Simu
yako ni nguvu kubwa sana ya kukuwezesha kuwafikia wateja wengi na
kuwauzia pia. Itumie simu yako kama kifaa cha masoko na mauzo kwa
kuwasiliana na wateja wako kabla na baada ya kununua.
Kila
mteja anayefika kwenye biashara yako au anayejibu kutokana na matangazo
yanayotolewa na biashara, taarifa zake zinapaswa kuhifadhiwa. Hifadhi
namba zao za simu na tengeneza mpango wa kuwa unawapigia simu wateja
wako.
Kwa
wale ambao hawajanunua wapigie kuwaeleza manufaa ya kile unachouza na
kuwashawishi kuja kununua. Kwa ambao wameshanunua wapigie kujua
wanaendeleaje na kile walichonunua kimewafaaje.
Kwa kutumia simu yako vizuri utaweza kuwafikia wateja wengi na kuuza zaidi.
Njia
bora ya kuandaa mpango huu wa simu ni kurusha matangazo ambayo
yanawataka wateja wako kupiga simu, kutuma ujumbe au kuja kwenye
biashara yako. Na mteja akishakutafuta, basi tunza mawasiliano yake,
hasa simu na hapo utaendelea kuyatumia kwa masoko na mauzo zaidi.
No comments:
Post a Comment