Wednesday, June 25, 2025

NAMNA YA KUPANGILIA RATIBA YA WIKI HI KIPOROFESSIONAL --------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924136

 Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional Rafiki yangu mpendwa, salaam Miongoni mwa ujuzi muhimu sana ambao unahitaji ili kufanikisha malengo Yako ya mwaka 2025 ni ujuzi wa kuipangilia wiki yako. Wiki ni ndogo sana ila usipoipangilia vizuri inapotea na ukipoteza wiki nyingi mfululizo, mwisho wa siku unakuwa umeupot

Sasa ya nini uupoteze mwaka mzima wakati Kuna uwezekano mzuri tu wa kufanya makubwa kwa kuanza kitu kidogo kama kuipangilia wiki yako.

Anza wiki hii kuipangilia kila wiki yako.

Ni majukumu gani uliyonayo?

Ili kuipangilia wiki yako kiprofessional, anza kwa kujiuliza ni majukum gani yaliyombele yako kwa wiki inayofuata?

Kisha yapangilie kulingana na umuhimu. Majukumu ambayo ni ya muhimu zaidi yape kipaumbele kwanza.

Kwenye siku yako usipange vitu VINGI VYA kufanya. Ukiweza kuwa na vitu vitatu tu vinatosha, vikizidi visiwe zaidi ya sita. Hii itakusaidia kufokasi kwenye mambo machache ila utakayoyawekea NGUVU kubwa na kuyafanikisha pia.

Unavyoianza wiki yako pia, hakikisha wiki hii unapanga muda wa kujisomea vitabu. Inashangaza kuona kwamba watu wanapangilia mpaka muda wa kula ila hawapangilii muda wa kujisomea. Changamoto kubwa ni kwamba, tumbo likiwa na njaa huwa linapiga kelele. Ndiyo utasikia mtu anasema; “nina njaa“. Ila akili yako ikiwa na njaa haisemi. Ila ilipata utapiamlo wa akili, utazidi kuwa nyuma mara zote. Hivyo, fanya kadiri uwezavyo kuhakikisha kwamba, kila siku unapata muda wa kujisomea.

Pata kozi yoyote fupi. Online kuna kozi nyingi fupi. Kwenye ratiba yako weka muda wa kujifunza kozi yoyote fupi kuhusiana na eneo ambalo ungependa kulifahamu kwa undani. Inawezekana Hilo eneo tayari unalifahamy vizuri tu, lakini Kuna jambo moja au mawili unaweza kujifunza kuongezea au kutanua kile ambacho tayari unajua.

Siwezi moja kwa moja kukwambia ujifunze kozi gani, ila fahamu ya kuwa kozi za namna hii zipo nyingi. Ni juu Yako kujua wapi unahitaji KUWEKEZA NGUVU ili uwe Bora zaidi. Maeneo ya kujifunza na kupata kozi kama hizi pia ni mengi, mfano skillshare, Udemy, Coursera, learn digital with Google, na nyingine nyingi kama zinavyoonekana kwenye picha hapo chini.


No comments:

Post a Comment