Saturday, May 18, 2019

KILA MTU ANA HAIBA HIZI TATU : UJASIRIAMALI, UMENEJA , UFUNDI , ZIIBUE NA ZIFANYIE KAZI UTAFANIKIWA KATIKA BIASHARA YAKO

( 1 ). MJASIRIAMALI.

Hii ni haiba ambayo inabeba nafsi ya mjasiriamali. Mjasiriamali ni mtu wa kuja na mawazo mapya ya kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zinapatikana. Mjasiriamali ni mtu wa ndoto na maono makubwa, mtu wa kutengeneza picha za mambo yasiyoonekana. Mjasiriamali anaangalia mambo yalivyo na kujiuliza vipi kama yangekuwa tofauti.

Bila ya mjasiriamali hakuna mawazo mapya, hakuna ugunduzi na wala hakuna maono makubwa ya kibiashara.

Nafsi ya ujasiriamali ndiyo inawasukuma wengi kuingia kwenye biashara, lakini nafsi hii imekuwa haidumu kwa muda mrefu, inazidiwa nguvu na nafsi nyingine na ndiyo maana tunasema mtu anakuwa amepatwa na kifafa cha ujasiriamali. Wazo la ujasiriamali linamjia kwa muda mfupi na nafsi hii kuondoka kabisa.

( 2 ). MSIMAMIZI/MENEJA.

Hii ni haiba inayobeba nafsi ya usimamizi au umeneja kwenye biashara. Meneja ndiye mtu ambaye anaisimamia biashara kwa ukaribu, kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Huyu ni mtu ambaye anahakikisha rasilimali za biashara zinatumika vizuri. Pia meneja anahakikisha kilichofanywa kwenye biashara jana ndiyo kinafanywa leo. Mameneja hawapendi kujaribu vitu vipya kwa sababu hawana uhakika navyo.

Tofauti kubwa ya mjasiriamali na meneja ni mabadiliko, mjasiriamali anatafuta mabadiliko na kuwa tayari kuyafanyia kazi. Lakini meneja hataki kabisa mabadiliko, anataka kuendelea kufanya mambo kama ambavyo amekuwa

Meneja ndiyo nafsi inayoiwezesha biashara kufanya kazi. Mjasiriamali anakuwa na mawazo mapya na makubwa, lakini hawezi kuyafanyia kazi mawazo hayo kwa muda. Hivyo anahitaji kuwa na meneja ambaye anafanyia kazi mawazo hayo mapya.

( 3 ).FUNDI/MTAALAMU.

Hii haiba inayobeba nafsi ya ufundi au utaalamu unaohitajika kwenye biashara. Huu ni ule ujuzi au utaalamu ambao mtu anaingia nao kwenye biashara. Fundi kazi yake ni kutengeneza vitu na anapenda sana kutengeneza vitu. Haiba hii ya ufundi inapenda kufanya yale yanayopaswa kufanywa kwenye biashara.

Wakati mjasiriamali anakuja na mawazo mapya, meneja anaweka mfumo mzuri wa kufanyia kazi mawazo hayo, fundi ndiye anayefanya kazi kwenye biashara hiyo na kuzalisha matokeo yanayohitajika. Fundi ndiye anayezalisha matokeo kwenye biashara.

1 comment:

  1. Ili kufanikiwa kwenye biashara, lazima nafsi hizo tatu zifanye kazi kwa ushirikiano. Lazima uvae kofia hizo tatu kwa wakati mmoja.

    Nafsi ya ujasiriamali ikupe mawazo mapya, nafsi ya umeneja itengeneze mfumo wa kufanyia kazi mawazo hayo mapya na nafsi ya ufundi ichukue hatua za kufanyia kazi. Nafsi hizi tatu zinapokuwa na nguvu sawa wakati wote, utaweza kuanzisha biashara ambayo itakua na kudumu kwa muda mrefu.

    ReplyDelete