Kama
kipato chako ni kidogo na hakitoshelezi, tatizo lako kubwa ni moja,
unauza kidogo. Na ili kuondoka kwenye hali hiyo ya kipato kidogo na
kisichotosheleza unahitaji kuchukua hatua moja; KUUZA ZAIDI.
Usiniambie
wewe umeajiriwa na hivyo huwezi kuuza zaidi, kumbuka kuna kitu ambacho
unamuuzia mwajiri wako, sasa muuzie hicho zaidi. Mfano moja ya vitu
unamuuzia mwajiri wako ni muda wako. Hivyo kuna muda wa makubaliano wa
kufanya kazi kwa siku na kwa juma. Sasa wewe muuzie mwajiri wako muda
zaidi, kwa kuweka muda wa ziada kwenye majukumu ambayo ni muhimu kwa
mwajiri lakini yanakosa muda wa kufanyika. Kadhalika kwenye ujuzi na
uzoefu wako, ambavyo ni vitu vingine unavyomuuzia mwajiri wako, jiulize
ni wapi mwajiri ana uhitaji au changamoto na wewe unaweza kusaidia
zaidi, kisha mshawishi akupe nafasi hiyo kwa mbinu za mauzo ambazo
umejifunza.
Kila mtu anaweza kuuza zaidi, na hilo ndiyo suluhisho la kifedha kwa kila aliyekwama.
Unaweza
kuuza zaidi kwa wateja ulionao sasa, hapa unawapa bidhaa au huduma
ambayo hukuwa nayo awali. Ni njia rahisi kuanzia kwa sababu wateja
ulionao tayari wanakujua hivyo hawana wasiwasi sana na wewe.
Lakini
pia unaweza kuuza zaidi kwa kuwafikia wateja wapya. Hapa unatafuta
wateja ambao bado hawajanufaika na bidhaa au huduma zako kisha
unawashawishi wanunue, hivyo unaongeza wateja na mauzo pia.
Kwa
vyovyote vile, kila wakati kazana kuuza zaidi, kwa wateja ulionao sasa
wauzie zaidi ya wanavyonunua sasa na pia wafikie wateja wapya ambao
hawajawahi kununua kwako.
No comments:
Post a Comment