Mwanamuziki Na Biashara
Ya Muziki
Marehemu Dr. Remmy Ongala wa Tanzania alipata Mafanikio makubwa katika sanaa ya Muziki. Nyimbo zake zinakumbukwa mpaka leo kwa ujumbe wenye mafundisho.
Marehemu Dr. Remmy Ongala wa Tanzania alipata Mafanikio makubwa katika sanaa ya Muziki. Nyimbo zake zinakumbukwa mpaka leo kwa ujumbe wenye mafundisho.
Biashara ya muziki
ni nzuri kwa
mwanamuziki akiwa na
kipaji na akijua
namna ya kukiendeleza
kipaji chake.Anaweza kuwa
mwimbaji, Mpigaji wa chombo
Fulani cha muziki
kama vile gitaa , filimbi , tarumbeta, zumari ,
kinanda au ngoma. Baada
ya kujua kipaji chako
unapaswa kukiendeleza kipaji
hicho kwa kusomea
muziki au kujifunza
kutoka kwa wanamuziki
mahiri na ukishaujua
muziki unaweza kuanzisha bendi
au kutafuta studio
ya kurekodi muziki
wako na kuuza
kanda zako. Katika kurekodi
unapaswa kuwa na
fedha za kulipa
gharama za kurekodi. Kama huna
fedha unaweza kutafuta
mfadhili na ukaingia
naye mkataba wa
kugawana mapato ya
muziki ambapo itabidi
litafutwe soko na kutangazwa.Mbinu inayotumika
kutangazwa ni kupeleka
kanda hiyo katika
studio za redio, ikapigwa sana
na kusifiwa. Baada
ya hapo mwanamuziki
huandaa uzinduzi wa
kanda yake. Ili
kuvuta wateja unaweza, kufanya hivi : Unaweza kufanya ziara
ya mikoani kutangaza
muziki wako na
kuuza kanda zako.
No comments:
Post a Comment