Saturday, September 20, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI--- KUNUNUA HISA.

                                          KUNUNUA    HISA
Kununua   Hisa  ni  njia   nyingine  ya   KUWEKEZA. Faida  ya   kununua  HISA   ni  kwamba  thamani  ya   FEDHA  zako  katika   HISA  hukua   kutokana  na    ukuaji   wa   FAIDA   YA   KAMPUNI.

Kwa   mfano,  umenunua  HISA  1,000  za   kampuni   fulani   kwa   bei  ya  Tshs  300   kwa  HISA   utalipa   TShs  300,000/=  thamani   ya   HISA   zako   zile   zile   zikipanda   mara   mbili     ukiziuza  utapata  TShs   600,000 /= .
 FAIDA nyingine   ya   kuwekeza  katika   HISA  ni    kupata  GAWIO. Makampuni   mengi    hutengeneza  mahesabu    kila   baada  ya   miezi   3  na   kutoa   GAWIO   kwa    wenye   HISA.  

 HASARA  ya   kuwekeza  katika   HISA  kuna   wakati   makampuni  hupata  HASARA   na  hivyo  kutotoa  GAWIO  na    HISA  zinaweza  kushuka  thamani.

No comments:

Post a Comment