Upi mkakati wa masoko unaofanyia kazi wa biashara yako ?
Biashara
ni wateja, bila ya wateja, haijalishi una bidhaa au huduma bora kiasi
gani, huna biashara. Na njia pekee ya kuwaleta wateja kwenye biashara
hiyo ni mkakati wa masoko.
Wafanyabiashara
wengi wadogo huwa hawajisumbui kabisa na masoko. Huwa wanaendesha
biashara zao kwa mtazamo wa kizamani kwamba ukijenga biashara wateja
watakuja wenyewe. Lakini zama hizi ambazo wafanyabiashara ni wengi,
hakuna mteja atakayekuja kwako, bali unapaswa kuwatafuta wateja.
Unawatafuta wateja kupitia mpango mkakati wa masoko unaokuwa nao kwenye biashara yako.
Hii
ni kusema kwamba ili biashara yako ifanikiwe, lazima iwe na mkakati wa
masoko, ambao unawatambua wateja wa biashara hiyo, kuwafikia kule waliko
na kuwashawishi kununua.
Mkakati wako wa masoko unapaswa kuzingatia vitu vinne muhimu sana;
- Kuwatabua wateja sahihi wa biashara yako, wale ambao wanaweza kunufaika na bidhaa au huduma unazotoa.
- Kutambua vitu vitatu vinavyokutofautisha wewe na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama yako. Kama huna utofauti wowote na wafanyabiashara wengine, hakuna sababu ya mteja kuja kwako.
- Mchakato sahihi wa ufanyaji wako wa biashara, jinsi mteja anavyohudumiwa na hatua zote zinazochukuliwa kwenye biashara yako.
- Uhakika unaowapa wateja wako. Wateja wamepata fedha zao kwa shida, hawataki kuzipoteza, hivyo wanahofia sana kufanya manunuzi mapya. Unapaswa kuwapa uhakika kwamba wakinunua kwako hawapotezi fedha bali wanapata thamani.
Tengeneza
mkakati wako wa masoko ambao unajumuisha vitu hivyo vinne na utaweza
kuwafikia wateja wengi na kuwashawishi kununua kwako.
No comments:
Post a Comment