TUMBO LA JUU, ni eneo la nguvu kwenye miili yetu ,hili ni eneo la
mwili juu ya kitovu. Kituo hiki kinadhibiti tumbo la chakula, utumbo
mwembamba, bandama, ini, mfuko wa nyongo, figo na tezi zilizopo juu ya
figo.
Kituo
hiki kinahusika na matakwa yetu, nguvu zetu, udhibiti, hamasa, msukumo
na utawala. Hiki ni kituo cha mashindano na nguvu binafsi, kujithamini
na hata kuwatawala wengine.
Kituo
hiki kinapokuwa vizuri, unaweza kutumia nguvu za kituo hiki kufikia
malengo yako, kuwa na hamasa ya kupiga hatua zaidi na kuzivuka
changamoto mbalimbali unazokutana nazo. Kituo hiki pia kinakupa nguvu ya
kujilinda wewe mwenyewe na kuwalinda wale wa karibu kwako.
Watu
wamekuwa wanatumia vibaya nguvu za kituo hiki kwa kujiona wao ni wa
muhimu kuliko wengine, kutaka kuwatawala wengine na hata kuwaonea
wengine pale mtu anapokuwa na mamlaka au nguvu fulani.
Kutumia
vizuri nguvu za kituo hiki tunapaswa kujijua sisi wenyewe na kujua nini
hasa tunachotaka kisha kuweka nguvu zetu kwenye maeneo hayo. Hatupaswi
kujionesha kwa wengine au kuwalazimisha wengine wawe kama tunavyotaka
sisi.
No comments:
Post a Comment