Monday, January 5, 2015

MUZIKI KAMA FANI YA SANAA NA BIASHARA.

Sanaa  Ya   Muziki  Na   Biashara
 
 Mwanamuziki  chipukizi  Diamond wa  Tanzania  anaendelea  kupata mafanikio  makubwa  katika  sanaa  ya  Muziki .  Mungu  ambariki.
 
Nyanja  ya   muziki  ni  pana  sana  na  inawagusa  watu  wengi. Ni  fani  nzuri  na   inaleta  AJIRA  kwa  wengi  kwa  vile  ina  mvuto  hasa  pale  ambapo  panakuwepo  mfumo  mzuri  wa ubunifu  wa  nyimbo , utunzi  wake  na  uhitaji  wa  sanaa  hii  kwa  jinsi  invyotoa  burudani  na  mvuto  wa  hisia  nyingi  na  nzuri. Muziki  kama  sanaa  HAIJAPEWA  Kipaumbele   hapa  TANZANIA  kwa  maana  ya  kukuzwa  tangu  watoto  wetu  wakiwa   makinda, hadi  utoto  udogo  hadi  umri  wa  kwenda  shule  pindi  wawapo  mashuleni , wawapo  nyumbani  na  kupewa  ushindanishi  sawa  na  fani   na  sanaa  nyingine.Muziki  ni  sanaa ya  ajabu  sana.Upo  Katika  viini  vya  ujuzi  za  tafakari  katika  bongo  za  binadamu   na  kwa  namna  fulani  hata  viumbe  vingine.Ni  muhimu  sana  kutambua  UTAJIRI  unaoweza  kupatikana  kwa  Watanzania  wengi  kwa   kupitia  nyanja  hii  ya  muziki  kwa  kukuzwa  vipaji  kwa  jamii  yetu  ya  kuienzi  kwa  kila  namna  inayofaa  na  hivyo  kuithamini.Baada  ya  kukuza  vipaji, tutahitaji  kuwa  na  sheria  kali  ya  hati  miliki.
    
Mfano   mzuri  ni  katika  nchi  zilizoendelea  Ulaya  na  Marekani  ambapo  walio  wengi  wamekuwa  matajiri  kwa  kufanya   biashara  hii. SIRI   YA  MAFANIKIO  ni  kuendesha  biashara  kitaalamu  na  kibiashara  zaidi.  Hapa  kwetu   wanamuziki  hutoa   burudani  tu   wakati  hawalipwi  chochote  au  wanapata  malipo  kidogo  na   kuambulia sifa  tu.. Biashara  ya   MUZIKI  ikiendeshwa  vizuri  inaweza  kutoa   AJIRA  na  kipato  kwa   watu   wengi  sana  kama  vile ,  wanamuziki  wenyewe ,  wamiliki  wa  bendi ,  wamiliki  wa  kumbi  za  muziki,wamiliki  wa  studio  za  kurekodia  , studio  za  video  na  luninga , wahandisi  wa  sauti, wazalishaji , wasambazaji  na   wauzaji  wa   kanda  za  muziki.
Je, unahisi  una  kipaji  cha  Kuimba ??
 Fanya  hivi :  Ni  rahisi  tu. Unakwenda  studio  na  wimbo  wako, unamweleza  mwenye  studio—Producer.  Una  REKODI.  {Siyo  lazima  ujue  kupiga  vyombo  vya  muziki }. Kuuza   na  Kusambaza  nakala  atakueleza   Producer. Anza  na  single  kisha  ALBAMU. We  imba  soko  lipo. Siyo  kwamba  wasanii  wote  wa  muziki  unaowajua  wanaweza  kuimba  vizuri  zaidi yako. Unaweza  kuwazidi  wengi  tu, ni  kwa  kuwa  hujaamua  kufanya  hivyo. JIAMINI   !!  UNAWEZA  VIZURI  SANA !! Imba  muziki  wa  kidunia {circular  music }  au  wa  kidini { religious music } kama  wewe  ni   mtu  wa  imani.
Bila  shaka  mtakubaliana   nami  kuwa   katika  sanaa, muziki  ni  eneo  lenye  kupendwa  na  watu  wengi   zaidi.

Mfano  wa  wanamuziki  waliofanikiwa   katika  Sanaa   hii  ya  muziki ni  Diamond { Tanzania } , Mzee   Yusufu { Tanzania}, Elton  John ,  Whitney   Houston n.k.

Japo  kila  mtu  anaweza, lakini siyo wote  tunapenda  kufanya  biashara. Mwingine   ukimpeleka  katika  uimbaji  kwa  mfano  au  maigizo , anafurahia  na  kujisikia  kafika  kuliko   kufanya  biashara.
 Hivyo  ndivyo  tulivyo.Mtu  unatakiwa  kufanya  kile  unachokipenda  na   kukifurahia. HAPO  UTAFIKA  MBALI.

Katika  Sanaa  kama  ilivyo  katika  biashara , kuna  vitu  vingi  vya  kufanya.Angalia  Kipaji , upenzi , soko  na   mazingira    mengine ya  Kiutendaji  kwa   ujumla.




Mfano wa wanamuziki waliofanikiwa katika Sanaa hii ya muziki ni Diamond  { Tanzania } , Mzee Yusufu { Tanzania}, Elton John , Whitney Houston n.k. Japo kila mtu anaweza, lakini siyo wote tunapenda kufanya biashara. Mwingine ukimpeleka katika uimbaji kwa mfano au maigizo , anafurahia na kujisikia kafika kuliko kufanya biashara. Hivyo ndivyo tulivyo.Mtu unatakiwa kufanya kile unachokipenda na kukifurahia. HAPO UTAFIKA MBALI. Katika Sanaa kama ilivyo katika biashara , kuna vitu vingi vya kufanya.Angalia Kipaji , upenzi , soko na mazingira mengine ya Kiutendaji kwa ujumla.










No comments:

Post a Comment