Pamoja
na madhara makubwa ya kiafya ya utumiaji wa sukari tutakayojifunza hapo
chini, sukari haina tofauti kubwa sana na madawa ya kulevya kama
kokeini au heroine.
Hii
ni kwa sababu matumizi ya sukari yamedhibitishwa kusisimua sehemu za
ubongo ambazo zinasisimuliwa na madawa hayo. Pale mtu anapotumia sukari,
ubongo unasisimka na kuzalisha homoni inayoitwa dopamine, hii ni homoni
ambayo huwa inaleta raha na kumsukuma mtu kurudia tena kile
alichofanya.
Hivyo
unapotumia sukari, ubongo unazalisha dopamine, ambayo inakufanya
ujisikie vizuri na upate utamu wa sukari. Lakini baada ya hapo
unasukumwa kutumia tena sukari ili upate utamu zaidi na kujisikia vizuri
zaidi.
Hii
ndiyo sababu watu wamekuwa wanapata msukumo mkubwa sana wa kutumia kitu
chenye sukari, na wakishatumia mara moja hawawezi kuacha, wanatumia
tena na tena na tena.
Matumizi
haya ya sukari yanaleta hali ya uteja au uraibu ambao ni mgumu sana
kuuvunja. Kila mtu anapoona kitu cha sukari akili yake haifikirii kitu
kingine chochote bali jinsi ya kupata sukari hiyo. Na anapoonja mara
moja, hawezi kujizuia bali atataka tena na tena.
Tafiti
zinaonesha pia ya kwamba matumizi ya sukari yamekuwa yanabadili tabia
za watu. Muda mfupi baada ya kutumia sukari watu wengi huwa wakorofi,
wenye hasira na wasio na subira. Sukari inawapa nguvu za ziada ambazo
zinawasukuma kuzitumia kwa njia ambazo siyo sahihi. Mtu anapokuwa na
sukari nyingi kwenye mwili huwa kwenye hali ya msongo kama mtu ambaye
ametumia kilevi.
Hivyo
kwa uwezo wa sukari kusisimua ubongo kama madawa mengine, kitendo cha
watu kuwa tegemezi kwenye sukari na kuadilika kwa tabia baada ya mtu
kutumia sukari, kunaifanya sukari kuwa kwenye kundi moja na madawa ya
kulevya.
No comments:
Post a Comment