MIPANGO YA KUSTAAFU
Maandalizi kwa ajili ya MAISHA YA UZEENI ni lazima yaanze tangu ukiwa KIJANA na sio mpaka uanze KUZEEKA. MAISHA YASIYO NA MIPANGO ENDELEVU mpaka unapofikisha UMRI WA MIAKA 65 hayawezi KUFANIKIWA GHAFLA pindi unapostaafu.
ANZA SASA kujiwekea AKIBA na kuwekeza kwa ajili MAISHA YAKO YA BAADAYE KUANZIA SASA.
HAUTAKIWI KUSUBIRI mpaka upate PESA ndio uanze MIPANGO YA KUSTAAFU , bali unatakiwa UWE na mipango KABLA ili utakapopata KAZI AU PESA uwe na kazi ya KUITEKELEZA TU MIPANGO ambayo tayari ilishapangwa.
SIRI YA MAFANIKIO: Watu wenye MIPANGO kabla ya kupata PESA HUFANYA MAMBO MAKUBWA sana na mazuri pindi wanapopata PESA kuliko wale WANAOSUBIRI na KUANZA MIPANGO baada ya kupata PESA AU PINDI PESA ZINAPOKUWA TAYARI MEZANI.
Hata kama unakaribia KUSTAAFU au tayari umeshastaafu bado unayo nafasi. Kamwe huwa hakuna kuchelewa katika kufanya MABADILIKO chanya katika maisha yako. NI BORA KUCHELEWA KULIKO KUTOFANYA KAMWE { Better late than never }.
Inakadiriwa kwamba ukiachana na kiwango cha kipato , zaidi ya 70% ya waajiriwa wanakuwa wameishiwa kabisa kabla ya mwisho wa mwezi. Mara nyingi wanaanza maisha ya MADENI mpaka MSHAHARA mwingine unapokuwa tayari. Hata kama wewe ni miongoni mwa hawa bado una uwezo wa KUJIWEKEA AKIBA kwa ajili ya maisha yako baada ya kustaafu.
MAISHA UNAYOISHI SASA YANAASHIRIA AINA YA MAISHA UTAKAYOISHI BAADAYE.
Mungu Akubariki kwa Kusoma Makala hii.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment