Tumbo la chini ni kituo cha nguvu kwenye mwili hili ni eneo la
mwili kwenye usawa wa kitovu. Kituo hiki kinadhibiti utumbo mpana,
kongosho, kiuno, mifuko ya mayai na tumbo la uzazi kwa wanawake.
Kituo
hiki kinahusika na ulaji, umeng’enyaji na utoaji wa mabaki ya chakula
mwilini. Homoni mbalimbali huzalisha kwenye kituo hiki ambazo zinahusika
na umeng’enyaji wa vyakula.
Kazi
kubwa ya kituo hiki ni mahusiano ya kijamii, familia, utamaduni na hata
mahusiano baina ya mtu mmoja na mwingine. Hiki ni kituo cha kushikilia
au kuachilia au kuondoa. Kituo hiki kinapokuwa vizuri, mtu unakuwa na
utulivu na kujisikia salama na amani.
Watu
wengi wamekuwa wanatumia nguvu ya kituo hiki vibaya kwa kuwa na hasira
na vinyongo kwa wengine na kukosa maelewano mazuri na wengine. Kila
unaposhikilia kitu ndani yako dhidi ya mtu mwingine, unashikilia nguvu
ambayo ungeweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Ulaji
uliopitiliza pia unaathiri kituo hiki kwa nguvu kubwa kutumika
kumeng’enya chakula na kuondoa uchafu mwilini kitu ambacho kinazuia
nguvu hiyo kutumika kwenye kutenda miujiza.
Ili kuweza kutumia vizuri nguvu ya kituo hiki, tunapaswa kudhibiti ulaji wetu na kuimarisha mahusiano yetu na wengine.
No comments:
Post a Comment