Ile kauli kwamba matajiri hawana furaha au huwezi kuwa na fedha na
ukawa na furaha, ni mtego ambao watu wamekuwa wanajitengenezea wenyewe
bila ya kujua.
Ipo hivi rafiki, wengi tunapokuwa tunaanzia chini, huwa tunafikiri
tutakapopata fedha basi ndiyo zitakuwa jawabu la kila kitu. Hivyo
tunaahirisha maisha yetu yote mpaka pale tutakapopata fedha.
Na hata kwa upande wa furaha, tunaahirisha furaha yetu tukiamini
tukishakuwa na fedha basi ndiyo tutakuwa na furaha. Tunaacha kufanya
yale mambo madogo madogo ya kila siku ambayo yanatuletea furaha,
tukiamini kwamba tukishakuwa na fedha nyingi, basi furaha itakuja
yenyewe.
Lakini hilo ni kinyume kabisa na msingi wa furaha, fedha haileti
furaha, bali furaha inaleta fedha. Kwa kifupi ni kwamba fedha ni zao la
furaha, na siyo kama wengi wanavyofikiri kwamba furaha ni zao la fedha.
Hivyo basi, usiahirishe furaha yako sasa kwa sababu unatafuta kwanza
fedha na unafikiri ukishakuwa nayo basi utapata furaha. Badala yake ishi
maisha yako kamili sasa, fanya vile vitu vidogo vidogo vinavyoleta
furaha kwenye maisha yako na hivi vitakuwezesha kupata fedha zaidi na
kwa kutokutumia nguvu kubwa kama unavyofanya unapokuwa huna furaha.
Usipuuze kitu chochote muhimu kwenye maisha yako kwa sababu unakazana
kupata fedha, weka kipaumbele chako kwenye furaha na fedha itakuwa
matokeo.
Jipende wewe mwenyewe kwanza, fanya kile unachopenda na zungukwa na
wale wanaokupenda, haya yatakuletea furaha na furaha yako itavutia fedha
zaidi kwako.
Fuata hili na hutafikia kwenye hali ya wengi ambao wana fedha lakini
hawana furaha, wewe tayari unayo kanuni ya kuwa na furaha na kuwa na
utajiri kwa wakati mmoja. Ifanyie kazi.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment