Wakati
mapinduzi ya viwanda yanaanza, watu waliambiwa ili kuwa na usalama wa
kazi basi soma kwa bidii, faulu sana na utapata kazi nzuri ambayo
utaifanya mpaka kustaafu kwako na hapo utalipwa mafao ya kukuwezesha
kuishi mpaka uzeeni.
Mapinduzi
ya viwanda yamefika tamati na sasa tupo kwenye mapinduzi ya taarifa.
Katika zama hizi uhakika pekee wa wewe kuwa na usalama kwenye kazi au
biashara siyo tu elimu au taaluma uliyonayo, bali kutengeneza ubobezi
kwenye kile unachofanya kiasi kwamba watu watapenda kufanya kazi na
wewe.
Unapaswa
kujijengea sifa ya ubobezi wa hali ya juu kwenye kile unachofanya kiasi
kwamba kila mwenye uhitaji unaohusu unachofanya anakufikiria wewe au
anaambiwa waje kwako.
Na
hilo linawezekana kama utaweka juhudi katika kujua vizuri kile
unachofanya, kukifanya vizuri na pia kutengeneza mtandao wa watu
wanaojua kuhusu unachofanya na hivyo kusambaza sifa zako kwa wengine
wengi.
No comments:
Post a Comment