Kwa wafanyabiashara na
wajasiriamali maana kuu
ya biashara zote
ziwe ni za
mjasiriamali mdogo au muwekezaji
mkubwa ni “ KUTATUA
MATATIZO YA WENGINE
“. Tunasema mtu
fulani kafanikiwa kimaisha. NI
TAJIRI ! .Ana
pesa nyingi. Naam ! Ni kweli
kafanikiwa , lakini amefanya nini
kupata pesa hizo ?
SIRI NI HII
:
Katatua matatizo ya
watu ! Naam , ndiyo ukweli. Hakuna njia
ya mkato !! BUNI
shughuli inayotatua matatizo
ya watu, utapata PESA !!
Kabla
ya kuanza biashara
yoyote hata kama
ni ndogo kiasi
gani , FANYA UTAFITI wa
kutosha kama biashara
unayotaka kufanya kama
inaweza kuwatatulia watu
matatizo yao ? Kama
jibu ni NDIYO basi
ANZA MARA
MOJA , hakika UTAFANIKIWA . Kama
jibu ni HAPANA , LIACHE
MARA MOJA ! Huwezi kufanikiwa
kwa kuuza sweta
na Mwamvuli wakati
wa joto . Ukipata HASARA utalalamika,
“ Mie nina
mkosi ! “
Siyo
mkosi ! Bali umeshindwa kuwatatulia watu shida
zao. Watu hawana shida
ya sweta au
mwamvuli. Biashara yako imekosa
maana.Ulifikiri maana ya
biashara ni kupata
pesa ? La hasha ! Maana
na sababu ya
biashara yako ni
kutatua MATATIZO YA
WATU. Ndugu yangu
kupata Pesa ni
malengo yako tu. ANGALIA MAZINGIRA , NYAKATI, WATU,
Kwa mfano
kuna kijiji au
mji wana ukosefu
wa mafuta ya
taa. Karibu watu 200
katika kijiji hicho
au mji huo wanalazimika
kusafiri mamia ya
kilometa kufuata mafuta
ya taa katika
kijiji kingine au
mji mwingine. Kama utaleta
duka lenye kuuza mafuta
ya taa hapo . NINI
KITATOKEA HAPO ? JIBU
UNALO : NI KUPATA
PESA .
ANGALIZO
:
Usiseme unataka kufanya
biashara YOYOTE ile kwani kusema kwamba
unataka kufanya biashara
yoyote ile BILA
YA KUFANYA UTAFITI NI
KUPOTEZA MWELEKEO ndugu
yangu kwa kuwa
utakuwa HUJUI UNATAKA
KUFANYA NINI , Watu wana
shida gani hapa ?au
eneo unaloishi ? Wanahitaji
nini ? Nini hawana
?. Kama hujui cha
kufanya hakuna kitu
utakochofanya. HILI NI TATIZO
LA WATANZANIA WENGI !!
WAZO + UTAFITI + MTAJI== BIASHARA
KWANINI UTAFITI
NI MUHIMU KABLA
YA BIASHARA ?
Kutofanya utafiti
ni chanzo cha
biashara nyingi kuanguka
au kuharibika.
Utafiti ni
moja ya sababu
zilizowafanya Wazungu wafike
hapo walipo leo. Wao wamewekeza
zaidi kwenye UTAFITI
kuliko kitu chochote.Je, unaifahamu JAPAN ? K una
wakati maendeleo yake
yalikuwa kama Tanzania. Lakini baada
ya kuwekeza kwenye
UTAFITI , leo ni ya
tatu duniani kwa
uchumi. Leo hii nchi
ya CHINA ina
nguvu kubwa kiuchumi. Ni
tishio duniani .Ni matokeo
ya kuwekeza katika
UTAFITI.Hizo ni nchi ,
lakini UTAFITI unahitajika
sana pia kwa mtu binafsi
kwa ajili ya
maendeleo yake.
Unapofanya UTAFITI
utajua watu wanahitaji
nini ? Nini hawana ?Baada
ya kuwaza fanya
UTAFITI . Hata kama utatumia
miezi , miaka katika utafiti wako. Hakika utakachofanya hapo
baada ya UTAFITI , watu watakubali , watakuheshimu. Usikurupuke tu
kwa kuiga fulani
alifanya hivi akapata
pesa , nawe unaingia.
Mh ! Hatari ndugu
yangu ! Vitu vya
kuigilizia havimfikishi mtu
mbali . USIIGILIZIE, JIFUNZE KISHA
LIPA GHARAMA NA
UTOE VYA KWAKO. Watanzania wengi
wanapenda vitu bwelele , vya
rahisi rahisi hawapendi
kulipa gharama !
JITAMBUE : Nataka utambue
kitu muhimu kwamba
wewe ni wa
pekee katika kila kitu
hapa duniani. Uliumbwa kwa
jinsi ya ajabu
na ya kutisha
{ ZABURI 139 : 14 }, hakuna aliye
kama wewe ulimwenguni
kote , kwa hiyo usijaribu
kuwa fulani. Unaweza kutamani
jinsi watu fulani
wanavyofanya mambo yao
lakini usisahau kwamba wapo
wanaotamani jinsi unavyofanya
wewe pia. Kama bado
hujawaona subiri kidogo
wanakutafuta. Mtu mmoja mwenye
hekima akasema , “
washa moto kwenye
kichwa chako , watu
lazima watakuja tu
kuona jinsi unavyowaka “ Watu hawana
haja ya kuona
marudio, wanataka kuona vitu
vipya. Nitaandika makala
yenye kichwa “ USIIGE BALI
JIFUNZE NA TOA
CHA KWAKO “ ndani
ya blog hii
MAISHA NA MAFANIKIO
BLOG. Endelea kutembelea blog
hii ujifunze siri za
kufanikiwa katika maisha ! UNAWEZA KUFANIKIWA ! HUJACHELEWA !!
JE,
NITAFANYA BIASHARA GANI ?
Lazima
ujiulize kwamba unataka
kufanya biashara gani ? Fanya
UTAFITI wa kutosha
kama biashara unayotaka
kufanya itakuwa na manufaa
, au
laa ! Njia ya
kukusaidia ndugu yangu
mtanzania kuamua ufanye
biashara gani ni
katika utafiti wako
ujiulize maswali yafuatayo :--
{1}. Umewahi
kufanya kazi au
biashara gani ?
{2}. Umesomea nini ?
{ 3}. Vipaji
vyako ni vipi ?
{4 }. Ni
biashara ipi au
kazi ipi unapenda
zaidi kuliko nyingine
na kwa sababu
gani ?
{5}. Je,
jambo ninalotaka kufanya
litaleta faida ?
{6}. Je, litawaondolea watu
matatizo ?
{7}. Je, litabadilisha maisha
yangu kwa kiwango
gani ?
{8}.Je, watu
waliowahi kufanya kama
ninalotaka kufanya wakoje ?
{9}.J e, watu
wanasemaje ?
{10 }.Je, eneo
linafaa kufanyia shughuli
hii ?
Orodha
ni ndefu . Ukisha jiuliza
maswali haya chukua
kalamu na karatasi
uandike maswali yako
na kuyajibu.Ukikagua maswali
na majibu yako
utagundua shughuli unayoipenda , unayoiweza na
una kipaji na
hiyo ndiyo inayokufaa. Ukishachagua biashara
unayoipenda ni rahisi
sana KUFANIKIWA kwani
shughuli utazifanya kwa
hiyari bila kujilazimisha.
USHAURI WANGU
: Kama
utakuwa bado hujafikia
uamuzi baada ya
hapo basi tafuta
na wasiliana na
washauri ili mbadilishane
mawazo na ufundishwe
jinsi ya kuamua
ufanye biashara gani .
MAMBO MUHIMU
YA KUFANYIA UTAFITI
KABLA YA BIASHARA
{1}. Kujua siri
ya biashara unayotaka
kufanya ili upate
mbinu za kupata
mafanikio.Unaweza kupata siri
au kujifunza mbinu
kutoka kwa watu
wanaofanya biashara kama
unayotaka kufanya.Suala hili
ni gumu sana
kwani wafanyabiashara wengi
huwa wanaficha siri
za biashara zao
ili kulinda wasizidiwe
maarifa na washindani
wao.Unaweza kuipata siri
hiyo kama utakwenda
kupata ushauri toka kwa
mfanyabiashara ambaye yuko
mbali na mahali
unapofanyia biashara , au tafuta
ushauri kwa wataalamu
wa mambo ya
biashara.
{2}.Fanya utafiti
wa soko la
bidhaa unazouza au
unazotarajia kuuza. Jiulize ,
je, bidhaa unazotaka
kuziuza zina soko ? Utawauzia watu
gani na utauzaje ? Kama wewe ni ni
mzalishaji , una mazao / bidhaa
unapaswa kuuza kwa
jumla , mchanganyikio ama rejareja ? Je, utatangaza vipi
bidhaa zako ? Nitafundisha kwa
kirefu katika makala
yenye kichwa “
TANGAZA KILE ULICHONACHO /TANGAZA HUDUMA AU
BIDHAA ZAKO “
{3}. Tengeneza bajeti
yako kwa kuorodhesha
vitu vinavyohitajika na
gharama zake ili
kuweza kuanzisha biashara
yako. Vitu hivyo
ni :--
{a}.Gharama
za Kujenga au
kupanga ofisi.
{b}.Gharama
za Leseni ya biashara.
{c}.Makadirio
ya KODI toka
TRA.
{d}.Gharama
ya vifaa vya
ofisi yaani , Samai, makaratasi, mitambo, mashine, n.k.
{e}.Manunuzi
ya malighafi au
bidhaa za kuanzia
biashara.
{f}.Idadi
ya wafanyakazi na
gharama za mishahara
yao.
{g}.Gharama
nyinginezo kama vile
umeme , maji, n.k.
{4}.Unatakiwa kujua
ni MTAJI kiasi
gani unahitajika kuanzisha
biashara yako. MTAJI HUO
utaujua baada ya
kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika
kipengele namba { 3} hapo
juu. Gharama hizi ni za mwaka
ule wa kwanza
wa kuanzia biashara.
{5}.
TAFUTA MTAJI
Mtaji unaweza
kupatikana kutoka kwenye
vyanzo vifuatavyo :
{a}. Akiba au
mshahara.
{b}.Msaada
au mkopo kutoka
kwa ndugu na
jamaa.
{c}. Kuingia
ubia na mtu mwenye
mtaji
{d}. Mkopo
toka baadhi ya
asasi kama vyama
vya akiba na
mikopo {SACCOS },NGO za kifedha
isipokuwa Benki kwani
hizi huwa hazitoi
mikopo kwa mtu
anayeanzisha biashara.
Nitafundisha kwa
kirefu katika makala
yenye kichwa “ NI VIPI
UPATE MTAJI ? Pia
nitafundisha “ UNASHINDWA KUPATA
MKOPO BENKI ? NJIA HIZI
HAPA.
“ Kuna
njia moja tu
ya kujitengenezea pesa
nyingi , nayo ni biashara
yako mwenyewe “ { J.PAULO
GETTY }.
Asante msomaji
wangu kwa kusoma
makala hii nzuri
yenye kuelimisha ! Tembelea
“ MAISHA NA
MAFANIKO BLOG” kwa
kujifunza mambo mapya
kila siku !! USIKATE
TAMAA , UNAWEZA KUFANIKIWA
!! Mungu
Akubariki !!
Makala hii
imeandikwa na MWL
JAPHET MASATU . Ni Mwl
wa Saikolojia, Elimu ya
Maisha na Mafanikio , Biashara / Ujasiriamali.Anapatikana kwa namba
+ 255 716 924 136 / + 255 755
400 128 / + 255
785 957
077.
Kama
una lolote unataka
kuchangia mawazo , ushauri kuhusiana
na mada yetu
hii . Karibu
sana.
Kama
una
swali lolote kuhusiana
na mada yetu hii msomaji
wangu uliza !!!
No comments:
Post a Comment