( 1 ). MJASIRIAMALI.
Hii
ni haiba ambayo inabeba nafsi ya mjasiriamali. Mjasiriamali ni mtu wa
kuja na mawazo mapya ya kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zinapatikana.
Mjasiriamali ni mtu wa ndoto na maono makubwa, mtu wa kutengeneza picha
za mambo yasiyoonekana. Mjasiriamali anaangalia mambo yalivyo na
kujiuliza vipi kama yangekuwa tofauti.
Bila ya mjasiriamali hakuna mawazo mapya, hakuna ugunduzi na wala hakuna maono makubwa ya kibiashara.
Nafsi
ya ujasiriamali ndiyo inawasukuma wengi kuingia kwenye biashara, lakini
nafsi hii imekuwa haidumu kwa muda mrefu, inazidiwa nguvu na nafsi
nyingine na ndiyo maana tunasema mtu anakuwa amepatwa na kifafa cha
ujasiriamali. Wazo la ujasiriamali linamjia kwa muda mfupi na nafsi hii
kuondoka kabisa.
( 2 ). MSIMAMIZI/MENEJA.
Hii
ni haiba inayobeba nafsi ya usimamizi au umeneja kwenye biashara.
Meneja ndiye mtu ambaye anaisimamia biashara kwa ukaribu, kuhakikisha
kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Huyu ni mtu ambaye
anahakikisha rasilimali za biashara zinatumika vizuri. Pia meneja
anahakikisha kilichofanywa kwenye biashara jana ndiyo kinafanywa leo.
Mameneja hawapendi kujaribu vitu vipya kwa sababu hawana uhakika navyo.
Tofauti
kubwa ya mjasiriamali na meneja ni mabadiliko, mjasiriamali anatafuta
mabadiliko na kuwa tayari kuyafanyia kazi. Lakini meneja hataki kabisa
mabadiliko, anataka kuendelea kufanya mambo kama ambavyo amekuwa
Meneja
ndiyo nafsi inayoiwezesha biashara kufanya kazi. Mjasiriamali anakuwa
na mawazo mapya na makubwa, lakini hawezi kuyafanyia kazi mawazo hayo
kwa muda. Hivyo anahitaji kuwa na meneja ambaye anafanyia kazi mawazo
hayo mapya.
( 3 ).FUNDI/MTAALAMU.
Hii
haiba inayobeba nafsi ya ufundi au utaalamu unaohitajika kwenye
biashara. Huu ni ule ujuzi au utaalamu ambao mtu anaingia nao kwenye
biashara. Fundi kazi yake ni kutengeneza vitu na anapenda sana
kutengeneza vitu. Haiba hii ya ufundi inapenda kufanya yale yanayopaswa
kufanywa kwenye biashara.
Wakati
mjasiriamali anakuja na mawazo mapya, meneja anaweka mfumo mzuri wa
kufanyia kazi mawazo hayo, fundi ndiye anayefanya kazi kwenye biashara
hiyo na kuzalisha matokeo yanayohitajika. Fundi ndiye anayezalisha
matokeo kwenye biashara.