Wengi
wameingia kwenye mtego huo, kazi wanaifanya kweli, na wanafikia umri wa
kustaafu, wanastaafu, mafao wanayapata, lakini maisha hayawi mazuri
bali yanakuwa yamejaa msongo. Na wengi, hawavuki miaka mitano, wanafariki ndani ya miaka mitano baada ya kustaafu.
Hivyo kama hutaki kufa mapema, basi usikubali kustaafu. Kila
siku ya maisha yako ifanye kuwa siku ya kazi, na kadiri mwili
unavyokuwa kwenye kazi, unakuwa imara zaidi ya mwili uliopumzika.
Hivyo chagua kufanya kazi au biashara ambayo utaendelea kuifanya hata ukiwa na miaka 80, 90 na hata 100. Chagua kufanya kazi mpaka siku unayokufa, na utakuwa na maisha marefu, na yaliyo bora zaidi.
Kama
umeajiriwa na ukifika miaka 60 au 65 ni lazima ustaafu, hakikisha
unatengeneza mazingira ya kukuwezesha kuwa na kazi ya kuendelea kufanya
hata baada ya kustaafu kwenye ajira. Na hapo siyo ukatafute tena ajira za muda, badala yake uwe umeshajenga kitu chako ambacho utakifanyia kazi kwa miaka yako yote.