Sunday, May 18, 2025

MAKALA : NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA NDOTO ZAKO UMEIBEBA WEWE MWENYEWE NA SI MTU MWINGINE--------NA MWL. JAPHET MASATU -------CALL / SMS / WHATSAPP + 266 716 924 136

 Kakaa/Dadaa Yangu...

‎

‎Umesahau wewe ni nani.

‎

‎Umesahau kuwa ndani yako kuna nguvu ya kutikisa dunia.

‎

‎Umejikatia tamaa kimya kimya.

‎

‎Kila siku unasema *labda mimi sina bahati.*

‎

‎Umeanza kuamini maisha ni magumu na huwezi kubadilisha chochote.

‎

‎Lakini ukweli ni huu: UNA NGUVU YA MIUJIZA NDANI YAKO  ,  

‎

‎Unaitumia vibaya.

‎Au hujui hata ipo.

‎

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyeanzisha biashara kwa buku 5 akafika juu?

‎

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyefeli shule lakini leo anaajiri waliopata division one?

‎

‎Ulishawahi kumuona mtu aliyetelekezwa, akasota, lakini leo anajenga nyumba yake?

‎

‎Wote hawa hawakuwa na miujiza ya mbinguni.

‎

‎Walitumia nguvu ya ndani waliyoamka nayo kila siku.

‎

‎Na hiyo nguvu wewe pia unayo.

‎

‎Lakini... unaitumia kuskroll TikTok.

‎

‎Unaitumia kulalamika.

‎

‎Unaitumia kutafuta huruma badala ya suluhisho.

‎

‎Una nguvu lakini hauna mwelekeo.

‎

‎Miujiza sio kupasuliwa mbingu.

‎Sio malaika kushuka.

‎

‎Miujiza ni pale mtu wa kawaida anapoamua kuamka na kuchukua hatua isiyo ya kawaida.

‎

‎Ni pale mtu anapoamua kuamka kabla ya wengine.

‎Kuanza kuandika ndoto zake.

‎

‎Kuanza kusoma vitabu badala ya magazeti ya udaku.

‎Kuanza kuomba kazi kwa bidii badala ya kuomba msaada.

‎Miujiza ni matokeo ya msimamo.

‎

‎Suluhisho Lipo. Na Lipo Ndani Yako.

‎

‎Badilisha namna unavyofikiri.

‎Acha kusema “sina mtaji” sema “naanza na hiki kidogo.”

‎

‎Acha kusema “nimechelewa”  sema “leo ndiyo siku yangu ya kwanza.”

‎

‎Acha kujificha nyuma ya visingizio.

‎Toka uvunguni.

‎Toka kwenye comfort zone ya umaskini wa mawazo.

‎

‎Chukua hatua.

‎Anza leo.

‎Fanya kitu.

‎

‎Kwa sababu NGUVU YA MIUJIZA UMEIBEBEA WEWE MWENYEWE.

‎

‎Bado namkumbuka....

‎

‎Kuna bro mmoja alichoka na maisha.

‎Alikuwa hana kazi. Hana mtaji. Hana cheti.

‎

‎Alikaa chini akaandika: “Mwaka huu lazima niwe mtu mwingine.”

‎

‎Akaanza kuuza karanga mtaani.

‎

‎Akaweka akiba ya mia mia.

‎

‎Alikuwa anasoma vitabu alivyokopeshwa.

‎

‎Alifungua YouTube kujifunza marketing.

‎Miaka mitatu baadaye...

‎

‎Ana biashara ya kuuza nafaka.

‎Ana familia.

‎Ana ndoto mpya kila mwaka.

‎

‎Aliniambia hivi:

‎

‎“Miujiza haikunitokea, niliitengeneza mwenyewe.”

‎

‎Sasa Wewe Una Sababu Gani Ya Kukata Tamaa?

‎

‎Huna sababu.

‎

‎Una kila sababu ya kusimama.

‎

‎Chukua kalamu na kuandika ndoto zako.

‎

‎Zima data saa tatu usiku na kupanga kesho yako.

‎

‎Na anza kutenda miujiza ya kweli kupitia nguvu yako ya ndani.

‎

‎Kumbuka: Miujiza Haiporomoki.

‎

‎Miujiza hutengenezwa.

‎

‎Na hutengenezwa na watu kama wewe.

‎

‎Watu wa kawaida lakini walioamua kuishi maisha ya ajabu.

 

ENDELEA   KUTEMBELEA    BLOG  HII     UTAJIFUNZA  MENGI   "  MAISHA    NA  MAFANIKIO ( LIFE  &   YOU  )  BLOG  "  PENDA    KUNUNUA    VITABU  NA    KUVISOMA   UTAGUNDUA  SIRI  NYINGI   ZA  DUNIA  HII.

No comments:

Post a Comment