Kituo
cha kwanza cha nguvu kipo kwenye viungo vyetu vya uzazi na kinadhibiti
sehemu za mwili zilizopo chini ya kitovu. Hapa inahusika uke, uume,
kibofu cha mkojo, sehemu ya mwisho ya utumbo na hata ngozi na misuli
inayozunguka maeneo haya.
Kazi
kubwa ya kituo hiki ni uzazi, jinsia, kujamiiana na kutoa uchafu
mwilini. Homoni za uzazi huzalishwa kwenye kituo hiki. Kituo hiki kina
nguvu kubwa sana ya ubunifu na uumbaji, fikiria nguvu ambayo inatumika
katika kujamiiana na hata kupata mtoto.
Watu
wengi wamekuwa wanatumia nguvu ya kituo hiki vibaya kwa kuelekeza nguvu
zao nyingi kwenye kujamiiana na kuwa na mahusiano mengi ya kingono.
Hili linawapunguzia uwezo wa kufanya makubwa kwenye maisha yao.
Ili
uweze kutumia nguvu hii ya kituo cha kwanza katika kufanya miujiza,
unapaswa kujidhibiti sana kwenye eneo la ngono, kwa kuwa hili ndiyo
linapoteza nguvu za wengi.
No comments:
Post a Comment