“In
the new world of sales, being able to ask the right questions is more
valuable than producing the right answers. Unfortunately, our schools
often have the opposite emphasis. They teach us how to answer, but not
how to ask.” ― Daniel H. Pink
Kwenye
ulimwengu mpya wa mauzo, kuuliza maswali sahihi ni bora kuliko kuwa na
majibu sahihi. Kwa sababu tayari mteja anajua mengi zaidi, jukumu lako
kama muuzaji ni kuuliza maswali yatakayokupa wewe fursa ya kumjua mteja
zaidi.
Lakini
kwa bahati mbaya sana, elimu ya darasani iko kinyume na hili. Miaka
yote ambayo tumekaa shuleni tumekuwa tunafundishwa jinsi ya kujibu
maswali ili kufaulu mtihani. Hivyo unakuwa vizuri sana kwenye kujibu
maswali, lakini unapofika mtaani unakuta tayari kila mtu ana majibu.
Hivyo elimu ya darasani inakwama hapo.
Ili
kupiga hatua kwenye kitu chochote unachofanya kwenye maisha yako,
jifunze jinsi ya kuuliza maswali sahihi, maswali ambayo yatakupa nafasi
ya kumjua mtu zaidi na mahitaji yake, ili uweze kumhudumia zaidi.
Kadiri
unavyoweza kuuliza maswali sahihi na kusikiliza kwa makini majibu
yanayotolewa, ndivyo unavyoweza kujifunza na kujua hatua sahihi za
kuchukua.
No comments:
Post a Comment