Kama
hujui unakokwenda, huwezi kufika na hata ukifika hutajua kama umefika.
Hatua ya kwanza kuchukua ili kupata unachotaka ni kujua wapi
unapokwenda.
Unapaswa
kujua kwamba kila mtu kwenye maisha kuna kitu anauza, iwe upo kwenye
biashara au ajira, hivyo jua ni nini unachouza na uweze kukiuza vizuri
zaidi.
Zipo
njia tatu za kukuwezesha kuuza zaidi, kupata wateja wapya, kuuza zaidi
kwa wateja ulionao na kuwafanya wateja ulionao waje kununua mara nyingi
zaidi.
Kama
umeajiriwa, unauza muda wako, utaalamu wako na uzoefu wako kwa mwajiri
wako. Na kitu kimoja ambacho kila mwajiri anapenda sana ni mtu ambaye
anaweza kutatua matatizo na siyo anayesababisha matatizo.
Chochote
unachochagua kufanya, hakikisha unakifanya kwa utofauti mkubwa na
wengine wanavyokifanya. Usikubali kufanya kwa mazoea au kuiga kile
ambacho wengine wanafanya.
Wape
wateja wako urahisi wa kusema ndiyo kwa kile unachouza, kwa kutoa
thamani kubwa sana ambayo hawawezi kuipata sehemu nyingine yoyote ile.
Yaani unapaswa kutoa thamani kubwa kiasi kwamba mteja atajiona ni mjinga
kujaribu kutafuta sehemu nyingine ya kununua.
No comments:
Post a Comment