MATAJIRI huwa wanachagua kulipwa kwa matokeo ambayo wanazalisha na hilo linawapelekea kulipwa zaidi kadiri wanavyozalisha zaidi.
MASKINI huwa wanachagua kulipwa kwa muda wanaofanya kazi, na hilo linawapa ukomo kwenye kulipwa kwao kwa sababu muda una ukomo.
Acha sasa kutaka kulipwa kwa muda na anza kuchagua kulipwa kwa matokeo
unayozalisha. Muda una ukomo, lakini matokeo hayana ukomo.
Ajira ni moja ya maeneo ambao unalipwa kwa muda, ndiyo maana unapaswa kuwa na biashara ya pembeni.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Showing posts with label KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Show all posts
Showing posts with label KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Show all posts
Thursday, December 19, 2019
Friday, September 13, 2019
MIPANGO YA MAISHA INAPASWA KUJA KABLA YA MIPANGO YA BIASHARA.
Ni
rahisi sana kuweka malengo na mipango mikubwa ya kibiashara, lakini
unapokaa na kujiuliza kwa nini unataka kufikia malengo hayo makubwa
unakosa jibu la uhakika.
Watu
wengi wamekuwa wanapotea kwenye biashara kwa sababu wanaweka malengo ya
biashara kabla hawajaweka malengo ya maisha. Wanataka kuwa mabilionea
kupitia biashara zao, na hilo linawataka kuweka maisha yao yote kwenye
biashara na kusahau vitu vingine vyote. Wanaweza kufikia lengo hilo,
lakini maeneo mengine ya maisha yao kama afya na mahusiano yanakuwa
yameathirika sana.
Kabla
hujaweka lengo kubwa la biashara, anza kwanza na lengo kuu la maisha
yako. Jua unataka kuwa na maisha ya aina gani, jua maisha ya mafanikio
kwa upande wako yana maana gani.
Ukishajua
kwamba unataka nini kwenye maisha yako, hapo sasa unaweza kuitumia
biashara yako kuwa na maisha unayoyataka wewe. Lakini ukianza kufikiria
unachotaka kwenye biashara pekee, utaishia kuwa na maisha mabovu sana.
Monday, September 2, 2019
UNAPOJIAJRI , UNAPASWA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALE WALIOAJIRIWA.
Unapojiajiri, unapaswa kufikiri tofauti
kabisa na wale walioajiriwa. Kwa sababu kuna vitu ambavyo watu
walioajiriwa hawajisumbui navyo sana, kwa sababu wameahidiwa vinafanyiwa
kazi, mfano bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengineyo. Unapoachana na
ajira na kuamua kujiajiri moja kwa moja, mambo hayo utapaswa
kuyahangaikia mwenyewe, lazima utafute bima yako na familia yako na pia
lazima uwekeze ili kujiandaa kwa siku zijazo. Kwa sababu hakuna
anayekuandalia mafao, unapaswa kutengeneza uwekezaji wako mwenyewe,
ambao miaka mingi ijayo utaweza kukuingizia wewe kipato hata kama
hufanyi kazi moja kwa moja.
Tuesday, August 13, 2019
ELIMU YA DARASANI INAPOKWAMA.
“In
the new world of sales, being able to ask the right questions is more
valuable than producing the right answers. Unfortunately, our schools
often have the opposite emphasis. They teach us how to answer, but not
how to ask.” ― Daniel H. Pink
Kwenye
ulimwengu mpya wa mauzo, kuuliza maswali sahihi ni bora kuliko kuwa na
majibu sahihi. Kwa sababu tayari mteja anajua mengi zaidi, jukumu lako
kama muuzaji ni kuuliza maswali yatakayokupa wewe fursa ya kumjua mteja
zaidi.
Lakini
kwa bahati mbaya sana, elimu ya darasani iko kinyume na hili. Miaka
yote ambayo tumekaa shuleni tumekuwa tunafundishwa jinsi ya kujibu
maswali ili kufaulu mtihani. Hivyo unakuwa vizuri sana kwenye kujibu
maswali, lakini unapofika mtaani unakuta tayari kila mtu ana majibu.
Hivyo elimu ya darasani inakwama hapo.
Ili
kupiga hatua kwenye kitu chochote unachofanya kwenye maisha yako,
jifunze jinsi ya kuuliza maswali sahihi, maswali ambayo yatakupa nafasi
ya kumjua mtu zaidi na mahitaji yake, ili uweze kumhudumia zaidi.
Kadiri
unavyoweza kuuliza maswali sahihi na kusikiliza kwa makini majibu
yanayotolewa, ndivyo unavyoweza kujifunza na kujua hatua sahihi za
kuchukua.
Wednesday, August 7, 2019
JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KUPITIA UANDISHI.
( 1 ). kuandika kuhusu kazi au biashara yako. Hapa unaandika nakala za mauzo,
zinazowavutia watu kwenye kazi au biashara unayofanya na kuwashawishi
kuja kununua kile unachotoa. Kadiri unavyoweza kandika vizuri, ndivyo
unavyoweza kuwavutia wengi na kuuza zaidi.
( 2 ). kuwaandikia wengine. Popote pale ulipo, kuna watu wana bidhaa au huduma
nzuri sana, zinazoweza kuwasaidia wengine kupiga hatua zaidi kwenye
maisha yao, lakini hawajaweza kuwafikia watu wengi. Hapo kuna fursa ya
wewe kuijua vizuri bidhaa au huduma hiyo, kisha kuandika nakala za mauzo
na kila anayenunua bidhaa au huduma kupitia nakala zako, basi mtu huyo
anakupa wewe kamisheni. Angalia ni bidhaa au huduma zipi unaweza
kuzifanyia hivyo, ingia makubaliano na wahusika na anza kuandika nakala
za mauzo.
( 3 ). kuwa mwandishi na kuuza kazi zako za uandishi. Unaweza kuwa mwandishi
kwenye eneo lolote unalochagua, na kwa kujifunza njia bora za uandishi
wenye ushawishi, ukaweza kuwavutia watu kusoma kazi zako na hata
kuzinunua pia. Hapa unaweza kuwa na vitabu, kozi au huduma nyingine kama
za ushauri ambapo utawavutia watu kuzipata kupitia uandishi wenye
ushawishi.
Rafiki,
hapo ulipo sasa, unaweza kutumia uandishi wa nakala za mauzo kama
sehemu ya kuingiza kipato cha pembeni. Jifunze na kuwa mwandishi bora,
andika sana na kuwa na mpango bora wa kutengeneza kipato kupitia
uandishi wako.
UJUZI ULIOZALISHA MAMILIONEA WENGI DUNIANI.
“There
is virtually no other skill that can make you as much money as
copywriting. Nearly all internet millionaires know this secret: more
than their product, more than their traffic generation techniques, more
than their email campaigns, more than who their joint-venture partners
might be, it’s their copywriting that has made them rich.” – Ray
Edwards.
Upo
ujuzi mmoja ambao umezalisha mamilionea wengi dunia kuliko ujuzi
mwingine wowote ule. Ujuzi huo ni uandishi wa nakala za mauzo
(copywriting). Kama umewahi kuona tangazo la bidhaa kwenye tv, redio au
gazeti na likaingia kwenye fikra zako kiasi cha kuwa unafikiria tangazo
hilo muda mwingi basi jua kuna watu walikaa chini na kuandika tangazo
hilo, ili kukulenga wewe.
Kama
umewahi kusoma maelezo ya kitu fulani na ukatoka ukiwa na hamasa na
kuchukua hatua mara moja, basi jua hapo kuna watu wamekaa chini kaundika
kitu kinachokulenga wewe, wakiwa wana hatua ambayo wanataka wewe
uchukue.
Uandishi
wa nakala za mauzo, ni moja ya ujuzi ambao unalipa zaidi duniani, hasa
pale mtu anapoweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu. Jifunze uandishi
wenye ushawishi kama tulivyojifunza kwenye kitabu cha juma hili na
utaweza kuongeza kipato chako maradufu.
Sunday, August 4, 2019
Monday, July 29, 2019
VITU VIWILI UNAVYOHITAJI ILI WATU WAKUSIKILIZE.
“There
is only one excuse for a speaker's asking the attention of his
audience: he must have either truth or entertainment for them.” ― Dale
Carnegie
Kama unataka watu wakusikilize unapoongea, unapaswa kuwa na moja au vyote kati ya vitu hivi viwili; ukweli au burudani.
Watu
wanapenda kusikiliza ukweli, ukweli ambao unawawezesha kufanya maamuzi
sahihi na kupiga hatua kwenye maisha yao, ukweli unaowafanya waone wapi
walikuwa wanakosea na hatua sahihi za kuchukua ni zipi. Unapokuwa na
ukweli, watu wanakusikiliza, hasa pale unapokuwa na ushahidi wa ukweli
huo. Japokuwa wakati mwingine ukweli huwa unaumiza na watu wengi
kuukataa, lakini unapousimamia unapata watu wa kukusikiliza. Hii ndiyo
inayosababisha tunawasikiliza waalimu, washauri, au viongozi mbalimbali,
ambao tunajua wana ukweli ambao tunauhitaji.
Watu
wanapenda burudani, watu wanapenda kusahau changamoto zao za maisha kwa
muda na kucheka kidogo. Na hapa ndipo wasanii na wachekeshaji
wanapopata nafasi ya kuwafikia wengine kupitia sanaa zao. Watu
watamsikiliza mtu kama wanaburudika kwa kumsikiliza.
Hivyo
rafiki, kama unataka kuwa mnenaji mzuri, kazana kuweka vitu hivi viwili
kwenye unenaji wako, ukweli na burudani. Kila unapopata nafasi ya
kuongea mbele ya wengine, jua ni ukweli gani ambao unataka watu hao
wajue, labda kuhusu wewe, kuhusu mada unayozungumzia au kuhusu bidhaa au
huduma unayotaka kuwauzia. Ukweli huu uwafanye waondoke na kitu ambacho
hawakuwa wanakijua awali na wawe na hatua za kuchukua ambazo hawakuwa
wanachukua awali. Pia waburudishe watu kupitia unenaji wako, kuwa na
hadithi, mifano au visa ambavyo vinaufukisha ukweli huo kwa njia ambayo
inawaburudisha watu. Unahitaji kuwa na maandalizi ya mifano au hadithi
utakazotumia kwenye unenaji wako, ambavyo vitafikisha ukweli na
kuwaburudisha watu pia.
Zingatia vitu hivyo viwili katika unenaji, ukweli na burudani na watu watapenda kukusikiliza kila wakati bila ya kuchoka.
Tuesday, July 23, 2019
TUMIA MTANDAO WA INTANETI VIZURI.
Mtandao
wa intaneti una nguvu kubwa ya kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi.
Watu wengi wamekuwa wanachukulia mtandao wa intaneti kama sehemu ya
kutoa maarifa na taarifa pekee, lakini pia unaweza kutumika kupata
wateja zaidi wa biashara yako.
Katika kutumia mtandao wa intaneti kupata wateja zaidi unapaswa kuwa na vitu viwili;
Moja
unapaswa kuwa na tovuti ya biashara yako, hii inaeleza kila kitu kuhusu
biashara yako. Hapa ndipo nyumbani kwa biashara yako mtandaoni. Watu
wanaweza kuingia na kupata taarifa muda wowote ule, masaa 24 kila siku.
Unaweza pia kuuza bidhaa zako moja kwa moja kwenye tovuti ya biashara
yako.
Mbili
unapaswa kuwa na blogu ya biashara yako. Blogu hii unaitumia kutoa
taarifa na maarifa yanayohusiana na biashara yako. Unaweza kuitumia
blogu kutoa elimu kwa wateja wako kuhusu biashara yako, hivyo watu
wanapokuwa na shida na kutafuta suluhisho, wanaletwa kwenye blogu ya
biashara yako. Kwa kupata ushauri wako mzuri, wanakuamini na kuwa tayari
kununua kile unachouza.
Tumia vitu hivyo viwili ili biashara yako iweze kunufaika na mtandao wa intaneti.
TUMIA SIMU KUUZA.
Simu
yako ni nguvu kubwa sana ya kukuwezesha kuwafikia wateja wengi na
kuwauzia pia. Itumie simu yako kama kifaa cha masoko na mauzo kwa
kuwasiliana na wateja wako kabla na baada ya kununua.
Kila
mteja anayefika kwenye biashara yako au anayejibu kutokana na matangazo
yanayotolewa na biashara, taarifa zake zinapaswa kuhifadhiwa. Hifadhi
namba zao za simu na tengeneza mpango wa kuwa unawapigia simu wateja
wako.
Kwa
wale ambao hawajanunua wapigie kuwaeleza manufaa ya kile unachouza na
kuwashawishi kuja kununua. Kwa ambao wameshanunua wapigie kujua
wanaendeleaje na kile walichonunua kimewafaaje.
Kwa kutumia simu yako vizuri utaweza kuwafikia wateja wengi na kuuza zaidi.
Njia
bora ya kuandaa mpango huu wa simu ni kurusha matangazo ambayo
yanawataka wateja wako kupiga simu, kutuma ujumbe au kuja kwenye
biashara yako. Na mteja akishakutafuta, basi tunza mawasiliano yake,
hasa simu na hapo utaendelea kuyatumia kwa masoko na mauzo zaidi.
PIMA KILA KITU.
Kila
hatua unayochukua kwenye biashara yako, unapaswa kuipima, la sivyo
hutaweza kujua kama inaleta matokeo sahihi au la. Usiendeshe biashara
yako kwa kubahatisha, badala yake iendeshe kwa kupima kila unachofanya
na kisha kufanya maamuzi sahihi kutokana na matokeo unayoyapata baada ya
kupima.
Kwenye
biashara, mara nyingi unachotaka wewe siyo ambacho soko linataka,
unachopenda wewe siyo ambacho soko linapenda. Hivyo acha kujifikiria
wewe na angalia soko linapenda nini kisha lipe.
Kama
unaendesha matangazo, pima matangazo hayo kwa kutumia njia mbalimbali
kama kutumia vichwa vya habari tofauti, kutumia vyombo vya habari
tofauti, kutoa ofa tofauti, kutumia bei tofauti na hata kutoa ofa
tofauti. Kisha pima matokeo unayopata kwa kila njia unayotumia na ile
inayoleta matokeo mazuri ndiyo inakuwa njia kuu.
Kila
unachofanya kwenye biashara yako, unapaswa kukipima na kujua matokeo
yake. Na hata baada ya kupata matokeo bora kabisa na kuchagua njia kuu,
bado unapaswa kuendelea kupima kadiri unavyokwenda ili uweze kujua
matokeo unayopata na kama kuna njia bora zaidi basi itumike hiyo.
Unapokuwa
unapima, unapaswa kuanza kwa hatua ndogo na ukishapata matokeo basi
unakwenda kwenye hatua kubwa. Kwa mfano kama unajaribu tangazo, anza kwa
kuwafikia watu wachache kisha ukishaona njia bora ndiyo unapeleka
tangazo hilo kwa watu wengi zaidi.
PATA HASARA MWANZONI KUPATA FAIDA MBELENI.
Kikwazo
kikubwa cha ukuaji wa biashara imekuwa kushindwa kumshawishi mteja
kununua kwa mara ya kwanza. Hivyo hapa ndipo unapaswa kuweka nguvu zako
kubwa.
Kwa
sababu tayari una mkakati bora wa kutoa thamani kubwa kwa wateja wako,
hawataweza kuona hilo mpaka pale watakaponunua kwako kwa mara ya kwanza.
Swali ni je utawezaje kumshawishi mteja kununua kwako kwa mara ya kwanza, mteja ambaye hajawahi kununua kabisa kwako?
Jibu
ni kwa kuondoa vizingiti au vikwazo vyote ambavyo vinamzuia mteja kwa
sasa. Kikwazo kikubwa kabisa kimekuwa ni hatari ambayo mteja anaona iko
mbele yake, ya kupoteza fedha zake iwapo anachonunua hakitamfaa.
Hatua
za kuchukua ni kuwa na mkakati wa kupata hasara mara ya kwanza mteja
anaponunua kwako, lakini kwa kuwa utamhudumia vizuri na atarudi tena na
tena, basi utaweza kutengeneza faida siku za mbeleni.
Hapa
unaweza kutoa zawadi kwa mteja anaponunua kwa mara ya kwanza au kuwa na
punguzo fulani. Vyote ni kumfanya achukue hatua ya kununua kwako kama
kukujaribu, na akishanunua kwako mara moja, ataendelea kununua.
Zawadi
au punguzo unalompa mwanzo linaondoa kabisa ile faida ambayo ungeweza
kuipata, lakini anapokuja kununua tena, unatengeneza faida.
Chukua
mfano unauza kitu ambacho bei yake ni elfu 10 na faida unayopata ni
elfu 3. Mteja ananunua kitu hicho kila mwezi mara moja na unaweza kwenda
naye kwa angalau miaka mitatu. Sasa unaweza kumpa mteja wako zawadi au
punguzo la hiyo elfu tatu na hata zaidi anaponunua kwa mara ya kwanza.
Lakini atakapoendelea kununua, utarudisha faida hiyo na zaidi.
Kabla
ya kuchukua hatua hii unapaswa kukokotoa kiasi cha faida unachopata na
muda ambao mteja atanunua ili uweze kupata matokeo mazuri.
ONDOA KABISA HATARI KWA MTEJA.
Tumeona
kikwazo cha wateja kununua kwa mara ya kwanza kwako ni hatari ya
kupoteza fedha zao iwapo kitu walichonunua hakitawafaa kama walivyotaka.
Tumejifunza njia moja ya kuwapa ofa au zawadi ambayo itawasukuma
kununua.
Ipo
njia nyingine yenye nguvu zaidi, ambayo ukiitumia lazima mteja anunue.
Njia hiyo ni kuondoa kabisa hatari kwa mteja. Yaani hapa unaondoa nafasi
yoyote ile ya mteja kupoteza fedha zake, na unakwenda mbele zaidi kwa
kumlipa kwa muda au chochote alichopoteza.
Jay
anaiita mbinu hii BETTER-THAN-RISK-FREE GUARANTEE (BTRF). Biashara
nyingi huwa zinamrudishia mtu fedha aliyonunulia kitu kama hakijamfaa,
au kumpa kitu kingine. Sasa wewe unahitaji kwenda zaidi ya hapo,
unahitaji kumrejeshea mteja kile alicholipa, lakini pia kumlipa fidia
kwa muda aliopoteza au usumbufu uliomsababishia.
Kwa
kuwa tayari kumlipa fidia mteja wako pale ambapo hajaridhishwa na
ulichomuuzia inaonesha unamjali sana na pia una uhakika sana na kile
unachouza. Kadiri mteja anavyopata uhakika wa aina hii, ndivyo
anavyokuwa tayari zaidi kununua kile unachouza.
Kama
kweli unajali kuhusu wateja wako na kama kweli unaamini kwenye kile
unachouza na umechagua kuwazia wateja sahihi, unaweza kutumia mbinu hii
na hutapata hasara yoyote. Kwa sababu kwanza utawahudumia wateja sahihi
na watakuwa tayari kwenda na wewe kwa muda mrefu.
KUWA NA KITU CHA KUKUTOFAUTISHA NA WENGINE.
Ili
kufanikiwa kwenye biashara au chochote unachofanya, unapaswa
kujitofautisha na wale wanaofanya kile unachofanya. Hivyo hapa unahitaji
kutengeneza utofauti wako na kuwaeleza wateja nini wakija kwako
wanapata ambacho hawawezi kupata sehemu nyingine yoyote ile.
Angalia
jinsi washindani wako wanafanya mambo yao, kisha wewe kuwa na njia bora
zaidi ya kufanya ambayo inawapa wateja thamani kubwa, kisha hakikisha
wateja wanajua kuhusu utofauti wako. Njia zote za masoko unazotumia
zinapaswa kueleza utofauti wako na wengine, ili wateja washawishike kuja
kwako na siyo kwenda kwa wengine.
Baadhi ya maeneo ambayo unaweza kujitofautisha kwenye biashara ni bei, huduma, ubora, upekee, uharaka, uhakika na mengine.
Njia
bora ya kujitofautisha ni kuchagua eneo dogo (niche) ambalo
utalihudumia vizuri zaidi kuliko kuhangaika na eneo kubwa. Hapa
unachagua aina fulani ya wateja, wenye sifa za kipekee ambao utaweza
kuwahudumia vizuri na kuachana na wateja wengine wote. Kuachana na
wateja wengine huwa ni kitu kigumu kwa wafanyabiashara wengi, lakini
unapaswa kukumbuka kwamba huwezi kuwaridhisha watu wote.
Tengeneza
ujumbe unaobeba utofauti wako kibiashara na kila unapokutana au
kuwasiliana na wateja hakikisha unawapa ujumbe huo. Ujumbe huu unapaswa
kurudiwa rudiwa mara nyingi mpaka watu wauelewe na kuihusisha biashara
yako na ule utofauti unaotengeneza. Yaani pale mteja anapotaka kitu cha
tofauti na kinachomfaa yeye, basi anajua atakipata kwako
JUA UNAKOKWENDA.
Kama
hujui unakokwenda, huwezi kufika na hata ukifika hutajua kama umefika.
Hatua ya kwanza kuchukua ili kupata unachotaka ni kujua wapi
unapokwenda.
Unapaswa
kujua kwamba kila mtu kwenye maisha kuna kitu anauza, iwe upo kwenye
biashara au ajira, hivyo jua ni nini unachouza na uweze kukiuza vizuri
zaidi.
Zipo
njia tatu za kukuwezesha kuuza zaidi, kupata wateja wapya, kuuza zaidi
kwa wateja ulionao na kuwafanya wateja ulionao waje kununua mara nyingi
zaidi.
Kama
umeajiriwa, unauza muda wako, utaalamu wako na uzoefu wako kwa mwajiri
wako. Na kitu kimoja ambacho kila mwajiri anapenda sana ni mtu ambaye
anaweza kutatua matatizo na siyo anayesababisha matatizo.
Chochote
unachochagua kufanya, hakikisha unakifanya kwa utofauti mkubwa na
wengine wanavyokifanya. Usikubali kufanya kwa mazoea au kuiga kile
ambacho wengine wanafanya.
Wape
wateja wako urahisi wa kusema ndiyo kwa kile unachouza, kwa kutoa
thamani kubwa sana ambayo hawawezi kuipata sehemu nyingine yoyote ile.
Yaani unapaswa kutoa thamani kubwa kiasi kwamba mteja atajiona ni mjinga
kujaribu kutafuta sehemu nyingine ya kununua.
TATIZO HUJUI UNACHOTAKA.
Pata
picha, unataka kuwa na safari, unaondoka nyumbani umebeba mizigo yako
na kuelekea kituo cha mabasi. Unakaribishwa na kuulizwa unaenda wapi,
unasema popote basi linapokwenda. Je unafikiri basi hilo litakupeleka
wapi?
Unaweza
kushangaa na kujiuliza inawezekanaje mtu mwenye akili timamu aende
kituo cha basi kwa ajili ya safari halafu hajui anakokwenda!
Kabla
hujaendelea kushangaa, hebu jiulize kwanza maswali haya muhimu;
unakwenda wapi na maisha yako? unakwenda wapi na biashara unayofanya?
Unakwenda wapi na kazi uliyonayo? Unakwenda wapi na mahusiano uliyonayo?
Kwa
maneno mengine, miaka 5, 10, 20 na zaidi ijayo unajiona wapi? Kama
huwezi kutoa jibu moja kwamba unajiona wapi katika vipindi hivyo, kwa
hakika huna tofauti na anayeenda kwenye kituo cha mabasi huku akiwa
hajui anakwenda wapi.
Na
hivi ndivyo watu wengi wanavyoendesha maisha yao, wanakazana sana
kufanya chochote wanachofanya, lakini hawajui wanakwenda wapi, hivyo
wanafanya leo kama walivyofanya jana, huku kesho ikiwa haipo kwenye
mawazo yao kabisa.
Kama
mpaka sasa maisha yako huyaelewi, kama umeshajaribu kazi na biashara
nyingi lakini bado huoni matokeo mazuri, tatizo lako ni moja, hujui nini
hasa unachotaka, hujui wapi hata unakotaka kufika.
Na
kama hutachukua hatua ya kwanza muhimu ya kujua kwanza nini unachotaka
na wapi unapotaka kufika, hutaweza kuwa na maisha bora. Kila siku
utaishia kuyumbishwa kama bendera inayopeperushwa na upepo. Watu
watakuja kwako na kila aina ya fursa mpya na utahangaika nazo, na hakuna
hata moja itakayokusaidia kufanikiwa.
Jua
kwanza ni nini hasa unachotaka, jua ni wapi unakotaka kufika, kisha
weka juhudi zako zote katika kufika kule unakotaka kufika. Kuwa kiziwi
na kipofu kwa vitu vingine vyote visivyohusiana na kile unachotaka.
Usiwe mtu wa kukimbizana na kila aina ya fursa mpya, badala yake weka
nguvu kubwa kufika kule unakotaka kufika.
Kujua unachotaka na kuweza kukipata, anza kwa kujiuliza maswali haya muhimu sana;
- Mimi ni nani?
- Ni nini ninachotaka?
- Ni nini kinanipa furaha?
- Nini hakinipi furaha?
- Uimara wangu uko wapi?
- Udhaifu wangu uko wapi?
- Ni mchango gani mkubwa naweza kutoa kwa wengine kupitia maisha yangu, kazi yangu, biashara yangu na mahusiano yangu?
Ukijiuliza
na kujipa majibu sahihi kwenye maswali hayo saba, na kufanyia kazi
majibu hayo, utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Monday, July 15, 2019
JINSI YA KUPATA WAZO LA TOFAUTI NA WENGINE NA KUFANIKIWA
Katika kupata wazo bora, zingatia mambo yafuatayo;
Moja; anza na chochote unachojali sana.
Watu
wengi wamekuwa wanafikiria kwamba ili uweze kuleta mabadiliko makubwa
kwako na kwa wengine basi inabidi uwe na wazo kubwa na la kipekee sana.
Wazo ambalo wengine hawajawahi kuwa nalo. Huo siyo ukweli, unaweza
kuanza na wazo lolote na ukaweza kulijenga kwa utofauti na
ukajitofautisha sana.
Anza
na chochote unachojali, unachopenda, unachoamini, unachojua, ulichozoea
au ambacho umesomea. Chochote kile ambacho unaona kinaweza kuwa bora
zaidi ya kilivyo sasa, unaweza kukichukua kama wazo lako la kufanyia
kazi.
Mbili; uliza maswali ambayo hayaulizwi.
Watu
wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea kwa sababu wanafanya kile ambacho
kila mtu anafanya, na hawathubutu kujaribu vitu vya tofauti. Sasa kwa
wazo unalotaka kufanyia kazi kuliboresha zaidi, anza kwa kuuliza maswali
ambayo watu wengine hawaulizi.
Maswali
hayo yanaweza kuwa, vipi kama.... vipi kinyume cha... Hapa unajaribu
kupata picha ya tofauti na wengi walivyozoea, kwa kuona upande wa pili
wa vitu au kwa namna ya tofauti.
Tatu; angalia uzoefu wako binafsi.
Baada
ya kujiuliza maswali ya tofauti kwenye wazo unalotaka kufanyia kazi,
angalia uzoefu wako binafsi kwenye wazo hilo. Usijidharau kwa sababu
labda huna elimu kubwa au uzoefu mkubwa kwenye jambo hilo. Labda siku za
nyuma umewahi kujaribu kufanya tofauti na ukapata matokeo ya tofauti,
hiyo inatosha kukuonesha kwamba kuna uwezekano wa kupata matokeo tofauti
na ambayo watu wanapata sasa.
Nne; chagua eneo la ubobezi kwenye wazo lako.
Wazo
unalokuwa nalo linaweza kuwa pana, sasa unahitaji kuchagua eneo ambalo
utabobea kwenye wazo hilo ili kujitofautisha kabisa na wengine. Badala
ya kutaka kufanya kila kitu, unachagua eneo moja ambalo utaweka muda na
nguvu zako na kuweza kutengeneza ubobezi mkubwa. Ni kupitia ubobezi huu
ndiyo unaweza kupiga hatua kubwa kwenye wazo hilo.
Tano; fanya utafiti.
Watu
wengi wamekuwa wanapata mawazo mapya ya kuboresha zaidi, lakini
hawanufaiki nayo kwa sababu huwa hawaweki kazi inayopaswa kuwekwa ili
mtu kubobea kwenye kitu hicho. Moja ya kazi kubwa unayopaswa kuweka ni
kufanya utafiti. Siyo kusoma tafiti, badala yake kufanya utafiti mpya,
kwa kuangalia yale maeneo ambayo unataka yawe bora kisha kuja na njia
bora za kuyaboresha kutoka kwenye tafiti mbalimbali zinazogusa wazo
hilo.
Sita; unganisha mawazo.
Kuna
maeneo mengine ambayo yameweza kupiga hatua kubwa, ambayo ni tofauti na
wazo unalofanyia kazi wewe. hii haikuzuii wewe kujifunza kutoka maeneo
hayo. Jifunze kupitia maeneo mbalimbali kwa hatua ambazo watu wameweza
kupiga, kisha unganisha mawazo hayo na wazo unalofanyia kazi kuweza
kuona jinsi gani ya kuboresha wazo unalofanyia kazi. Kumbuka misingi ya
mafanikio kwenye kila eneo inafanana, hivyo kwa kuangalia jinsi ambavyo
mawazo mengine yamefanikiwa, utaweza kufanikisha wazo lako pia.
Saba; tengeneza nguzo ya kubeba wazo lako jipya.
Baada
ya kuchagua wazo unalotaka kuboresha, ukauliza maswali ya tofauti,
ukatumia uzoefu wako, ukafanya utafiti na hata kujifunza kutoka maeneo
mengine, unakuwa umejifunza mambo mengi sana kuhusiana na wazo lako
jipya. Hapa unakuwa na maarifa na taarifa nyingi ambazo mtu mwingine
siyo rahisi kuyaelewa. Hivyo ili wazo lako la kuboresha liweze kueleweka
na kutumiwa na wengine, unahitaji kutengeneza nguzo ya kubeba wazo
lako. Hapa unatengeneza mfumo unaobeba wazo lako jipya, kwa namna ambayo
watu wengine wanaelewa jinsi linavyofanya kazi na matokeo ya tofauti
yanavyopatikana.
Kwa
hatua hizo saba, unakuwa umekamilisha wazo lako la tofauti, ambalo
linaleta matokeo bora kuliko yale ambayo yamezoeleka. Baada ya hapo sasa
unakwenda kwenye hatua ya pili ambayo ni kujenga wafuasi kwenye wazo
lako.
Friday, July 5, 2019
TOKA KWENYE UMASKINI NA UTEGEMEZI KWA KUCHUKUA HATUA HIZI KUELEKEA UTAJIRI
HATUA YA KWANZA; TAMBUA ASILIMIA 95 HAWATAFANIKIWA.
Hatua ya kwanza ya kutoka kwenye umasikini na kuelekea kwenye utajiri ni kutambua kwamba asilimia95 ya watu hawatafanikiwa. Kwa maneno mengine ni kwamba utajiri siyo kwa kila mtu. Hata watu wote wangepewa fedha sawa au fursa sawa, bado mgawanyo utabaki vile vile, asilimia 5 watafanikiwa sana na asilimia 95 watakuwa na maisha magumu.
Na hili liko wazi ukiangalia kwenye jamii zetu. Mambo kama haya yapo wazi kabisa;
Ukianzia kwenye upande wa afya ya mwili, watu wengi wanakabiliwa na magonjwa sugu kama presha na kisukari, wengi hawapo kwenye afya nzuri inayowawezesha kujituma zaidi kwenye kazi zao.
Ukienda upande wa afya ya akili na roho, wengi wana msongo wa mawazo na sonona, hawawezi kuyakabili maisha yao bila ya kutumia dawa au vilevi vya kuwasahaulisha matatizo yao kwa muda.
Upande wa mahusiano nao una changamoto kubwa kwa wengi, ndoa nyingi zinavunjika na familia kusambaratika.
Kwenye fedha ndiyo mambo ni magumu zaidi. Wengi wapo kwenye madeni, kipato hakitoshelezi matumizi na hivyo wanaendelea kukopa, kitu ambacho kinawaumiza zaidi na kuwaweka kwenye umasikini mkubwa.
Ni muhimu sana utambue hali halisi na jinsi ambavyo wengi wanakwamba kwenye hali hiyo, ili wewe ukatae hali hiyo na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
HATUA YA PILI; TAMBUA CHANZO CHA WENGI KUBAKI KWENYE UMASIKINI.
Baada ya kukubali kwamba wengi hawatafanikiwa, hata kama kila kitu kitatolewa sawa kwa wote, hatua ya pili ni kutambua chanzo cha wengi kubaki kwenye umasikini.
Siyo bahati nzuri kwamba asilimia 5 pekee ndiyo wanaofanikiwa sana na siyo bahati mbaya kwamba asilimia 95 wanabaki kwenye umasikini mkubwa.
Kila kinachotokea kwenye maisha ya mtu kinasababishwa, na ili kubadili matokeo, unapaswa kubadili kwanza kisababishi.
Ili kuondoka kwenye kundi kubwa la wasiofanikiwa na kwenda kwenye kundi dogo la wanaofanikiwa, jua sababu hizi zinazowaweka watu kwenye umasikini na ondokana nazo mara moja.
Rafiki, epuka sababu hizi saba ambazo zimewaweka wengi kwenye umasikini mkubwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini huo kama utaendelea kukumbatia sababu hizo.
HATUA YA TATU; CHORA MSTARI.
Baada ya kuzijua sababu ambazo zimekuweka kwenye umasikini kwa muda mrefu, sasa kuna hatua ya tatu ya kuchukua, ambayo ni kuchora mstari.
Kuchora mstari maana yake ni kufanya maamuzi kwamba kuanzia sasa mambo yako yote yanabadilika. Unaachana na mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Maamuzi hayo unayafanya sasa na hatua unaanza kuzichukua sasa. Siyo baadaye, siyo kesho, siyo wiki ijayo, siyo mwezi ujao na wala siyo mwaka ujao. Ni leo, ni sasa. Kama hutachora mstari sasa hivi na kuanza kuishi maisha mapya, utaendelea kujichelewesha kufanikiwa.
Kataa kuwa wa kawaida, kataa kubaki kwenye umasikini na maisha magumu na chagua kufanikiwa na kufikia utajiri. Chagua kuziishi tabia ambazo zitayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usikubali kuendesha maisha yako kwa ukawaida, halafu unapofika ukingoni mwa maisha unagundua hukuishi maisha yako. Chagua leo kuyaishi maisha yako, chagua kuwa bora zaidi ya pale ulipo sasa. Yote yanawezekana na yapo ndani ya uwezo wako.
Hatua ya kwanza ya kutoka kwenye umasikini na kuelekea kwenye utajiri ni kutambua kwamba asilimia95 ya watu hawatafanikiwa. Kwa maneno mengine ni kwamba utajiri siyo kwa kila mtu. Hata watu wote wangepewa fedha sawa au fursa sawa, bado mgawanyo utabaki vile vile, asilimia 5 watafanikiwa sana na asilimia 95 watakuwa na maisha magumu.
Na hili liko wazi ukiangalia kwenye jamii zetu. Mambo kama haya yapo wazi kabisa;
Ukianzia kwenye upande wa afya ya mwili, watu wengi wanakabiliwa na magonjwa sugu kama presha na kisukari, wengi hawapo kwenye afya nzuri inayowawezesha kujituma zaidi kwenye kazi zao.
Ukienda upande wa afya ya akili na roho, wengi wana msongo wa mawazo na sonona, hawawezi kuyakabili maisha yao bila ya kutumia dawa au vilevi vya kuwasahaulisha matatizo yao kwa muda.
Upande wa mahusiano nao una changamoto kubwa kwa wengi, ndoa nyingi zinavunjika na familia kusambaratika.
Kwenye fedha ndiyo mambo ni magumu zaidi. Wengi wapo kwenye madeni, kipato hakitoshelezi matumizi na hivyo wanaendelea kukopa, kitu ambacho kinawaumiza zaidi na kuwaweka kwenye umasikini mkubwa.
Ni muhimu sana utambue hali halisi na jinsi ambavyo wengi wanakwamba kwenye hali hiyo, ili wewe ukatae hali hiyo na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
HATUA YA PILI; TAMBUA CHANZO CHA WENGI KUBAKI KWENYE UMASIKINI.
Baada ya kukubali kwamba wengi hawatafanikiwa, hata kama kila kitu kitatolewa sawa kwa wote, hatua ya pili ni kutambua chanzo cha wengi kubaki kwenye umasikini.
Siyo bahati nzuri kwamba asilimia 5 pekee ndiyo wanaofanikiwa sana na siyo bahati mbaya kwamba asilimia 95 wanabaki kwenye umasikini mkubwa.
Kila kinachotokea kwenye maisha ya mtu kinasababishwa, na ili kubadili matokeo, unapaswa kubadili kwanza kisababishi.
Ili kuondoka kwenye kundi kubwa la wasiofanikiwa na kwenda kwenye kundi dogo la wanaofanikiwa, jua sababu hizi zinazowaweka watu kwenye umasikini na ondokana nazo mara moja.
- Kuangalia nyuma badala ya mbele. Wale wanaoshindwa wanatumia muda wao mwingi kuangalia mambo ya nyuma kuliko pale walipo sasa na kule anakokwenda. Wamekuwa wanatumia matukio ya nyuma kama sababu ya wao kushindwa kupiga hatua zaidi. Wataeleza jinsi ambavyo walidhulumiwa, kuteswa au kunyanyaswa huko nyuma. Wataeleza jinsi ambavyo wamejaribu mambo mengi lakini wameshindwa. Kwa kuangalia zaidi nyuma kuliko mbele kunawafanya kuangalia kushindwa zaidi kuliko kufanikiwa.
- Kukosa kusudi la maisha. Watu wengi wanaendesha maisha yao bila ya kusudi, hawajui nini wanachotaka kwenye maisha yao na wala hawajisukumi kufanya chochote kikubwa. Kwa kukosa kusudi wanajikuta wanakimbizana na kila kitu, mwisho wa siku wanachoka na hakuna hatua wanayokuwa wamepiga.
- Kutenga madhara ya matukio. Watu wengi wanabaki kwenye umasikini kwa sababu hawana nidhamu. Mtu anapanga kufanya kitu fulani, lakini wakati wa kufanya unapofika hafanyi na anajipa sababu. Anachoamini ni kwamba asipofanya kitu mara moja hakuna madhara makubwa, atafanya siku nyingine. Asichojua ni kwamba kila tukio lina madhara kwenye maisha yake. Mfano mtu anapoacha kufanya kile alichopanga, hilo lina madhara makubwa kwake, anajichukulia kama mtu asiye makini na ni rahisi kurudia hilo kwenye maeneo mengine ya maisha yake.
- Kukosa uwajibikaji. Watu wote waliofanikiwa wanajua uwajibikaji ni muhimu sana kwenye mafanikio yao. Ndiyo maana watu hao wana mamenta, makocha na washauri mbalimbali, hawa wanahakikisha watu hao wanatekeleza kile walichopanga. Lakini wasiofanikiwa hawapendi kabisa uwajibikaji, wao wanataka kuendesha maisha kama wanavyojisikia wenyewe. Bila ya uwajibikaji, hakuna hatua mtu anaweza kupiga.
- Kuzungukwa na watu wa kawaida. Utafiti unaonesha kwamba maisha yako ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka au unaotumia nao muda wako mwingi. Kinachowafanya watu wengi kubaki kwenye umasikini ni kuzungukwa na watu masikini. Unapozungukwa na watu masikini, fikra zako na hata matendo yako yanakuwa kama yao na hilo linapelekea ubaki kwenye umasikini.
- Kutokujiendeleza binafsi. Watu wanaoshindwa huwa hawajiendelezi wao binafsi. Wakishahitimu masomo ndiyo basi, hawajisumbui tena kuendelea kujifunza hasa kusoma vitabu. Na hata wakisoma vitabu basi ni vya hadithi, na siyo vya kujifunza. Wale wanaofanikiwa wanaweka uzito mkubwa sana kwenye kujiendeleza wao binafsi. Wananunua na kusoma vitabu vinavyowafanya kuwa bora zaidi. Pia wanahudhuria mafunzo na semina mbalimbali zinazowafanya kuwa bora zaidi.
- Kukosa uharaka. Watu wengi hawapigi hatua kwenye maisha yao kwa sababu hawana ile hali ya uharaka wa kuchukua hatua kwenye jambo lolote. Ni watu wa kuahirisha mambo na kusubiri mpaka dakika za mwisho ndiyo wachukue hatua. Kwa kukosa hali hii ya uharaka wengi wamekuwa wanajichelewesha wao wenyewe kufanikiwa.
Rafiki, epuka sababu hizi saba ambazo zimewaweka wengi kwenye umasikini mkubwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini huo kama utaendelea kukumbatia sababu hizo.
HATUA YA TATU; CHORA MSTARI.
Baada ya kuzijua sababu ambazo zimekuweka kwenye umasikini kwa muda mrefu, sasa kuna hatua ya tatu ya kuchukua, ambayo ni kuchora mstari.
Kuchora mstari maana yake ni kufanya maamuzi kwamba kuanzia sasa mambo yako yote yanabadilika. Unaachana na mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Maamuzi hayo unayafanya sasa na hatua unaanza kuzichukua sasa. Siyo baadaye, siyo kesho, siyo wiki ijayo, siyo mwezi ujao na wala siyo mwaka ujao. Ni leo, ni sasa. Kama hutachora mstari sasa hivi na kuanza kuishi maisha mapya, utaendelea kujichelewesha kufanikiwa.
Kataa kuwa wa kawaida, kataa kubaki kwenye umasikini na maisha magumu na chagua kufanikiwa na kufikia utajiri. Chagua kuziishi tabia ambazo zitayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usikubali kuendesha maisha yako kwa ukawaida, halafu unapofika ukingoni mwa maisha unagundua hukuishi maisha yako. Chagua leo kuyaishi maisha yako, chagua kuwa bora zaidi ya pale ulipo sasa. Yote yanawezekana na yapo ndani ya uwezo wako.
Saturday, June 22, 2019
ACHA MAIGIZO KATIKA MAISHA YAKO, ISHI UHALISIA WAKO
Watu wanalalamika kwamba hawapati watu sahihi kwenye maisha
yao, hawapati wenza sahihi, hawapati watu sahihi wa kushirikiana nao. Na hilo ni rahisi kupata sababu, ambayo ni kila mtu kuwa kwenye maigizo wakati wa kuanza. Na
kwa kuwa tunajua maigizo huwa hayadumu muda mrefu, basi muda
unapokwenda, rangi halisi za watu zinaonekana na watu kufikiri wenzao
wamebadilika. Watu huwa hawabadiliki, ila wanajionesha, wanachoka kuigiza na mambo yanabaki wazi.
Acha
kuigiza, acha kuishi maisha ya wengine, ishi maisha yako, ishi uhalisia
wako, fanya kile chenye maana kwako, kile ambacho unakiamini kweli,
kile ambacho upo tayari kukifanya hata kama hakuna anayekuangalia,
hakuna anayekusifia, na kwa njia hii utakuwa na maisha yenye furaha, na
pia utawavutia watu sahihi kwa kuwa kile unachoonesha ndicho kilicho
ndani yako.
Subscribe to:
Posts (Atom)