Ili kupata unachotaka, unahitaji kupata mwongozo kutoka kwa mtu mwingine. Mtu huyo anaweza kuwa kocha, menta au mshauri ambaye anakusimamia ufike kule unakotaka kufika.
Iko hivi rafiki, sisi binadamu ni wavivu na hatupendi kujitesa. Tunaweza
kuweka mipango mikubwa na mizuri sana, lakini tunapokutana na ugumu ni
rahisi kuacha na kujiambia haiwezekani au hatuwezi.
Lakini
unapokuwa na mtu wa pembeni ambaye anakuangalia na kukusimamia, kwanza
hutataka kumwangusha, hivyo utajisukuma zaidi na pili yeye mwenyewe
hatakubaliana na wewe kirahisi, hivyo itakubidi ujaribu tena na tena na
tena kabla hujasema haiwezekani.
Watu wengi wamekuwa wanajiwekea malengo peke yao, na asilimia 99 wamekuwa hawayafikii. Ila wale wanaoweka malengo na kuwa na mtu wa kuwasimamia kwenye malengo yao, zaidi ya asilimia 90 wanayafikia.
Hii
ndiyo nguvu kubwa iliyopo kwa kuwa na mwongozo. Kwa sababu pia mtu
anayekuongoza anaweza kukushauri vizuri pale ambapo unakuwa umekwama. Ni rahisi kuona makosa ya mchezaji aliyepo uwanjani ukiwa nje ya uwanja, lakini yule aliyepo uwanjani anaweza asione kwa urahisi. Kuna
makosa unaweza kuwa unafanya kwenye maisha yako lakini huyaoni, ila
unapokuwa na mtu anayekusimamia, atakuonesha makosa hayo kwa urahisi na
utaweza kupiga hatua sana.
Unahitaji kuwa na mtu wa kukusimamia kwenye malengo na mipango uliyonayo ambaye atakusukuma kuyafikia.
No comments:
Post a Comment