ULIPO SASA; je unaamini kwamba wewe ni mbunifu? Je kuna mtu mbunifu ambaye unapenda sana kuwa kama yeye? Ni mambo gani ya kibunifu ambayo unafanya sasa kwenye maisha yako? Je ni vipaji gani ulivyonavyo na unavitumiaje?
UNAKOTAKA KUFIKA; ni ubunifu gani ambao ungependa kuwa nao na kubobea
zaidi siku zijazo? Ni jinsi gani unaweza kutumia ubunifu huo kuwasaidia
wengine zaidi. Chagua ubunifu unayotaka kuwa nao na jiendeleze kila siku
na kutoa mchango kwa wengine.
VIWANGO VYA KUJIWEKEA; chagua aina ya ubunifu ambao utakuwa unajihusisha nao na kila siku tenga muda wa kujiendeleza kwenye ubunifu huo. Unaweza pia kujiunga na wengine au kushiriki madarasa yanayokuwezesha kukuza zaidi ubunifu wako.
KITABU CHA KUSOMA; soma kitabu THE WAR OF ART cha Steeven Pressfield ambacho kitaamsha na kuchochea ubunifu uliopo ndani yako na kuweza kufanya kazi za kibunifu.

No comments:
Post a Comment