Friday, January 9, 2015

BIASHARA YA KUMBI ZA STAREHE / SHEREHE / HARUSI / MIKUTANO.


KUMBI   ZA   STAREHE/SHEREHE/HARUSI/MIKUTANO
 
Biashara  ya   ukumbi  wa   starehe /sherehe/ harusi/mikutano  ni   biashara  nzuri  kwani   kutokana   na  maendeleo  ya  sayansi   na  teknolojia, mahitaji  ya   kumbi  za   starehe /sherehe/starehe /mikutano  yameongezeka  sana.  Biashara  hii  inahitaji  mtaji  mkubwa  kuifanya  na  ubunifu  ili  kufanikiwa. Ili  ukumbi  uweze  kuvutia  wateja  unatakiwa  uwe  na  nafasi  kubwa  yenye  sakafu , kuta  zipigwe  rangi, upambwe  kwa   maua,  uwe  na  kaunta   ya  vinywaji  na  ikibidi  uwe  na  huduma  za  vinywaji, uwe  unaingiza  hewa   safi ,  uwe  na  mapanga  boi  au  kiyoyozi  na  pia  uwe   na  vivutio  vingine   kama   michezo  ya  “darts”   “pool  table”  uwe  na  luninga , muziki  wa  disko  na  uwe   na  huduma   ya   vitafunio   na    vyakula. Ukumbi  unapaswa   kutangazwa  ili   ufahamike. Vile  vile   mmiliki  wa   ukumbi  unaweza  kuingia   mkataba   na   bendi  za   muziki  au   vikundi  vya  sanaa  viweze   kufanya   maonyesho   na  kuvutia   wateja. Ukumbi  unaweza   kuendesha  matamasha  ya  burudani  kuanzisha  kikundi  cha  sanaa  au  bendi  ya  muziki  kufanya  maonyesho  ili   kuvutia  wateja.
  
Mapato  ya ukumbi  hupatikana  kutokana  na  viingilio  vinavyolipwa  mlangoni  kuingia  ukumbini  na  kuingia   mikataba   na  bendi  za   muziki  au   vikundi  vya  sanaa   kufanya  maonyesho  ukumbini.

Matatizo  ya   biashara  hii  ni   kushindwa   kudhibiti  mapato   kwa  watu  kuingia  ukumbini   lakini  mapato  yote   hayawasilishwi   kwa   mmiliki  wa  ukumbi , kukosekana   kwa  wateja   kama  ukumbi  hauvutii , uchafu   kwenye  ukumbi   na  vyooni ,  uchakavu   wa   ukumbi  na  kukosekana  ubunifu   toka   kwa   mmiliki  wa   ukumbi.Ili  kukabiliana  na  matatizo  haya   mmiliki  wa  ukumbi   anatakiwa  kuwa   mbunifu  na azingatie  mambo   niliyoeleza  hapo  mwanzoni  kuhusu   uendeshaji wa   biashara  hii, awape  motisha  wafanyakazi  wake  ili   wamfanyie   kazi    yake  vizuri.Pia  aweke  sanduku   la   Maoni   kupata    maoni   ya   wateja    na   autangaze  ukumbi   wake   na  kuingia   mikataba  na  vikundi vya   muziki  na  sanaa.

2 comments:

  1. Naweza kupata ramani ya ukumbi mdogo wa sherehe ukubwa 2000cmx800cm?

    ReplyDelete
  2. Nawweza kupata makadirio ya garama za ujenzi wa ukumbi wa wastani unaoweza kuingia watu 250-300?

    ReplyDelete