Watu wengi zaidi hasa VIJANA, wanaonekana kupoteza SHABAHA yao au LENGO lao katika MAISHA. HUISHI maisha ya hapa na pale WAKIFUKUZIA MANUFAA YA MUDA MFUPI. SABABU yao pekee ya kufanya KAZI ni ili kupata HUNDI YA MALIPO kwa madhumuni ya kukidhi MATAMANIO YA KUFANYA ANASA NA STAREHE.Utafutaji wa FURAHA wa namna hii hauwezi kumfkisha mtu popote.
Bila kujali zama tunazoishi , dhati ya UBINADAMU inabaki kuwa ile ile. NI KUTAFUTA MAISHA yenye KUPENDEZA na KUFANIKIWA kufikia hali ya KUTOKUFA KWA KUKIACHIA KIZAZI KIJACHO jambo ambalo LITAENDELEA KUKINUFAISHA.Tunapaswa kutafuta MAISHA yaliyotimia ili siku moja tuweze kusema
"NILIFANYA KAZI KWA BIDII , NILITENDA MAMBO YENYE MANUFAA , NA NINAJISIKIA FURAHA."
Baadhi ya watu wanaweza wasikubaliane na mimi kuhusu WAZO HILI , LAKINI naamini kwa dhati kabisa kwamba njia hii ya KUJIBIDIISHA KATIKA MAISHA NI BORA ZAIDI KULIKO ILE NJIA RAHISI. Watu wenye uzoefu mkubwa zaidi wanaweza kuelewa kile ninachokisema. KWA BAHATI MBAYA , WATU WA AINA HIYO HAWAKO TAYARI KUTOA MAONI YAO KUHUSU MAISHA. SABABU ambayo kwa kawaida wamekuwa wakiitoa ni kwamba, WAKATI umebadilika na HADITHI zao za kale hazina mchango wowote KWA VIJANA WA LEO. LAKINI kama tukizungumza kwa dhati ya moyoni , WATU WENGI WATAJITOKEZA kuzungumzia kile TUNACHOAMINI.
KWA KUHITIMISHA NASEMA " MFUMO wa MAISHA RAHISI MWANZONI UNAWEZA KUONEKANA KAMA WA KUCHANGAMSHA NA KUVUTIA HATA HIVYO HUFIKA WAKATI SISI SOTE TUKATAMANI KUWA NA SHABAHA YA/ LENGO LA JUU ZAIDI KIMAISHA.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
No comments:
Post a Comment