KUCHORA PICHA AKILINI , ni njia iliyofanyiwa utafiti na imewaletea watu mafanikio. KWA NINI ?
UNAPOWAZIA KILA SIKU KUPATA KITU FULANI , BASI NI KAMA SAWA UMEJIPA KAZI YA KUKIPATA. Njia za kupata kitu hicho lazima zitaibuka.
KWA MFANO , umetunga taswira unamiliki GARI LA KISASA aina ya RANGE ROVER VOGUE na uko na jamaa na ndugu wanakupongeza , unadhani utaishia hapo ? HAPANA ! Ni hivi. Unaweza kujikuta ukilazimika kuzungumza na watu mbalimbali ambao unaona kwamba wanaweza kukusaidia. KWA NINI ?
Kwa sababu kuna nguvu iko ndani ya mwili wako ambayo ilichora picha ya GARI LA KISASA aina ya RANGE ROVER VOGUE nzuri na ndugu wanakupongeza , na sasa inataka {kitu} GARI LA KISASA aina ya RANGE ROVER VOGUE hiyo itokee kweli.
KAMA PIA , utatunga taswira kwamba UNAMILIKI PESA NYINGI ,akili itakuwa na FURAHA na AMANI. Ajabu na kweli ! Baadaye unaweza kumiliki pesa nyingi. Hii ni kwa sababu , AKILI INA NGUVU YA KUTENGENEZA PICHA AMBAYO BAADAYE INAWEZA KUWA KWELI. Tunapotengeneza picha kuwa tumepata pesa , tunachochea nguvu ya ajabu kutoka miilini mwetu , ambayo inataka pesa hizo zitokee kweli katika uhalisia. Huwezi kupata PESA ilhali mawazo yako , yametawaliwa na kukosa PESA. Anza kufanya leo ndugu yangu , utaona ajabu kubwa !
WATANZANIA WENGI HAWAAMINI KUHUSU KUTUNGA TASWIRA AU PICHA ! KWANINI ?
Kuna baadhi ya watanzania ambao huona kuwa kutunga taswira au picha hakuna maana. Hawa ni kwa sababu hawafahamu kuhusu jambo hili.
JIFUNZE SIRI HII : WASANII wengi , WAANDISHI na WANASAYANSI wameweza kufanya maajabu makubwa kutokana na utungaji wa taswira au picha.
MWANARIADHA mmoja wa nchini KENYA , alishinda MAREKANI medani ya dhahabu katika shindano la riadha mwaka 1999.Alipohojiwa kueleza siri ya ushindi wake , alisema :
"Muda mchache kabla sijaingia katika uwanja wa mashindano , nilivuta taswira kwa kuwaletea washindani wangu akilini. Nilichora picha akilini kuwa tuko uwanjani tunakimbia na ninawapita wote. "
Wanariadha ambao hufanya zoezi hili la kutunga taswira mara nyingi wamefanya vizuri na kutunikiwa zawadi.
KWANINI WANAMICHEZO WA TANZANIA HUFANYA VIBAYA KATIKA MICHEZO ? Sababu inayopelekea watanzania kushindwa katika michezo mbalimbali ni kwamba hawaamini au hawajui jinsi gani suala la utungaji taswira au picha kabla ya kuingia uwanja wa mashindano linavyofanya kazi na kuleta matokeo mazuri ya ushindi ! Wanamichezo wengi wa tanzania huwa hawana taswira au picha ya ushindi akilini mwao. Wengi huwa wana picha au taswira ya kushindwa , kukata tamaa , hofu hutawala vichwani { fear complex },huwaza mambo ya starehe zaidi ! matokeo ni kushindwa vibaya !
USHAURI WANGU KWA WANAMICHEZO WA TANZANIA. Licha ya kukaa kambini kwa muda mrefu , kufanya mazoezi mengi , kupata maelekezo ya kutosha toka kwa waalimu wa michezo ,kupata mahitaji yote yanayotakiwa kambini , hiyo haitoshi !
KWANINI ? Kama akili imekata tamaa, inawaza kushindwa , inajenga hofu badala ya kujenga hali ya kujiamini ,ushindi, haina taswira au picha ya ushindi ni kazi bure . Maana yake ni kwamba Unashughulika na mwili kuupatia mahitaji yake lakini unasahau kushughulika na akili yako, ambacho ndicho kitu cha muhimu zaidi ndugu yangu mpendwa.AKILI INA NGUVU YA KUTENGENEZA PICHA AMBAYO UNAITENGENEZA AKILINI MWAKO NA BAADAYE INAWEZA KUWA KWELI. Kuchora picha akilini , ni njia iliyofanyiwa utafiti na imewaletea watu mbalimbali mafanikio makubwa. Kwa mfano Mwanasayansi maarufu ARCHIMEDES alikuwa akitumia mbinu ya utungaji taswira au picha katika tafiti zake na kweli alifanikiwa sana.
Kama unapenda kuwa mchezaji fulani maarufu ulimwenguni, kwa mfano pele hebu chukua picha yake na uiweke ukutani au sehemu ambayo unadhani unaweza kuiona kila siku. Na tamka maneno ya ushindi kila siku, waweza kusema , " Nataka kuwa bingwa kaika mchezo wa mpira wa miguu kama pele au zaidi ya yeye ." Utaniambia ndugu yangu maneno haya hayapotei bure yana athari sana katika akili zetu" ANZA KUFANYA LEO , UTAONA AJABU KUBWA !
EWE MWANAMICHEZO FANYA HIVI : Kabla hujaingia katika uwanja wa mashindano , vuta taswira au picha kwa kuwaleta washindani wako akilini. Chora picha akilini mwako kuwa mko uwanjani unawanyanyasa washindani wako kwa kuutawala mpira.Ni hivi , Njia ya ushindi zitaibuka, kuna nguvu itataka iwe kweli, njia zitajitokeza, utaamsha nguvu iliyolalal. FANYA LEO UONE.
No comments:
Post a Comment