UWEZO WETU wa KUFANIKIWA katika Safari yetu ndefu ya MAISHA hautegemei uwezo wa AKILI peke yake.
Tunapofikiria kuhusu UWEZO WA MTU hatuna budi kujumuisha pia UTASHI WAKE. Kama mtu ameshindwa kuishinda NAFSI yake na kuamua kuchukua NJIA RAHISI bila shaka UWEZO wake kamili utakuwa pia UMEPUNGUZWA SANA.
UNAPOKUWA SHULENI utagundua ya kwamba kuna aina mbili {2} za WANAFUNZI :-
AINA YA KWANZA ni wale ambao hawana UWEZO SANA KIAKILI lakini hujitahidi sana SHULENI ili wahitimu wakiwa wamefanya vizuri katika MASOMO YOTE.
AINA YA PILI ni wale wenye AKILI NYINGI lakini hupenda STAREHE na katika MUDA wao wote chuoni huwa hawana nafasi hata ya kufungua kitabu.
HUYU wa pili angesema " yule MBUKUZI maefaulu Vizuri , lakini kama ningekuwa nimesoma kama yeye , ASINGEWEZA KUNISHINDA AU ASINGEWEZA KUFUA DAFU KWANGU ".
BAADA ya kuhitimu , yule mpenda starehe anakutana na rafiki yake mwingine mwenye MAFANIKIO katika biashara , na kusema " HAKUWA NA AKILI SHULENI. ALAMA ZANGU ZILIKUWA NZURI KULIKO ZAKE " akimaanisha kwamba kama YEYE angekuwa ndiye mwenye BIASHARA ile bila shaka angekuwa AMEFANYA VIZURI ZAIDI.
JE, LAKINI HUO NDIO UKWELI WENYEWE ?Kujisomea sana ni kuishinda ILE SEHEMU MOJA YA NAFSI YAKO INAYOTAMANI STAREHE ZILIZOPO-----KUJINYIMA SHEREHE NA HATA KUTAZAMA RUNINGA. BILA SHAKA PIA RAFIKI ALIYEFANIKIWA AMEJINYIMA MAMBO HAYO.
ILIMBIDI AJIZUIE NA TAMAA ZA STAREHE NA KUUTUMIA MUDA WAKE WOTE KWENYE SHUGHULI ZAKE. INAHITAJI UAMUZI MKUBWA ILI KUISHINDA NAFSI .
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment