Sehemu kubwa ya matatizo ya biashara yanasababishwa na mfanyabiashara kufikiri yeye ni biashara yake, kitu ambacho siyo kabisa.
Biashara nyingi hazikui kwa sababu hakuna mpaka baina ya biashara na mmiliki wa biashara.
Mtu anaweza kutoa fedha kiholela kwenye biashara kwa sababu anaona
biashara ni yake. Kitu ambacho kinakuwa na athari kubwa sana kwenye
ukuaji wa biashara hiyo.
Ndugu ,
naomba nikusisitizie hili, na liandike mahali ambapo utaweza kulisoma
kila siku; WEWE SIYO BIASHARA YAKO, wewe na biashara yako ni vitu viwili
tofauti kabisa.
Wewe una maisha yako, ndoto zako na mahusiano yako, biashara ina maisha yake, ndoto zake na mahusiano yake. Kinachowaunganisha
wewe na biashara yako ni mtaji ambao umeuweka kwenye biashara hiyo,
mtaji huo umeikopesha biashara, na njia pekee ya kunufaika kupitia
biashara hiyo ni pale inaopata faida baada ya kufanyika kwa biashara.
Ukiweza
kuelewa hili, kwamba wewe siyo biashara yako, ukaiheshimu biashara yako
na kuiacha ikue bila ya kuiingilia, ukaiendesha kwa misingi ya ukuaji
wa biashara, utaiwezesha biashara hiyo kukua zaidi.
No comments:
Post a Comment