Kuna
wakati tunakutana na mabadiliko makubwa kimaisha kwenye afya zetu.
mabadiliko haya yanaweza kutuyumbisha sana kama hatuna msingi sahihi
tunaouishi. Mfano ni pale mtu anapopata ulemavu wa mwili ambao unaathiri
maisha na hata kazi za mtu. Wengi huvurugwa sana na mabadiliko ya aina
hii, kitu ambacho hupelekea maisha yao kudorora na hata kufa mapema.
Wastoa
wanatupa njia sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya aina hii, kwa
kutuambia tunapaswa kufikiria na kutumia kile tulichonacho na siyo
kuangalia tumekosa nini. Kama umepata ulemavu wa miguu, kumbuka bado una
mikono, macho, masikio, na viungo vingine, ambavyo kama utaweza
kuvitumia vizuri maisha yako yatakuwa bora.
Mmoja
wa wanafalsafa wa Ustoa, Epictetus, ambaye alikuwa mwalimu bora sana wa
falsafa hii, alikuwa mtumwa. Katika maisha yake ya utumwa, aliumizwa na
kupata ulemavu wa miguu. Hili lilimpa ulemavu wa maisha, lakini
hakuruhusu ulemavu huo uathiri maisha yake, aliangalia mambo gani
mengine anayoweza kufanya, kama kujifunza na kufundisha falsafa na siyo
kuangalia alichokosa.
Somo
muhimu la kuondoka nalo hapa ni usiweke nguvu zako kwenye yale
uliyokosa au kupoteza, badala yake weka nguvu zako kwenye yale uliyonayo
na jinsi unavyoweza kuyatumia kwa ubora zaidi.
No comments:
Post a Comment