba nikueleze
siri ndugu yangu, watu
matajiri na waliofanikiwa
ni wale ambao
hufanya mambo kwa tofauti, ni WANAUME
na WANAWAKE mbao
wanaamka wakati MASKINI
wanaendelea kulala na
kukoroma katika maisha
yao. Likiwa kama jambo
la uhakika , watu matajiri
na wafanikiwa wakubwa
ni watu wasiolala.Watu MASKINI
hupenda kulala sana !! ACHA
MAZOEA YA KULALA SANA!!
Watanzania wengi hupenda
USINGIZI KUPITA KIASI ! NDIO MAANA
NI WENGI NI
MASKINI !
Ni ukweli
usiofichika kwamba, watu wengi
wameelewa kwamba, wakati watu
wanapolala na wakati
kila mahali pakiwa
kimya bila kelele , ndipo wao
wanapowaza mawazo ya
kujenga.
Cha kushangaza
ni kwamba , watu wachache
tu ndio waliofanikiwa
katika mataifa mengi
duniani. Nenda kawaulize washerekeaji
wa mafanikio katika
eneo lolote lile, kama vile biashara
kubwa ya ujasiriamali , inayosukuma na
kushawishi wengine,
watakuambia kuhusu ukweli
huu. Ni wale wanakaa macho
wakati wa usiku
wakifanya kazi , kutafakari ,
wakipanga mipango na kuyafanyia kazi
matamanio yao, wanacheka na
kuchukua vitu kirahisi . Siku inapoisha
wengine wanahangaika ,
wakisukumana na kufukuzana
katikati ya makundi
ya watu wanaopiga
kelele mitaani , katika maofisi na
sehemu za masoko.
WAKATI WA
USIKU NI MZURI SANA
KUUTUMIA : KWANINI ?
MATAJIRI wengi wamejikita
zaidi katika muda
wa usiku ambapo
hakuna washindani wengi
zaidi wakati hakuna
kusukumana na haraka, hakuna kelele
zitakozozuia kuwaza kwao
na nafsi zao.Watu wengi
ni MASKINI kwa
sababu wanalala kupita
kiasi hawana muda
wa kutafakari,na kupanga
mipango na kuyafanyia
kazi malengo yao. Tumepewa na mwenyezi
MUNGU muda wa saa 24
tuutumie vizuri ili
kuboresha MAISHA yetu ! Watanzania
tubadilike sasa ! Haina maana
ya kwamba ukeshe
usilale ndugu yangu, hapana ni
kuwa na MUDA
WA KUTAFAKARI, KUPANGA MIPANGO, KUFANYA KAZI .Usiku
ni muda mzuri
kutokana na UTULIVU
ULIOPO tofauti na
mchana.Na wewe ndugu
yangu Mtanzania tumia muda
wa usiku KUFANYA
MAMBO TOFAUTI YA
UBUNIFU ! Sisi binadamu tunapaswa
kuwa wabunifu kwahiyo tunahitaji
muda wa ziada
ili kuwekeza nguvu zetu, mali
zetu , na muda wetu
kwenye ubunifu wetu.Tuutumie
USIKU kwa kutafakari mambo
yetu ya ubunifu !
NENO LA
HEKIMA : “ Kama ni
lazima upate amana
ya pesa na
kuwa na pesa
zisizo na mpaka, jifunze kutumia
nyakati zisizo za
kawaida kwa ajili
ya kuwaza uzalishaji “
KWA WANAFUNZI : Akili ya
binadamu huhitaji utulivu na
ukimya wakati wa
kujisomea. Usiku ni muda mzuri sana
kwa mwanafunzi kujisomea.Hakuna kelele za
aina yoyote , watu wamelala !!KANUNI INASEMA Ili uamke
usiku kujisomea unahitaji “KULALA
MAPEMA ILI UAMKE MAPEMA”
Ukiwa unalala kwa
kuchelewa zoezi la
kuamka usiku ili ujisomee litakushinda
mwanafunzi wangu! Kama unahudhuria
prep. Lala saa 4 usiku,amka
saa 10 . Kama huudhurii prep. Lala
saa 1 au saa
2 usiku na amka
saa saa 9 usiku! Uwe
na muda wa kupumzika kila dakika
45 au saa 1.
Muda wa
saa 2 au 3 kwa kusoma
unatosha sana.
Siyo lazima usome usiku, pia
inategemea wewe mwenyewe
mwanafunzi ni wakati
gani mzuri kwako kwa
kujisomea ? je, ni asubuhi, mchana au jioni !
USISOME KIMAZOEA !usifuate mkumbo , wenzako wamefanya
hivi , na wewe waiga !
wenzako wanapiga stori darasani muda
wote nawe wajiunga ! ACHA HIYO ! kuwa
wa tofauti jali muda wako
kimasomo zaidi. Na utafanikwa ! HESHIMU RATIBA
YAKO BINAFSI, RATIBA YA
SHULE, WAHESHIMU WAZAZI/
WALEZI WAKO,NDUGU ,MAJIRANI, WALIMU WAKO
SHULENI , WANAFUNZI WENZAKO,
WASIOJIWEZA/ YATIMA nk.
Kanuni inasema, “ If
you wake up early ,
you need to
go to bed
early. If you keep up
late, you need to
wake up late. “
maana yake “
Kama unataka kuamka
mapema, nenda ukalale mapema. Na
kama unataka kuamka kwa
kuchelewa , kalale kwa kuchelewa !
Tafadhali mwanafunzi potezea
mambo ambayo yatakupotezea
muda kama masuala
ya mapenzi, disko, kuangalia video/tv, kulala kupita kiasi, kunywa
pombe,kupiga stori, n.k.
Siku zote
usikubali kuwa mtu wa
kawaida. FANYA YALE
YA TOFAUTI. USIISHI KIMAZOEA
KAMA WATU WENGINE !!
BADILIKA , KUWA WA TOFAUTI, MAFANIKIO NI
YAKO !! USIWE BENDERA FUATA
UPEPO !
Kwa mfano , mimi
binafsi huwa naandika
makala zangu hizi wakati
wa usiku wakati watu wengine
wamelala. Huwa napenda kujisomea usiku ! Kwangu binafsi
usiku naupenda sana
kwa kufanya masuala
yangu ya kiubunifu ! Huwezi ukatumia muda
wa MCHANA pekee
kufanya mambo yote , ni
lazima pia uutumie
USIKU kama kweli
unapenda kupata MAFANIKIO
MAISHANI !!
USINGIZI HULETA
UMASKINI !
Utalala hadi lini
ewe mtanzania goi goi ? Lini
utazinduka kutoka katika
usingizi wako ? “ Bado
kulala kidogo, bado kusinzia
kidogo, bado kukunja mikono
upate usingizi.Hivyo UMASKINI
wako huja kama
MNYANG”NYANYI na uhitaji
wako kama mtu
mwenye silaha.” { MITHALI 24:33,34 }.
MITHALI
26:13 inasema : “Mtu mvivu
husema, simba yuko njiani.Simba
yuko katika njia
kuu .” Ni nini
asemacho mtu mvivu ? Hujitoa kwenye
majukumu yake. Anapenda kukaa
nyumbani na kukifanya
kitanda kuwa rafiki
yake.Mtu mvivu si
mbunifu.Huogopa kuthubutu.
Hupenda kukaa na
kujifariji.
USHAURI
WANGU ! Kama una
nia ya kutengeneza
PESA , hunabudi KUPIGANA NA
UZEMBE. Usiufanye USINGIZI kuwa
rafiki yako kwani
huwezi kutengeneza PESA
kitandani.WEWE NI
MASKINI KWA SABABU
UNALALA .UKWELI NI KWAMBA
, USINGIZI umewakaba watu wengi
na kupoteza HATIMA
zao. Watanzania wengi ni
wavivu , wazembe , wanapenda
kulala kupita kiasi. Maandiko matakatifu
yanasema “ Ukipenda Usingizi utakufa
Maskini “ Yaani KULALA
KUPITA KIASI. Mwili huhitaji
saa 8 ili kuendelea
kufanya kazi yake
kama kawaida .Ukilala pungufu
ya hapo , ni lazima
utalipia usingizi uliobaki
popote pale haijalishi
upo wapi ! Hii ni
suala la kimaumbile
zaidi .
Mungu anamchukia
mtu mvivu ndugu yangu ! “ Uvivu humtia mtu
katika usingizi mzito, na
nafsi yake MVIVU
itaonja njaa” { MITHALI 19:15 }. Mungu anatutarajia
tuwe tunaamka mapema
na kufanya kazi
kwa bidii popote
pale alipotuagiza.Kwahiyo ndugu
yangu mtanzania , usifuate mambo
yaliyozoeleka na ya
kawaida.Tuache kuishi kimazoea. CHAGUA KUWA
TOFAUTI !! JITIISHE MWENYEWE KUWA
TOFAUTI. INAWEZEKANA, NA
UNAWEZA KUFANIKIWA !
NENO LA
HEKIMA “ Lazima uwe
tofauti ! Utofauti wako
ndio ushawishi wako, Ushawishi wako
ndio Utajiri wako “
{ Greg O. lyoha }.
Kama
tunaamka asubuhi na
kuchagua kwamba siku
itakuwa ngumu na
mambo hayataenda vizuri , ni
wazi huo ndio
uchaguzi wetu na
ni kweli itakuwa
ya hovyo kwetu
kumbuka tunapata kile
tunachochagua.Tukiamka na kufikiria
kinyume na hayo ,
ni wazi
mambo yatakuwa kinyume , yaani yatakuwa
mazuri.
Asante
msomaji wangu, HUJACHELEWA , UNAWEZA
KUFANIKWA. Endelea kutembelea
blog yako hii kwa
kujifunza zaidi ! Mungu
akubariki sana !
Makala hii
imeandikwa na MWL.
JAPHET MASATU.Ni mwelimishaji
na mhamasishaji katika
masuala ya maisha
na mafanikio ,Saikolojia ,
biashara / ujasiriamali . Anapatikana
kwa + 255 716 93 4236 / +
255 755
400 128.
japhetmasatu@yahoo.com
No comments:
Post a Comment