Sunday, July 26, 2015

FIMBO HAIFUNZI MKE



                                  USIMPIGE  MKE  WAKO
  
KATIKA    maisha   ya  kila   siku , mume   na  mke   waweza  kuwa    wanaishi   kwa  kuheshimiana   na   kuonyeshana  UPENDO  wa   kila  hali. Kuna  baadhi   ya  watu  wamekuwa   na   IMANI  kwamba  mwanamke  bila   kupigwa   bado  hajaoneshwa  UPENDO.Hata  hivyo   IMANI  hii  mara   nyingi   imekuwa  ikijitokeza  katika  baadhi   ya  makabila ilhali  watu  wengine   , hasa  wale   wanaokwenda  na  mabadiliko   ya   SAYANSI    na  TEKNOLOJIA , wakijitahidi    kuyaepuka  katika  familia  zao.
       Matatizo  huweza  kuzuka  pale  nyumba   inapofikiwa  na  mgeni   ambaye  ana  uhusiano  na   mume  au    mke. Kwa  wenye  nyumba   wastaarabu, hata  kama  tayari  wamekwishaanza  kuwa  na  tofauti , hujitahidi  kwa  kila  hali ,  kuzificha  mpaka  pale   mgeni  huyo   atakapoondoka  ili  kulinda  SIFA   na  HESHIMA   yao  nje  ya  nyumba.
      Hata   hivyo, wapo  wale   wanaoona  kwamba  huo  ndio  wakati  mwafaka  wa  kuonesha  ubabe  kwamba  wana  uwezo  wa  kuzimiliki    nyumba  zao  ikiwa  ni  pamoja  na   kuwafanya   jambo  lolote  wake  zao  bila  kujali , kwani  ni  mali   yao. Wakati   mwingine, huweza  kuanzisha  kisa  kidogo  sana  ambacho  humsababisha  mume  huyo  kumpiga  mkewe  huku   mtazamaji  akibakia  hana  la  kufanya ,  kwani  WAPENDANAO  WAGOMBANAPO  ukaingilia , siku   wakipatana  watakuona  mchonganishi  wao.
      Kuna  wanaume  wengine  wenye  tabia  ya  kuchukia  pindi  wanaporudi  nyumbani  na  kukuta  WAGENI. Tena  cha  ajabu   zaidi ,  ni  pale   wanapowarushia  mzigo  WAKE  zao  kwa  madai  kwamba  wao  ndio   wamewaalika.  Ikumbukwe  kwamba  WAGENI  nyumbani  ni   BARAKA   na  mnatakiwa  mjitahidi  kwa  kila  hali  kuwakirimu  kwa  kilichopo. Pindi  unapoonesha  kuwa  na  shaka  na  mgeni  ikiwa  atagundua  hali  hiyo , yawezekana  kabisa  AKAONDOKA  nyumbani  kwenu  akiwa  amebeba  mzigo  wenye  sifa  mbaya  juu  ya  maisha  yenu  ambao  huenda  na  kuutua  huko  aendako.
      Tabia  ya  kugombana  na  kutaka  KUJIKWEZA  ili  KUONEKANA  kuwa  UNA  NGUVU  katika  nyumba  imekuwa  ikijitokeza  mara  nyingi  pindi  wanaume  wanapoona  kuna  ujio  ndani  ya  nyumba  zao. Huamua  kufanya  hivyo, kwa  ajili  ya  kujionesha   wana  nguvu  na   hawatawaliwi  na  wake  zao ,  kwa  kuwagombeza  bila  misingi  hata  mbele   ya  watoto  wao , si  hivyo  tu bali  pia  huweza  hata  kuwapiga mbele  ya  wageni  wakiwa   na  malengo  ya   kutafuta   sifa.
    Si  kwamba    wanaume  wote  wana  tabia  hii , la  hasha !!  Bali  ni  muhimu  kwa  wale   wenye  tabia hizi ,  KUJIFAHAMU  AU  KUJITAMBUA  MWANAMKE  HAFUNZWI  WALA  KUREKEBISHWA  KWA   FIMBO !!  ONGEA  NA  MKE  WAKO  !!  ACHA  UBABE  WEWE  MWANAUME !!  JISHUSHE  WAKATI   WOTE KWA   MKEO.  FANYA  LEO   UONE  UTANIAMBIA   BABA !! ONYESHA  MAPENZI  YA  DHATI  KWA    MKEO    SIYO   NGUVU  ZA  MWILI. MWANAKE   ANAHITAJI   UPENDO TOKA   KWAKO  BABA  !!
  Si   kwamba   mke   ni  mnyama  au  mtoto  mdogo  kiasi  kwamba  akielezwa  tu  kwa  maneno   hukosa uwezo  wa  kuelewa   anachoambiwa  ni  nini  na  anapaswa  kutekeleza  vipi. Kibaya  zaidi  ni   pale  unapompiga  mkeo  mbele   ya   mtu  ambaye  ana  uhusiano  naye  wa  karibu   zaidi. Moja  kwa  moja  hata  kama  ulikuwa   na  nia   nzuri  ya  kumwonya   atachukulia  kuwa   unamnyanayasa  ndugu  yake  huku  anakuona. Yawezekana  akawa  hajapanga   kuondoka  na  kulazimisha  kuondoka  kwa  hasira  ya  yale  uliyomfanyia  ndugu yake.
   Anapofika  kwa   wazazi  ama  walezi   huweza   kukupakazia  ikiwa  ni  pamoja  na  kutia  chumvi   dhidi   ya  uhusiano  mlionao  na  wakati   mwingine   shutuma   huweza   kuwa  nyingi  zaidi  hata   kama   uliwafanyia  kitendo  kizuri   kiasi  gani   kwa  nia   ya  kuwapoza. La   ya  hivyo , huo  waweza  kuwa  mwanzo   wa     kuvurugika   kwa  ndoa  yenu. Mpaka  hapo   hakutakuwa   na   wa  kumlaumu   kwani  awali   MUME  kama  muhimili  wa  nyumba ,  alikuwa  na  NIA  ya  ajabu.
  Kwa  WANAUME  ambao  bado  wana  tabia  ya  kutumia  FIMBO  kama   njia   pekee  ya  KUWAELIMISHA  wake  zao , ni  vema   wakafahamu  kuwa  njia hiyo  SASA  IMEPITWA  NA   WAKATI.  Hali   kadhalika   kwa  kufanya  hivyo   mbele  ya  watoto ,  ina   maana   kwamba   UNAMDHALILISHA  MKEO  na  kumjengea  ukuta  wa  kutokuwa  na  maamuzi  na  watoto  hasa  katika  masuala   ya  KUWAKANYA.Kwani  daima   atakapowapiga   hawatasita   kumwambia    mbona   na  wewe     Baba  huwa   anakupiga !!”Hata  kama  mbele  za  watu.
               EWE  BABA  ACHA  KUMPIGA   MKEO ,   ONGEA  NAYE !! JIFUNZE   KUMSIKILIZA!


              ASANTE    MSOMAJI  WANGU  KWA  KUSOMA   MAKALA  HII , KARIBU   KWA  MAONI , USHAURI , CHANGAMOTO  !!  WEWE   WAONAJE  SUALA  HILI   LA  KUPIGA    WANAWAKE KATIKA  NDOA ?

  
  Makala  hii  imeandikwa   na  MWL.  JAPHET    MASATU , Mwelimishaji   na   mhamasihaji  katika  masuala  ya   Elimu  ya  maisha  na   Mafanikio ,  Mahusiano, biashara /  ujasiriamali, anapatikana  kwa namba    + 255  755 400  128 { WhatsApp}  /   +  255 716  924136   /  +  255 785  957077.  EMAIL :  japhetmasatu@yahoo.com

1 comment:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    ReplyDelete