Ili
kufanikiwa kwenye biashara au chochote unachofanya, unapaswa
kujitofautisha na wale wanaofanya kile unachofanya. Hivyo hapa unahitaji
kutengeneza utofauti wako na kuwaeleza wateja nini wakija kwako
wanapata ambacho hawawezi kupata sehemu nyingine yoyote ile.
Angalia
jinsi washindani wako wanafanya mambo yao, kisha wewe kuwa na njia bora
zaidi ya kufanya ambayo inawapa wateja thamani kubwa, kisha hakikisha
wateja wanajua kuhusu utofauti wako. Njia zote za masoko unazotumia
zinapaswa kueleza utofauti wako na wengine, ili wateja washawishike kuja
kwako na siyo kwenda kwa wengine.
Baadhi ya maeneo ambayo unaweza kujitofautisha kwenye biashara ni bei, huduma, ubora, upekee, uharaka, uhakika na mengine.
Njia
bora ya kujitofautisha ni kuchagua eneo dogo (niche) ambalo
utalihudumia vizuri zaidi kuliko kuhangaika na eneo kubwa. Hapa
unachagua aina fulani ya wateja, wenye sifa za kipekee ambao utaweza
kuwahudumia vizuri na kuachana na wateja wengine wote. Kuachana na
wateja wengine huwa ni kitu kigumu kwa wafanyabiashara wengi, lakini
unapaswa kukumbuka kwamba huwezi kuwaridhisha watu wote.
Tengeneza
ujumbe unaobeba utofauti wako kibiashara na kila unapokutana au
kuwasiliana na wateja hakikisha unawapa ujumbe huo. Ujumbe huu unapaswa
kurudiwa rudiwa mara nyingi mpaka watu wauelewe na kuihusisha biashara
yako na ule utofauti unaotengeneza. Yaani pale mteja anapotaka kitu cha
tofauti na kinachomfaa yeye, basi anajua atakipata kwako
No comments:
Post a Comment