BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Showing posts with label WATU MAARUFU DUNIANI. Show all posts
Showing posts with label WATU MAARUFU DUNIANI. Show all posts
Saturday, July 29, 2017
Friday, December 9, 2016
Sunday, June 12, 2016
MUHAMMAD ALI , BONDIA ALIYETIKISA DUNIA
Muhammad Ali (74),
bingwa wa zamani wa dunia wa ngumi za uzani wa juu na mmoja kati ya
wanamasumbwi bora zaidi duniani, aliyefariki katika Hospitali ya Phoenix Area,
Arizona, nchini Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita.
Bondia huyo
aliyetamba katika miaka ya 1960 mpaka 1980 alipoamua kujiuzuru, atakumbukwa
daima kwa mchango wake mkubwa katika mchezo huo. Mwanamichezo huyo wa masumbwi,
alijulikana zaidi kwa jina la “The Greatest” Alilazwa katika hospitali hiyo
akisumbuliwa na tatizo la upumuaji uliosababishwa na ugonjwa Parkison Disease.
Alizaliwa katika
kitongoji cha Cassius Marcellus Clay,Louisville, Kentucky, Januari 17, mwaka
1942. Alikuwa ni kijana wa mtoto wa mchoraji. Akiwa na umri wa miaka 12,
aliibiwa baiskeli na aliwaambia maafisa wa polisi atahakikisha kwamba anawapata
wezi wake.
Enzi za uhai
wake alikuwa amevunja rekodi ya kutwaa ubingwa wa dunia mara tatu wa ngumi za
Uzani wa Juu. Mwaka 1981 aliamua kustaafu mchezo wa ndondi. Baadaye alianza
kusumbuliwa na ugonjwa wa Parkinson hadi alipofikwa na mauti wiki iliyopita.
Pamoja na
kusumbuliwa na ugonjwa huo, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi na
maambukizi katika njia ya mkojo. Msemaji wa familia ya bondia huyo, Bob Gunnell
alisema kabla ya kufariki kwake alikuwa chini ya uangalizi wa Jopo la Madaktari
na kwamba alikuwa anatarajia kutembelea jiji la London lakini alijikuta
akisumbuliwa na maradhi hayo.
Kilichosababisha
kujiunga na mchezo huo
Muhammad Ali
hakuwa na nia ya kujiunga na mchezo wa ndondi, bali aliingia huko kwa bahati
tu. Akiwa na umri wa miaka 12 akiwa na rafiki zake ndipo baiskeli yake ikaibwa.
Baada ya kugundua
kwamba baiskeli yake imeibwa alishauriwa kwenye nyumba ya taasisi ya mafunzo ya
Columbia ambako alimkuta Ofisa wa Polisi aliyefahamika kwa jina la Joe Martin
aliyekuwa akisimamia mafunzo ya ndondi.
Alipomweleza Ofisa
huyo wa Polisi kuhusu tukio la kuibwa kwa baiskeli yake na mtu ambaye
hakufahamika alishauriwa kuanza kunoa ngumi zake kwa kujifunza mchezo huo wa
ngumi kabla ya kuanza kumsaka mwizi huyo.
Alifanya bidii
katika mafunzo hayo ya ndondi na alipofikisha umri wa miaka 18 alikuwa
ameshinda medali ya dhahabu, katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini
Rome, Italia.
Ali alikuwa
akiishi Louisville katika jimbo la Kentucky akijulikana kwa jina Mercellus
Cassius Clay Jr kabla ya kubadili dini mwaka 1975 na kuitwa Muhammad Ali akiwa
amefikisha umri wa miaka 33.
Rekodi yake
ulingoni
Alicheza jumla ya
mapambano 61, kati ya hayo alishinda 56, huku akishinda mapambano 37 kwa “knock
out” na alipigwa katika mapambano mitano tu.
Akiwa kijana mdogo
mwenye umri wa miaka 22 alivunja rekodi ya kutwaa ubingwa wa ngumi za uzani wa
juu, ambayo baadaye ilikuja kuvunjwa na Mike Tyson mwaka 1986 akiwa na umri wa
miaka 20.
Hata hivyo baada
ya kutwaa taji la dunia la uzito wa juu mwaka 1967, alikamatwa na kutupwa
jela kwa kosa la usaliti, kwa kukataa kujiunga na Jeshi la Marekani ili
kushiriki katika vita vya Vietnam. Ali alivunja rekodi ya kutwaa mataji matatu
ya uzito wa juu wa dunia mwaka 1964, 1974 na 1978.
Mazishi yake
Mazishi ya
Muhammad Ali yatkuwa ni ya wazi katika eneo la makaburi, matayarisho ya mazishi
pamoja na zoezi zima la vitafanyika siku ya Ijumaa, nyumbani kwake, Louisville.
Rais wa zamani wa
Marekani, Bill Clinton anatarajiwa kushiriki. Bingwa huyo wa ndondi za uzito wa
juu mara tatu wa mmoja wa wanamichezo wa aina yake katika karne ya 20.
Nukuu
zake
“Pepea kama
kipepeo, ng’ata kama nyuki. Mikono haiwezi kupiga kitu ambacho macho hayaoni,”
Maneno hayo yalikuwa yakirudiwa mara kwa mara kuelezea stairi yake ya kupigana
anapokuwa kwenye ringi.
“Nilipigana na
mamba, nikapambana na nyangumi, nilikumbatia moto, niliipeleka jela radi, mimi
ni mtu mbaya ….Wiki iliyopita niliua mwamba, nikajeruhi jiwe, nilisababisha
jiwe likalazwa hospitali. Mimi ni hatari, ninaweza kusababisha dawa zikaugua,” maneno hayo aliyasema huku akicheka alipokuwa anaingia
kwenye pambano lake la mwaka 1974, lililochezwa katika ardhi ya Afrika, nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kumshinda mpinzani wake George Foreman,
katika pambano lililoitwa ‘Rumble in the Jungle’
CHANZO HABARI : GAZETI LA JAMHURI ,08 JUNI , 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)