ULIPO SASA; ni katika mazingira gani unajisikia furaha? Je umeridhika na pale unapoishi sasa na jinsi unavyoishi? Je unaamini unastahili kuwa na mazingira bora na ya kifahari, kuanzia nyumbani mpaka kwenye kazi zako?
UNAKOTAKA KUFIKA; tengeneza picha ya mazingira bora kwako, kuanzia
nyumbani, kazini na popote unapokuwa. Kama usingekuwa na kikwazo
chochote, hasa kifedha, ungeishi nyumba ya aina gani, ungeendesha gari
ya aina gani na eneo lako la kazi lingekuwaje? Beba picha hii kila siku
ya maisha yako na ifanyie kazi kuifikia.
VIWANGO VYA KUJIWEKEA; yafanye mazingira yako kuwa safi na yanayokupa hamasa zaidi. Fanya chumba chako kuwa safi, nyumba safi, mazingira masafi na hata eneo lako la kazi liwe safi na vitu vipangiliwe kiasi cha kuwa rahisi kupata chochote unachotaka kutumia.
KITABU CHA KUSOMA; soma kitabu kinachoitwa THE MAGIC OF THINKING BIG kilichoandikwa na David Schwarrz. Kitabu hiki kitakusukuma kuboresha maisha yako na kuwa na ndoto kubwa kuhusu nyumbani kwako, ofisini kwako na mengine mengi.

No comments:
Post a Comment