Showing posts with label BIASHARA NA UJASIRIAMALI---TUSOME VITABU----TANZANIA.. Show all posts
Showing posts with label BIASHARA NA UJASIRIAMALI---TUSOME VITABU----TANZANIA.. Show all posts

Thursday, May 15, 2025

MAKALA : USILAUMU WAZAZI , SI KOSA LAKO HATUKUFUNDISHWA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA NA MAUZO---JIFUNZE UINUKE---BIASHARA NI AKILI NA MAARIFA------------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

*Siyo Kosa Lako, Hujafundishwa TU!*

‎Kakaa/Dadaa..

‎Unajua kuna watu wanawacheka wajasiriamali wadogo?

‎Huku wakiwasema vibaya:...

‎*Mbona kila biashara unayoanzisha haifiki miezi mitatu?*

‎*Unapenda kulalamika sana!”

‎*Wewe huwezi fanikiwa kamwe!*

Na huwa naumia nikisikia haya maneno.

‎Kwa sababu…

‎Watu hawajui mateso yanayomfanya mtu aamue kuuza maandazi saa 12 asubuhi bila hata chai.

‎Hawajui…

‎Maumivu ya kutafuta mtaji wa elfu 20 kwa kuazima mia mia.

‎Kunyanyaswa na maneno ya jamaa zako:

‎ “Kama ni biashara ya maandazi si kila mtu anafanya?”

‎Kukesha ukitengeneza sabuni halafu asubuhi mvua inanyesha, hakuna mtu hata mmoja kununua.

‎‎Sasa leo nakuambia ukweli:

‎Siyo Kosa LAKO.

‎Haujafundishwa TU!..

‎Tatizo Si Wewe, Ni Mfumo Wetu.

‎Shule zetu hazikufundisha namna ya kuuza.

‎Hazikufundisha namna ya kujua faida.

‎Hazikufundisha namna ya kumshawishi mteja.

‎Tulifundishwa 1+1=2.

‎Lakini hatukufundishwa jinsi ya kutengeneza buku kwa kuuza karanga.

‎Ukatoka shule ukiwa na degree.

‎Au ukiwa form four.

‎Au hata bila cheti.

Lakini wote mko sokoni mnaanza biashara kama vipofu wanaovuka barabara.

‎Na Ndio Maana…

‎Unajikuta unafungua duka la vocha,

‎Unaanza kuuza na sabuni tano, pipi za mchina, na airtime ya mia.

‎Mwishoni mwa mwezi…

‎Umeuza elfu 50.

‎Umebakiwa na 10.

‎Na hata hujui imepotelea wapi.

‎Wewe si mzembe.

‎Wewe si mjinga.

‎Wewe ni mtu jasiri lakini hujapewa silaha.

‎Sasa Sikiliza Hii:

‎Kabla hujaanza biashara yoyote…

‎Unahitaji kujua vitu vitano tu vya msingi:

‎1. Shida ya watu ni ipi?

‎Watu hawataki bidhaa, wanataka suluhisho.

‎2. Unawauzia kina nani?

‎Hakuna biashara ya “kila mtu”

‎3. Unawafikiaje?

‎Kama hawaitwi hawaji. Kama hawajui hawanunui.

‎4. Bei yako inasemaje?

‎Bei nzuri haimaanishi rahisi inamaanisha INAOANA na thamani.

‎5. Faida yako iko wapi?

‎Si pesa inayoingia, ni pesa inayobaki baada ya gharama.

‎Stori Ya Kweli Ya Dada Zawadi Wa Gongo La Mboto....

‎Zawadi alikuwa anafua nguo kwa watu.

‎Kila siku jua likitoka, anajitwika ndoo, anazunguka mtaani akitafuta wateja wa kuwafulia hadi jioni.

‎‎Analipwa elfu mbili elfu tatu.

‎Anaondoka na macho mekundu, mikono iliyochubuka,

‎Lakini hana hela hata ya sabuni.

‎Siku moja alihudhuria semina ya biashara.

‎Akaambiwa kitu kimoja tu:

‎‎ *Fungua huduma yako. Uisajili. Toa package. Weka namba zako mitandaoni.*

‎Leo Zawadi haendi nyumba hadi nyumba.

‎Anapokea simu.

‎Wateja wanamfuata.

‎Anatoza elfu kumi hadi elfu ishirini kwa huduma ya kitaalamu.

‎Na bado anafua nguo.

‎Lakini kwa akili.

‎Tunaambiwa tukomae. Lakini hatuambiwi namna.

‎Tunaambiwa tufanye kazi kwa bidii. Lakini bidii bila maarifa ni kama kukata mti kwa kijiko.

‎SULUHISHO?

‎Sihitaji nikuambie uache biashara.

‎La hasha.

‎Nakuheshimu.

‎Ninachokuambia ni hivii…:

‎Chukua hatua ya kutafuta elimu ya msingi ya biashara.

‎Elimu inayoeleweka.

‎Elimu ya mtaani.

‎Elimu ya kweli.

‎Kabla hujapoteza muda tena,

‎Kabla hujakataliwa tena,

‎Kabla hujachoka kujaribu jifunze.

Kwa Nini?

‎Kwa sababu:

‎Huwezi kufanikiwa kwa kukurupuka.

‎Na

‎Siyo kosa lako kuwa hujui.

‎Lakini litakuwa kosa lako ukikataa kujua.

‎Kama makala hii imekuongelea wewe, huna haja ya kujionea aibu.

‎Kila shujaa alianza akiwa hajui.

‎Lakini waliamua KUJIFUNZA.

‎‎Nataka nikupe silaha mbili za siri.

‎Ni silaha za kumtokomeza ujinga,

Silaha hizo ni Elimu Ya Msingi Ya Biashara na CHUO CHA MAUZO, Kwa Mtu Wa Mtaa.

‎#SioKosaLako

‎#JifunzeUinuke

‎#BiasharaNiAkiliNaMaarifa