MAISHA ni mchezo wa kuigiza ambao kila mmoja wetu ana nafasi mahususi ya kushiriki kama MWIGIZAJI. Hata hivyo tunachofanya katika MAISHA yetu wenyewe, ni zaidi ya KUSHIRIKI tu kama WAIGIZAJI----hakika tunaandika Mchezo wenyewe. TOFAUTI na Mchezo ambao tayari tunafahamu kwamba HATIMA yake ni nini , HATIMA YA MAISHA YETU TUMEISHIKILIA MIKONONI MWETU WENYEWE .
BAADHI YA WATU huamini kwamba HATIMA ya MAISHA YETU huwa tayari imeamuliwa hata KABLA YA KUZALIWA KWETU. MIMI SI KAMA hao wanaoamini hivyo. NINACHOAMINI MIMI NI KWAMBA UPO UWEZEKANO WA KUBADILI HATIMA YA MAISHA YETU WENYEWE KWA KUBORESHA NAMNA TUNAVYOZITUMIA FIKRA ZETU.
BADALA YA KUISHI KWA KUTEGEMEA KUDURA TULIVYOPANGIWA , Tupanue FIKRA ZETU ili zituwezeshe KUANDIKA MCHEZO WA MAISHA YETU TUKIWA TUMEJIPANGIA NAFASI TUNAZOPENDELEA KUSHIRIKI KATIKA MCHEZO HUO. Kadiri tutakavyoweza kufanya jambo hili mapema ndivyo tutakavyoharakisha mwanzo wetu sisi wenyewe wa kutawala kikamilifu kila kipengele cha MAISHA yetu ya kila siku.
KATIKA MCHEZO UITWAO MAISHA KUNA TOFAUTI KUBWA SANA BAINA YA WALE WALIOJIPANGIA WENYEWE NAFASI ZA UHUSIKA KWENYE MCHEZO HUO , NA WALE WANAOISHI MAISHA YA MAJALIWA YASIYO NA LENGO.
FURSA mbalimbali zinatusubiri katika mambo mengi yanayohusu MAISHA YETU. Tuna UWEZO WA KUZIPATA FURSA HIZO KAMA TUKIPANIA. HATA HIVYO tusipokuwa na DHAMIRI pamoja na MALENGO BAYANA KATIKA FIKRA ZETU , haitakuwa rahisi kufaulu hata katika FURSA zile za kawaida na bayana kabisa.
KANUNI YA MAFANIKIO----JIPATIE NAMBA KATIKA MCHEZO UITWAO MAISHA.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment