Wednesday, May 1, 2019

USISUBIRI KUSTAAFU, NDIO UFANYE UJASIRIAMALI USIJE UKAFA MAPEMA.

Wengi wameingia kwenye mtego huo, kazi wanaifanya kweli, na wanafikia umri wa kustaafu, wanastaafu, mafao wanayapata, lakini maisha hayawi mazuri bali yanakuwa yamejaa msongo. Na wengi, hawavuki miaka mitano, wanafariki ndani ya miaka mitano baada ya kustaafu.
 
Hivyo kama hutaki kufa mapema, basi usikubali kustaafu. Kila siku ya maisha yako ifanye kuwa siku ya kazi, na kadiri mwili unavyokuwa kwenye kazi, unakuwa imara zaidi ya mwili uliopumzika.
 
Hivyo chagua kufanya kazi au biashara ambayo utaendelea kuifanya hata ukiwa na miaka 80, 90 na hata 100. Chagua kufanya kazi mpaka siku unayokufa, na utakuwa na maisha marefu, na yaliyo bora zaidi.
 
Kama umeajiriwa na ukifika miaka 60 au 65 ni lazima ustaafu, hakikisha unatengeneza mazingira ya kukuwezesha kuwa na kazi ya kuendelea kufanya hata baada ya kustaafu kwenye ajira. Na hapo siyo ukatafute tena ajira za muda, badala yake uwe umeshajenga kitu chako ambacho utakifanyia kazi kwa miaka yako yote.

2 comments:

  1. Kama hutaki kufa mapema, basi usikubali kustaafu. Kila siku ya maisha yako ifanye kuwa siku ya kazi, na kadiri mwili unavyokuwa kwenye kazi, unakuwa imara zaidi ya mwili uliopumzika.

    ReplyDelete

  2. Huu ndiyo mtego ambao watu wamekuwa wanategwa na wanaingia kirahisi, fanya kazi kwa juhudi kubwa na utakapofika miaka 60 au 65 utaweza kustaafu, utalipwa mafao na kuwa na maisha mazuri ambayo hayana msongo.

    ReplyDelete