Watu wanaokuzunguka wana nguvu kubwa sana kwako, hata kama hujui. Watu
hao, hasa wale wa karibu, wana ushawishi mkubwa kwako. Kama
wanaokuzunguka wana mtazamo hasi wa kuona mambo hayawezekani, na wewe
pia utajikuta umebeba mtazamo huo, hata kama utakuwa unapingana nao
kiasi gani.
Na kama watu wanaokuzunguka wana mtazamo chanya wa inawezekana, na wewe pia utabeba mtazamo huo. Nguvu hii ya wanaokuzunguka ni nguvu kubwa sana unayopaswa kuwa nayo makini. Wengi wamekuwa wanapuuza nguvu hii, wakiamini wanaweza kuzungukwa na watu wa aina yoyote lakini wakafanikiwa.
Hicho kitu hakipo kabisa, kama haujazungukwa na watu sahihi, huwezi
kufanikiwa. Ni asili ya binadamu, hatuwezi kwenda juu zaidi ya wale
ambao wanatuzunguka.
Hivyo ili kupata kile unachotaka kwenye maisha, tafuta watu wanapiga hatua kwenye maisha yao na uwe nao karibu.
Watu ambao wanaamini kwenye ndoto kubwa na wasiokata tamaa. Watu hawa
watakupa nguvu ya kuendelea hata pale unapokutana na magumu na
changamoto.
No comments:
Post a Comment