Tumeona
kikwazo cha wateja kununua kwa mara ya kwanza kwako ni hatari ya
kupoteza fedha zao iwapo kitu walichonunua hakitawafaa kama walivyotaka.
Tumejifunza njia moja ya kuwapa ofa au zawadi ambayo itawasukuma
kununua.
Ipo
njia nyingine yenye nguvu zaidi, ambayo ukiitumia lazima mteja anunue.
Njia hiyo ni kuondoa kabisa hatari kwa mteja. Yaani hapa unaondoa nafasi
yoyote ile ya mteja kupoteza fedha zake, na unakwenda mbele zaidi kwa
kumlipa kwa muda au chochote alichopoteza.
Jay
anaiita mbinu hii BETTER-THAN-RISK-FREE GUARANTEE (BTRF). Biashara
nyingi huwa zinamrudishia mtu fedha aliyonunulia kitu kama hakijamfaa,
au kumpa kitu kingine. Sasa wewe unahitaji kwenda zaidi ya hapo,
unahitaji kumrejeshea mteja kile alicholipa, lakini pia kumlipa fidia
kwa muda aliopoteza au usumbufu uliomsababishia.
Kwa
kuwa tayari kumlipa fidia mteja wako pale ambapo hajaridhishwa na
ulichomuuzia inaonesha unamjali sana na pia una uhakika sana na kile
unachouza. Kadiri mteja anavyopata uhakika wa aina hii, ndivyo
anavyokuwa tayari zaidi kununua kile unachouza.
Kama
kweli unajali kuhusu wateja wako na kama kweli unaamini kwenye kile
unachouza na umechagua kuwazia wateja sahihi, unaweza kutumia mbinu hii
na hutapata hasara yoyote. Kwa sababu kwanza utawahudumia wateja sahihi
na watakuwa tayari kwenda na wewe kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment