Mmiliki wa
Bendi
Na Biashara Ya
Muziki
Asha Baraka mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta ,Tanzania amepata mafanikio makubwa katika sanaa ya Muziki !!
Asha Baraka mmiliki wa bendi ya Twanga pepeta ,Tanzania amepata mafanikio makubwa katika sanaa ya Muziki !!
Ili kuwa
mmiliki wa bendi
unapaswa uwe na
mapenzi na Muziki.
Wakati mwingine wamiliki
wa bendi za
muziki wanakuwa ni
wanamuziki. Biashara hii inahitaji
mtaji mkubwa kununulia
vyombo vya muziki
ambavyo ni aghali
sana na pia
kuwalipa mshahara wanamuziki.Biashara hii
inahitaji ubunifu ili
uweze kupata fedha.Biashara hii
inaweza kuingiza mapato
kwa njia mbalimbali
pamoja na viingilio
kwenye kumbi za
starehe, mialiko ya kutumbuiza
katika sherehe , mikataba ya
kupiga muziki katika
kumbi au mahoteli
kwa malipo maalumu
pamoja na mauzo ya
kanda za muziki.
Matatizo ya
biashara hii ni : kukosekana kwa
ubunifu kwa mmiliki
wa bendi au
wanamuziki, hivyo kuwa kuwa
gharama kubwa za
uendeshaji, uchakavu wa vyombo , maendeleo ya
teknolojia ambapo
mwanamuziki anaweza kwenda
studio na kurekodi
nyimbo zake hivyo
kuondokana na umuhimu
wa kujiunga na
bendi. Ili kukabiliana na
matatizo haya unatakiwa
uwe mbunifu na
kundi dogo la
wanamuziki wabunifu , wanaojua
kuimba na kupiga
chombo zaidi ya kimoja.Waanzishe mitindo
inayovutia wateja. Wajiepushe kuiga
muziki wa watu
wengine.Bendi itangazwe ,
iwe na
malengo ya kuwa
bendi ya Kimataifa.Ifanye ziara
nje ya nchi
kwani huko nako
wangependa kupata vionjo
vya muziki tofauti
tofauti na wa
kwao. Bendi irekodi
nyimbo nzuri na
kuuza kanda za
kaseti , video , CD na DVD. Bendi
iendeshe matamasha, Pia mmiliki
wa Bendi anatakiwa
kuwa na Ukumbi
wake ambapo ni makao makuu
ya bendi na
washabiki wajue hivyo.
No comments:
Post a Comment